Kuna msemo usemao kuwa "while a person is busy finding the keys to success, others are busy changing the lock". Msemo huu sijui nina mkosi nao maana kila ninachojaribu kufanya kunakuwepo na kiwingu. Nilipokuwa mdogo niliazimu moyoni ya kuwa elimu ndio itakuwa ufunguo wa kuendelea kwangu lakini wapi, nikaambulia patupu kutokana na shule za kayumba. Nikasema haina tabu na kuamua kuwa mchimbaji mdogomdogo napenyewe nikaambulia patupu maana serikali ya magamba iliamua kumuuzia mwekezaji eneo nililokua nachimba. Nikasema haina neno na kugeukia uvuvi lakini kutokana na ziwa kubinafisishwa kwa wawekezaji ilikuwa ni kukamatwa mara kwa mara eti eneo hilo hairuhusiwi kuvua, mwisho nikachoka na kuamua kuuza icecream ambayo ilikuwa inanilipa, magamba wakaona haiwezekani nitoke katika umasikini wakaamua kuningeleja. Kwa serikali ya magamba sijui nitatoka vp ktk umasikini manake kika ninachokifanya magamba wananibadilishia kufuri pale ninapokaribia kupata ufunguo.