Kwa nini mashabiki wa Yanga huamini Simba ni mbovu kuliko Timu yao?

Tangu nabi aingize mifumo yake yanga haijawahi zidiwa kimpira na timu yoyote Tanzania na CAF
Screenshot_20230417-144504_WhatsApp.jpg
 
Simba ni mbovu kwa yanga,timu imeshinda lakini kipindi Cha pili ni kubutua na kupoteza muda...bado haijawa timu alichofanya robertinho ni kutengeneza mbinu mbili tatu za kupata magoli,ndiyo maana alipojulikana kajaje kwenye game kipindi Cha pili akapotea
Sasa akikuwin kwa mbinu huwezi kukindi kwqmba ni Bora kwako?
 
Kila wakati Takwimu huwa zinasema tofauti na wana- Yanga wanavyoaminishwa na watu wao wanaowaamini. Juzi Kati hapa almanusra Manara awadanganye Yanga kwamba haijawahi kutokea Timu ya Tanzania kuongoza kundi kwenye mashindano ya CAF ikiwa na Pointi 13.

Alipokumbushwa kwamba simba iliwahi kuongoza kundi Ligi ya Mabingwa ikiwa na Pointi hizo 13, akakaa kimya. Lakini Takwimu zile zilishaanza kushadadiwa na watu wa Yanga kwa kasi ya ajabu sana.

Simba inaongoza kwa kuwa na magoli Mengi kwenye Ligi Kuu Tanzania, lakini mashabiki wa Yanga wameaminishwa kwamba Simba eti ndiyo yenye Fowadi mbovu sana kuliko wao. Inakuwaje Simba inayoipita Yanga magoli ya kufunga kwa tofauti zaidi ya magoli 10 eti yenyewe ndiyo iwe na fowadi mbovu?

Pia kuna hoja hii ya kwamba Simba haijawahi kuifunga Yanga tangu mwaka 2019, hii hoja ni ya kweli lakini imetiwa chumvi mno. Namshukuru sana JanguKamaJangu ambaye ameweka takwimu hizi hapa chini.

29/04/2018: Simba 1-0 Yanga

30/09/2018: Simba 0-0 Yanga

16/02/2019: Yanga 0-1 Simba

04/01/2020: Simba 2-2 Yanga

08/03/2020: Yanga 1-0 Simba

07/11/2020: Yanga 1-1 Simba

03/07/2021: Simba 0-1 Yanga

11/12/2021: Simba 0-0 Yanga

30/04/2022: Yanga 0-0 Simba

23/10/2022: Yanga 1-1 Simba

Kwa takwimu hizi inakuwaje watu wa Yanga wadhanie kwamba kuanzia mwaka 2019 Simba imekuwa dhaifu kwao??
Fanyeni usajiri acheni janjajanja. Ni wakati wa nyinyi kujifunza mengi kutoka kwa YANGA.
 
Back
Top Bottom