Kama sinema vile,jana muda wa saa kumi kasoro hivi mitaa ya Samora karibu na PPF House kibaka/mwizi alikuwa anafanya vitu vyake ghafla akakurupushwa na askari polisi mwenye sare na reflective jacket yake akaanza kumfukuza kupitia mtaa wa Mission, polisi akapigwa chenga kibaka katimua mpaka mitaa ya DMI na kuzama ndani na kuibukia bandarini.Wakati wote huo polisi alikuwa anamfukuza bila na kuwa na filimbi ambayo ingemsaidia kumtia nguvuni kiurahisi kama ilivyokuwa hapo zamani.Siku hivi vipi polisi hawabebi/vaa filimbi?