Kwa nini tume inachelewa kutangaza matokeo Igunga? Vurugu zimeanza

Kutoka kwa habari za uhakika kutoka kwa mawakala waliopo Igunga. Jumla ya kula za CHADEMA ni nyingi kuliko zile za CCM. NEC inasuasaua kutangaza Kashinde kashinda. Nape amesambaza matokeo ya uongo kuonyesha CCM imeshaanda. Watu bado wengi wakisubili matoke...LOLOTE LINAWEZA KUTOKA!!
Hii tume ya uchaguzi inataka kutuletea vurugu hapa, iweje mpaka leo hawataki kutupa matokeo? waliahidi kutoa matokeo ndani ya masaa ishirini na nne. hapa lazimA KIELEWEKE.
 
Tatizo ni nini? Kama vipi si watangaze alieshinda vinginevyo watakaribisha fujo. Mbona wenzetu Zambia walitangaza nchi nzima ndani ya masaa 24. Sisi jimbo moja tunashindwaje? HIZI NI DALILI ZA WIZI ULIO WAZI
 
Naomba sisiemu wachakachue kura za igunga ili tupate sababu ya kuanzisha maandamano nchi nzima.!
 
na kama ungefanyika uchaguzi wa nchi nzima.nadhani kwa hali hiiii ingekuwa ni mwaka mzima...jamani CCM NI PROFESSIONAL KWA KUIBA KURA.
 
kwani hao magamba si washashinda, sasa kwanini wasitangaze?nawasikitikia wana IGUNGA kuwa wamejichimbia kaburi miaka minne tena, wameongeza idadi ya watu wanaosinzia bungeni na kusema ndio kwa kila kitu na kuendeleza kula pesa za walalahoi bila ya kuwatendea haki. Wao ndio waliotuponza kwenye swala wa dowans kwani walimchagua rostam ambaye sa hivi anachekelea mabilion aliyolipwa...
 
Wapiga kura walikuwa wangapi? Sidhani kama walifika hata 200,000! Vituo havikufika 500! Wastani wa wapiga kura 400 kwa kituo! Upigaji kura uliisha saa 10, kura zilianza kuhesabiwa, let's say, saa 11. Hata kama kungekuwa na watu wawili wawili wa kuhesabu kura kila kituo, kazi ya kuhesabu ingeisha saa 11.30, matokeo kwa kituo yangefika Halmashauri ya Wilaya latest saa 12, na hapo, nusu saa ingetosha kupata jumla ya kura zote. kazi hiyo ingehitaji mtu mmoja tu ambaye angefanya Data Entry na kuiprint ndani ya robo saa. Saa 1 usiku kila mtu angekuwa nyumbani kwake, aidha akifurahia ushindi, au akifuta machozi!

NEC inataka kuniambia kwamba iko slow kiasi hicho?
 
Matokeo igunga: Ccm 26,266 chadema 22,443
Haya matokeo ni toka jana sa sita usiku. kama hakuna mapya si ni kiashiria tosha kuwa wameshamaliza kuhesabu???kwanini sasa wasitangaze??tena kwa bahati nzuri wezi wameshinda c watangaze tu kama hakuna utata??
 
Diwani wetu Nanyaro, Mbunge wetu Lema, mpooooo? Tuliwaambia kuwa mnatwanga maji kwenye kinu mkabisha. Ukinda na uhuni wenu kisiasa utazidi kuwaumbua katika chaguzi zijazo........aha aha ahaaa.!!!!!!! IMEKULA KWENU.

Pamoja na yote.....poleni sana kwa kuangukia pua, ndio siasa. Next time...
 
Kwa kweli hapa vyama vitakuwa vimejifunza kuwa watu wanataka mabadiliko.
Kumbe yale matokeo aliyotoa Nape ni feki??
Ndio kwanza ninaelewa kuwa yale ya Nape ni feki. Kama ni ya uongo, Nape emekosa sifa za kuwa kiongozi wa CCM kwani ni wao CCM wenyewe pamoja na Timu (Tume) yao ya Uchaguzi wanaosisitiza kuwa ni kosa kutangaza matokeo kabla ya Tume. Sasa Nape kama kiongozi anataka tumweleweje? Magamba magamba tu! hata wakiyavua watabakia na makovu.
 
Back
Top Bottom