Mu-Israeli
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 2,454
- 975
Hi wana JF wote.
Najiuliza sana kwa nini bei ya cement iko juu sana hapa Tanzania.
Najiuliza hivyo kwa sababu naona kuna cement toka nje ya nchi inakuja na kuuzwa kwa bei nafuu kuliko cement inayozalishwa hapa Tanzania.
Hiyo cement inayotoka nje imezalishwa kama cement yetu hapa, imesafirishwa, imelipiwa kodi, imelipiwa bima ya usafirishaji, n.k. halafu bado ni nafuu kuliko cement yetu !!!???
Nimeangalia bei za cement za nchini Pakistan ambako ndio inatoka cement nyingi inayoletwa hapa Tanzania.
Bei ya tani moja ya cement ni dola za kimarekani (USD) 62.00 kwa tani (ukinunua huko). Pia bei pamoja na usafirishaji mpaka bandari ya Dar es Salaam au Mombasa ni USD 90.21 kwa tani.
Bei hizo ukizibadilisha kuwa shilingi ni kama ifuatavyo:-
USD 62.00 = Tzs 99,200 kwa tani, ambayo ni Tzs. 4,960 kwa mfuko wa kilo 50.(Ukinunua kule Pakistan bila kusafirisha)
USD 90.21 = Tzs 144,336 kwa tani, ambayo ni Tzs. 7,218 kwa mfuko wa kilo 50 (bei pamoja na usafiri toka Pakistan mpaka Dar es Salaam).
Swali:-
Kinachofanya bei za cement zinazozalishwa Tanzania kuwa juu sana (Tzs. 12,000 au zaidi kwa mfuko wa kilo 50) ni nini ??
Visit: http://www.alibaba.com/product-free/107472674/Cement_52_5_in_20_ft.html