Kwa nini Chidumule kawachana waimbaji wa bongo flavor pamoja na wale wa dini?

Wakati nikisikiliza taarifa ya habari ITV Chidumule akiwa msibani kwa Dr. Remi Ongala alipewa nafasi ya kuongea chochote. Alisema kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki mahili lakini alikuwa hatembei mabega juu ila anashangaa wanamuziki wa bongo flavor ambao kwanza wamepanga kwenye mabanda ya uani harafu wanatembea mabega juu na wale wa dini kasema wakitoa kasingle kamoja basi wanamsahau hata askofu.

My take: Wanamuziki wa zamani hawawapendi vijana wa bongo flavor maana nilishamsikia ngurumo pia akiwachana kuwa wanaimbia juu, hivyo hawana maana.

ebu nisikie views zenu nanyi pia wana jf.

kiswahili kwa wachaga ni tatizo sana njii hii!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mwanamuziki hasa lazima awe na uwezo wa kupiga angalau ala moja ya mziki kama drum, guitar au keyboard.
Hao bongo falvor na gospel flavor wanaweza?
 
mwanamuziki hasa lazima awe na uwezo wa kupiga angalau ala moja ya mziki kama drum, guitar au keyboard.
Hao bongo falvor na gospel flavor wanaweza?

Ni asilimia tano katika ya wanamuziki wote wanaojua kutumia vyombo vya muziki
 
Ni kweli waimbaji wengi wa kizazi si wanamuziki kama wengi wanavyosema siku zote. Lakini hata hivyo katika biashara ya muziki hicho si kitu cha ajabu. Najua wengi wenu mnaosoma maoni haya ni wasomi na mnafahamu namna muziki kwa wenzetu unavyohusisha watu wengi mpaka wimbo ukausikia hewani.

Kuna wanamuziki wengi wa nje ambao ni waimbaji tu(kutoa sauti basi) ambao hawahusiki katika kutunga, kuandaa melody, kupiga chombo chochote cha muziki na zoezi zima la utayarishaji. Kila kitu kinafanywa na mtu mwingine. Lakni niambie jinsi albam zao zinavyouza! Mwimbaji asipoweza kucheza chombo chochote cha muziki haimanishi kuwa hawezi kabisa kupewa heshima yake. Sababu kubwa inayowafanya wanamuziki wa zamani wawadharau wale wa bongo flava ni wivu tu. Walikuwa na nyimbo nzuri sana katu sikatai lakini hazikuwapa chochote.

Leo hii vijana wanaodharauliwa kuwa si wanamuziki bali wababaishaji tu ndo ambao wamefanikiwa hata kuiweka kdg Tanzania kwenye ramani ya muziki duniani. Ni bendi gani ama mwanamuziki gani wa zamani ambaye amewashawahi kutajwa kuwania tuzo yoyote kubwa duniani? Kwa wengine yaweza kuwa ni sababu ndogo lakini hivyo ndo vigezo vya kutambua kama wanamuziki wetu wanatambuliwa nje ya mipaka. Wanamuziki wa zamani waache wivu kwani kulalama hadharani juu ya vijana wa sasa hv hakutasaidia chochote kama ujumbe wao wanautoa kwa dharau.

Pengine hawafurahishwi na maisha wanayoishi vijana wa sasa yaani jinsi wanavyovaa, wanavyoongea, maudhui katika nyimbo zao lakni watambue kuwa hao ni vijana sio wazee. Namheshimu sana mwanamuziki anayeipa heshima kazi ama style ya mwenzie hata kama haipendi.

Michael Jackson kabla ya kufa alikuwa ameshafanya kazi na wasanii wa sasa kama Akon, 50 Cent. Wil.iam kuonesha heshima katika mabadiliko ya muziki na pia kuwavutia mashabiki ambao muziki wa zamani hawaujui. Hayo ni maoni tu.

Umeongea vitu vya msingi sana ndugu.
Kwa Tanzania, mtu akitungiwa wimbo na wenzie na yeye akauimba tu, wenzi wanamchukulia kama hawezi lolote, matokeo yake ndipo linakuja suala la kuibiana mashairi kati ya wasanii na kutafsiri nyimbo za nje kuwa katika Kiswahili. Shida ni kwamba tunaua muziki kwa namna hii. Inabidi wanamuziki wa Tanzania wakubali vipaji vya wengine, kwamba:-
---Kuna watu wanajua kuandika mashairi lakini hawezi kuimba
---Kuna watu wanajua kuimba ila hawajui kutumia ala ya muziki hata moja hata moja
---Kuna watu wanajua kuimba ila hawawezi kuandika mashairi kabisa
---Kuna watu wanajua kutumia ala, kutengeneza muziki toka katika ala, lakini hawawezi kuimba kamwe
---Kuna watu wanatunga, wanaimba na kupiga ala mbalimbali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom