sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,022
- 5,254
Binadamu wote ni lazima tupitie kifo ikiwa ndio mwisho wa maisha yetu hapa duniani. Wakati wa uhai mtu unaweza kumiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika mahali tofauti tofauti ndani au nje ya nchi ya Tanzania. Kuondoka kwako duniani kwa njia ya kifo hakufanyi mali zako zipotee kwa kuchukuliwa na watu wasiokuhusu kwa kuwa tu hakuna usimamizi au mgawanyo sahihi. Uhamaji wa umiliki wa mali kutoka kwa marehemu kwenda kwa wapendwa wake walio hai ndiyo huitwa MIRATHI. Kufanikisha uhamaji huo, Bunge la JMT liliamua kutunga Sheria za Mirathi kuongoza na kusimamia ugawaji na usimamizi wa mali za marehemu.
A: NI SHERIA ZIPI ZINAZOSIMAMIA MAMBO YA MIRATHI TANZANIA?
👉Sheria za Kimila (Customary Laws)
👉Sheria za Kiislamu ikiwa ni pamoja na Quran na Sharia
👉Sheria ya Mirathi na usimamizi wa Mirathi, Sura ya 352 pamoja na kanuni zake,
👉Sheria ya urithi (The Law of Succession Act)
👉Pamoja na Sheria ya Mirathi ya India
B: NINI KIFANYIKE BAADA YA KIFO?
C: NI KINA NANI WANAORUHUSIWA KUOMBA USAJILI WA KIFO CHA MAREHEMU?
Muda ni ndani ya siku thelathini (30) kutokea tarehe ya kifo. Msajili wa vifo anaweza kuruhusu usajili ufanyike ndani ya miezi mitatu kutoka tarehe ya kifo ikiwa ataridhika na sababu za kuchelewa kusajili kifo ndani ya siku 30.
KIFO KINASAJILIWA WAPI?
Katika Ofisi za Msajili Mkuu wa vifo au katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya kifo kilipotokea ambapo kuna wasajili wa wilaya (RITA)
JE, NI MUHIMU KUELEZA SABABU ZA KIFO?
NDIYO. Sababu za kifo huandikwa na tabibu anayetambulika na serikali katika cheti cha sababu za kifo na cheti hicho huwasilishwa na tabibu huyo katika ofisi za msajili wa vifo wa wilaya – fomu hii inaweza kupewa kwa ndugu wa marehemu anayefuatilia usajili wa kifo.
D: JE NI MUDA GANI KISHERIA UTEUZI WA USIMAMIZI WA MIRATHI UNAWEZA KUOMBWA?
Kanuni za Sheria ya Mirathi (PAEA Rules) inaelekeza kuwa kipindi kinachoruhusiwa kuomba uteuzi wa usimamizi wa mirathi ni ndani ya muda wa miaka mitatu (3) kutoka tarehe marehemu alipofariki dunia.
Je, usimamizi wa mirathi unaweza kufanywa baada ya miaka mitatu (3) kupita?
NDIYO, inawezekana kuomba uteuzi wa usimamizi wa mirathi nje ya muda wa miaka mitatu kwa kueleza sababu zilizofanya maombi hayo yasifanyike ndani ya muda.
👉Ni vyema kupata huduma ya wakili kukusaidia kufanya maombi ya uteuzi wa usimamizi wa mirathi yanayofanyika nje ya muda. Ikiwa utahitaji msaada kwa hili, wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
E: NI SEHEMU IPI NI SAHIHI KUOMBA MAOMBI YA MIRATHI?
👉Mahakama ya Mwanzo – ikiwa mirathi inaombwa kwa sheria za kimila ama za dini ya kiislamu
👉Mahakama ya Wilaya – ikiwa mirathi inaombwa kwa sheria ya mirathi
👉Mahakama Kuu ya Tanzania – ikiwa mirathi ina utata kidogo juu ya sheria ipi inayopaswa kutumika kati ya sheria ya kimila, dini ya kiislamu au sheria ya mirathi
Utumizi wa Sheria hizo ni kwa kuzingatia hali ya kiimani na kimaisha ya marehemu kabla ya kifo chake, mfano kama marehemu alikuwa ni mtu wa kuzingatia mambo ya kimila ya kabila lake, basi mirathi yake itaombwa kwa mujibu wa sheria za kimila.
Naitwa Lusajo W. Mwakasege, Mwanasheria na Co-Partner wa Marm and Associates Advocates, namba yangu ya simu ni 0713-368153 (inapatikana whatsapp na telegram) na barua pepe yangu ni mwakasege@gmail.com. Tuanze somo letu:
A: NI SHERIA ZIPI ZINAZOSIMAMIA MAMBO YA MIRATHI TANZANIA?
👉Sheria za Kimila (Customary Laws)
👉Sheria za Kiislamu ikiwa ni pamoja na Quran na Sharia
👉Sheria ya Mirathi na usimamizi wa Mirathi, Sura ya 352 pamoja na kanuni zake,
👉Sheria ya urithi (The Law of Succession Act)
👉Pamoja na Sheria ya Mirathi ya India
B: NINI KIFANYIKE BAADA YA KIFO?
- Sajili kifo kwa msajili wa vizazi na vifo (RITA);
- Kikao cha ukoo kifanywe na uandikwe muhtasari wa kikao hicho pamoja na mahudhurio yakiwa na saini za waliohudhuria;
Kikao kinafanyika kwa ajili ya:- Kutambua majina ya warithi wa marehemu,
- Kutambua kama marehemu aliandika wosia (uonekane) au la kuhusiana na mali zake,
- Kutambua mali za marehemu na mahali zilipo,
- kutambua madeni ya marehemu anayodaiwa na anayodai,
- Kutambua sababu za kifo cha marehemu
- kutambua hali ya kiimani ya marehemu enzi za uhai wake;
- kutambua hali ya ndoa ya marehemu;
- Kutambua sheria na mahakama zitakazohusika na mirathi hiyo;
- Kumteua msimamizi wa Mirathi ya marehemu.
- Kutambua majina ya warithi wa marehemu,
- Majina ya warithi wa marehemu,
- kutambua hali ya ndoa ya marehemu;
- uwepo wa wosia wa mwisho wa marehemu au la,
- Kama kuna wosia, uoneshe yaliyomo ndani ya wosia
- Orodha ya madeni yaliyotambuliwa ya marehemu anayodaiwa ama anayodai,
- uteuzi wa msimamizi wa mirathi ya marehemu
C: NI KINA NANI WANAORUHUSIWA KUOMBA USAJILI WA KIFO CHA MAREHEMU?
- Ndugu wa karibu wa marehemu waliokuwepo wakati na mahali ambapo kifo cha marehemu kilitokea au waliowahi kumtembelea akiwa katika ugonjwa siku za mwisho za uhai wake;
- Ikiwa ndugu wa karibu hawapo, basi ndugu yoyote wa marehemu anayeishi ndani ya Wilaya kifo kilipotokea;
- Kama ndugu hawapo, mtu yeyote aliyekuwepo mahali na wakati kifo kilipotokea, AU
- Mmiliki wa nyumba ambapo kifo kilitokea;
- Ikiwa mwenye nyumba hayupo, basi Mkazi yeyote wa nyumba ambayo kifo kilitokea;
- Mtu aliyehusika na utunzaji wa mwili wa marehemu au aliyeagiza mazishi ya mwili huo (mfano, polisi au mahakama au viongozi wa mamlaka za serikali nk)