Kwa nini mim?

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,502
Kuna msemo usemao kuwa "while a person is busy finding the keys to success, others are busy changing the lock". Msemo huu sijui nina mkosi nao maana kila ninachojaribu kufanya kunakuwepo na kiwingu. Nilipokuwa mdogo niliazimu moyoni ya kuwa elimu ndio itakuwa ufunguo wa kuendelea kwangu lakini wapi, nikaambulia patupu kutokana na shule za kayumba. Nikasema haina tabu na kuamua kuwa mchimbaji mdogomdogo napenyewe nikaambulia patupu maana serikali ya magamba iliamua kumuuzia mwekezaji eneo nililokua nachimba. Nikasema haina neno na kugeukia uvuvi lakini kutokana na ziwa kubinafisishwa kwa wawekezaji ilikuwa ni kukamatwa mara kwa mara eti eneo hilo hairuhusiwi kuvua, mwisho nikachoka na kuamua kuuza icecream ambayo ilikuwa inanilipa, magamba wakaona haiwezekani nitoke katika umasikini wakaamua kuningeleja. Kwa serikali ya magamba sijui nitatoka vp ktk umasikini manake kika ninachokifanya magamba wananibadilishia kufuri pale ninapokaribia kupata ufunguo.

Maisha safari ndefu usife moyo,ongeza bidii kwa kila unalofanya utafanikiwa,maisha ni msukosuko lakini usitetereke.

Every dog has its day, never say die and you will eventually be there!

They say' failure is not failure until you quit'......pambana mkuu

asanteni sana kwa ushauri wenu ila magamba wanatia hasira sana.

Jitahidi tuu ndugu hakuna sehemu hao ccm wapo, hata magamba wenzao wanawadanganyaga kwa kofia na ubwabwa then nothing

na wengine waliofanikiwa je????/
ukiweka mentality yako hivyo hutafanikiwa

hiyo ice cream wamekufanya nini?
una vibali?tabu iko wapi?

Mkuu, usichoke kupambana kuna watu taingia enzi za Mwalimu Nyerere mpaka enzi za JK, wanapambana na bado hawajapata mafanikio lakini bado wanapambana
usikate tamaa mkuu endelea kupambana

na wengine waliofanikiwa je????/

ukiweka mentality yako hivyo hutafanikiwa

hiyo ice cream wamekufanya nini?

una vibali?tabu iko wapi?

kibali ninacho, tatizo umeme ndio wanaouchukua kila siku ilihali biashara yangu inategemea umeme kwa sana

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom