Kwa nini baadhi ya watu wana akili(iq) kubwa kuliko wenzao?

IQ ya mtu huchangiwa na mazingira na vinasaba vya mhusika.Hivyo ndugu yangu kama bado hujao basi jitahidi uweze kuja ku influence IQ ya watoto wako. Kama wewe unatafuta tu sura bila kitu kichwani ujue unatafuta kuleta kizazi chenye IQ ya chini ( probability ni kubwa).

Katika mazingira, mwanamke anayepata ujauzito halafu akawa mlevi au hapati lishe nzuri hiyo nayo huchangia kumfanya mwanae awe na IQ ya chini.Mtoto akisha zaliwa, je wazazi wanachangia vipi kuendeleza akili ya mtoto? Soma kitabu cha Joan Freeman - How to Raise a Bright Child - Utajionea mwenye ni vipi malezi na makuzi huchangia.Mzazi unatakiwa umwangalie mwanao ujue kama ni mtoto gifted ili uweze kumwendeleza zaidi badala ya kumshushia vipaji vyake.Mzazi mwelewa una uwezo mkubwa sana kuchangia kupandisha IQ ya watoto wako.
Haya ni kwa uchache tu.

Asante sana .. kwa jibu hili na pili kwa kutoa na reference,
 
Karibu Mpwa Sinkala habari za kupotea sisi tunaendelea kujenga nchi lakini tunarudishwa nyumba hatua 3 na tunajitahidi kupiga hatua moja mbele.
sinkala-albums-sinkala-picture747-avatar10550-7.gif
Aaah mjomba, mimi naona haupigi hatua zaidi ya kunyatia, sijui unamnyatia nani/nini !! Nilikuwa pembezoni kidogo pale Nakonde, sasa nimerudi.
 
IQ ya mtu huchangiwa na mazingira na vinasaba vya mhusika.Hivyo ndugu yangu kama bado hujao basi jitahidi uweze kuja ku influence IQ ya watoto wako. Kama wewe unatafuta tu sura bila kitu kichwani ujue unatafuta kuleta kizazi chenye IQ ya chini ( probability ni kubwa).

Katika mazingira, mwanamke anayepata ujauzito halafu akawa mlevi au hapati lishe nzuri hiyo nayo huchangia kumfanya mwanae awe na IQ ya chini.Mtoto akisha zaliwa, je wazazi wanachangia vipi kuendeleza akili ya mtoto? Soma kitabu cha Joan Freeman - How to Raise a Bright Child - Utajionea mwenye ni vipi malezi na makuzi huchangia.Mzazi unatakiwa umwangalie mwanao ujue kama ni mtoto gifted ili uweze kumwendeleza zaidi badala ya kumshushia vipaji vyake.Mzazi mwelewa una uwezo mkubwa sana kuchangia kupandisha IQ ya watoto wako.
Haya ni kwa uchache tu.

Asante sana .. kwa jibu hili na pili kwa kutoa na reference,

How to Raise A Bright Child

raiseabrightchild.jpg

The title of this book could be read in two different ways. The first is how to bring your child up to somehow make them ‘bright’. Indeed one of the aims of this book is to maximise your child’s intelligence and ensure that they realise all their potential. The second is what to do if you find you have a bright child and want to know how to deal with it!
Both of these aims are addressed in this book, both how to ensure that a bright child’s talents are recognised, and how to handle a very bright or gifted child to ensure that they also can develop their talents to the full.
The book begins pre-birth with the factors that are common to bright children, from their family situation and birth position, to how to look after your baby to encourage their love of learning from a young age. The book moves on through toddlerhood with practical suggestions for things to do with your child, as well as how to expand a discussion to help your child to develop thinking skills.
The book discusses the characteristics of bright children so that you can determine if your child is bright or gifted, and her suggestion that you keep records of your child’s development would also be a good idea to stop most parents worrying too!
A bright child’s experience of school will probably be the biggest factor in developing their lively minds. The book discusses preparing your child for school, the benefits of a good nursery education and how parents can continue to encourage their child’s curiosity and thirst for knowledge in tandem with their schoolwork.
Finally it discusses how to work alongside your school to ensure a bright child is not bored or discouraged by teaching methods that do not suit the enquiring mind. There are suggestions for how to create extra opportunities for your child if the school does not participate in any gifted children programmes. The book concludes with some fascinating observations on school from a number of bright children who took part in a study by the author. Many show both a surprising and saddening experience of being a bright child, and demonstrates how Dr Freeman’s assertion that a flexible teaching situation is often the most effective for a bright child.
‘How to Raise a Bright Child’ is written in a friendly and jargon-free way, and is an interesting and thought-provoking read on maximising your child’s potential.
 
Hii inatokana sana na mazingira aliyozaliwa mtu na malezi aliyokulia.watu karibu wote huwa tunazaliwa na akili ila huwa zinaharibiwa wakati wa kukua.wataalamu wanasema umri wa mtu kumjengea uwezo wake ni kati ya miaka 0-5.Huu ndio wakati wa kujenga utu wa mtu.Na IQ Huwa kwa watu walio wengi inajengwa.Una weza pia ukajibadilisha kutoka mbumbumbu na kuwa na akili ukitaka kama ukiamua kubadisha mawazo yako.
soma vitabu vya BEN CARSON vya GIFTED HANDS na THINK BIG utaona jinsi kijana huyu alivyobadilika kutoka ukilaza mpaka kuwa genius kwa ajili ya jitihada za mama yake japo alianza na mwanzo mbaya.
 
Thanks

Jibu tafadhali.

Kwanza ni lazima tutofautishe kati ya 'akili' na 'ujuzi'. Ujuzi unapatikana kwa kujifunza kutoka kwa wengine au kutokana na mazingira.

Akili ni uwezo wa utambuzi (cognitive ability) alionao mtu kulinganisha na watu wengine. Ni uwezo wa mtu kutatua matatizo na kuelewa nadharia (concepts) mbalimbali na hii inajumuisha uwezo wa ku-reason, uwezo wa kuona/kutambua uhusiano baina ya vitu, uwezo wa kuhifadhi taarifa('kichwani'!) na kutumia taarifa hizo (retrieving), nk. Wakati ujuzi unaweza kuongezwa, akili ipo relatively stable over time (haiwezi kuongezwa significantly). Kuna wanasanyansi wamewahi kusema, no matter how you are educated, you can not increase your IQ score.

Kuna vitu vingi vinachangia kiasi cha akili mtu alicho nacho. Kwa sehemu kubwa, kama walivyosema wengine akili mtu anazaliwa nayo. Sasa kama anazaliwa nayo, inategemea wazazi (kizazi) wa huyo mtu (genetics), afya ya ubongo kuanzia mtoto akiwa tumboni mpaka anazaliwa na kukua, size ya ubongo na pia gender.
 
Aiseee, kwa hiyo unaweza ukazaliwa mchaga lakini baadaye ukawa Mnyakiusa, asante kwa hili...ninavyofikiri, kabila ni asili ya Mbegu ya aliyeipandikiza na ukazaliwa, lakini haitokani na malezi! Ndiyo maana pamoja na obama kuwa Mmarekani kimalezi lakini ni Mjaluo

Hapo sasa mkuu nashindwa nikusaidiaje(kwa maana unatkiwa hata definition ya culture ufundishwe) lakini labda ungejiuliza kabila ni kitu gani? au ni vitu gani vinamfanya mtu awe mjaluo au mmasai? kwa maana nyingine kabila ni mambo ya mila na tamaduni ambazo mtu huzikuta duniani, hakuna mtoto anayekuwa mchaga akiwa tumboni kwa mama yake ila anaweza kupata uchaga akizaliwa. Ya kwamba Obama ni Mjaluo hiyo ni habari mpya kwangu ila ninajua baba yake ni mjaluo.Hivi niambie iwapo akisimama Obama na Hashim Thabiti ni kipi kinachoweza kusema kuhusu kabila zao?
 
Asante sana .. kwa jibu hili na pili kwa kutoa na reference,

How to Raise A Bright Child

raiseabrightchild.jpg

The title of this book could be read in two different ways. The first is how to bring your child up to somehow make them ‘bright’. Indeed one of the aims of this book is to maximise your child’s intelligence and ensure that they realise all their potential. The second is what to do if you find you have a bright child and want to know how to deal with it!
Both of these aims are addressed in this book, both how to ensure that a bright child’s talents are recognised, and how to handle a very bright or gifted child to ensure that they also can develop their talents to the full.
The book begins pre-birth with the factors that are common to bright children, from their family situation and birth position, to how to look after your baby to encourage their love of learning from a young age. The book moves on through toddlerhood with practical suggestions for things to do with your child, as well as how to expand a discussion to help your child to develop thinking skills.
The book discusses the characteristics of bright children so that you can determine if your child is bright or gifted, and her suggestion that you keep records of your child’s development would also be a good idea to stop most parents worrying too!
A bright child’s experience of school will probably be the biggest factor in developing their lively minds. The book discusses preparing your child for school, the benefits of a good nursery education and how parents can continue to encourage their child’s curiosity and thirst for knowledge in tandem with their schoolwork.
Finally it discusses how to work alongside your school to ensure a bright child is not bored or discouraged by teaching methods that do not suit the enquiring mind. There are suggestions for how to create extra opportunities for your child if the school does not participate in any gifted children programmes. The book concludes with some fascinating observations on school from a number of bright children who took part in a study by the author. Many show both a surprising and saddening experience of being a bright child, and demonstrates how Dr Freeman’s assertion that a flexible teaching situation is often the most effective for a bright child.
‘How to Raise a Bright Child’ is written in a friendly and jargon-free way, and is an interesting and thought-provoking read on maximising your child’s potential.

mkuu naweza pata link ya hiki kitabu tafadhali?
 
mkuu naweza pata link ya hiki kitabu tafadhali?
How to Raise a Bright Child is available at [ame="http://www.amazon.co.uk/gp/product/0091813913?ie=UTF8&tag=eparenting-21&linkCode=as2&camp=1634&creative=6738&creativeASIN=0091813913"]Amazon.co.uk[/ame] and [ame="http://playcom.at/jr16?LID=epbrightchild&DURL=http://www.play.com/Books/Books/4-/960891/-/Product.html"]Play.com[/ame].
 
Hili ni swali linaniumiza kichwa maisha yangu yote kwa nini baadhi ya watu wamejaliwa akili sana wakati wengine ni mambumbu au wana uwezo mdogo wa uweelewa wa mambo? kielimu na hata kimaisha?

Nitafurahi kuelewa ni kwanini kunakuwa na class ya watu katika ufahamu au uelewa wa mambo.

Mifano iko mingi kutoka mashuleni hadi katika maisha yetu ya kawaida.

Inategemea vitu vingi sana: mazingira (physical/psychological), peace of mind and concentration, upatikanaji wa material (mfano baadhi ya familia zinawawezesha watoto wao tangu wakiwa wadogo kupata learning facilities), bidii (juhudi) ya mtu mwenyewe...

Mimi siyo 'geneous' na mara nyingi nasoma kwa ku'struggle' kwa vile sina 'facilities' na uwezeshwaji. Nilipoanza masomo ya philosophy (History of Philosphy - mwaka 1 & Systematic Philosophy miaka 2) tulifanya 'memory test'. Idea ilikuwa kwamba watakao pata around 50% wasiruhusiwe kuendelea na masomo. Unajua tena masomo yetu (kwa context hii ninayozungumzia) yanahitaji mtu mwenye kichwa kizuri la sivyo mtu unachanganyikiwa au unawapotosha watu.

Mfano, katika somo la logic - huyo mwalimu alitaka mtu apate walau kuanzia 55% na siyo chini ya hapo. Basi tulipewa text (A4 page 1) kusoma na kisha mwalimu alitumia 'stop watch' kutwambia tukusanye hizo karatasi. Hatukujua tunafanya nini. Tulipomaliza, aliuliza maswali, ambayo tulijibu kwa muda uliopangwa na kisha kukusanya hiyo kazi.

Halafu tulipewa text nyingine (A4 page 1) na kuambiwa tuisome kwa kuzingatia muda. Ulipopita, alisema tukusanye na akauliza maswali ambayo kila mmoja wetu aliyajibu kwa kuandika. Halafu hizo karatasi za majibu zilikusanywa na baada ya siku kadhaa mwalimu alileta majibu kwa kila mmoja wetu na kutwambia nia ilikuwa kupima 'memory/retention capacity' yetu kwa 'simple text reading' na 'difficult text reading'.

Performance yangu ilikuwa kama ifuatavyo: 'simple text reading' nilipata 80% na 'difficult text reading' nilipata 80% pia. Niliambiwa kuwa kutokana na test hiyo, uwezo wangu wa kukumbuka vitu vyepesi unaelekea kuwa sawa na kukumbuka vitu vigumu (kila mwanafunzi aliambiwa peke yake).

Kwangu, ilitokana na ukweli kwamba nilijizoeza kusoma vitu vigumu muda sawa na vitu vyepesi on grounds kwamba nitakacho elewa nielewe na nitakachoshindwa kuelewa kwa muda huo basi kitasubiri muda mwingine. Baadhi ya colleagues, 'simple text reading', walipata 100% na 'difficult text reading' walipata 55%-70&.

Nilipokuwa Form One, nilijizoeza kutosoma usiku. Nilikuwa nasikiliza kile mwalimu anachofundisha na halafu ikifika muda wa kwenda kulala, nilikuwa nalala. Wanafunzi wenzangu wakiacha kupiga kelele nilikuwa naanza kukumbuka kile tulichojifunza darasani somo moja baada ya jingine. Kwa vile nilikuwa nafanya kila siku, kesho yake asubuhi nilikuwa nakumbuka almost kila kitu tulichojifunza jana yake.

Kwa jinsi hiyo, nilianza kusoma chapter moja mbele ya wenzangu kila siku so much so that nilipofika Form IV & VI, nilitegemea kupata DIVISION I tu na si chini. Sikuwa nafikiria Division nyingine ila nilikuwa sina uhakika na points na kwa kweli nilipata hiyo Division.

Nilipokuwa shule ya msingi, nilikuwa librarian. Na nilijizoeza kuazimisha wanafunzi wenzangu vitabu bila kuwaandika majina yao. Ila nilijua nani ameazima kitabu gani na anatakiwa arudishe tarehe gani tuliyokubaliana. Mtu akisahau nilikuwa namkumbusha.

Hata leo, nikimwazimisha mtu kitabu siandiki mahali au mtu akinikopa hela au nikimkopesha mtu hela siandiki hata kama ni watu 10 (ila kama ni hela inayohitaji maandishi kwa lengo la ushahidi kwa baadaye). Na hii ni kwa sababu tangu zamani nilikuwa najizoeza namna ya kukumbuka vitu na kufanya 'concentration' au 'memory exercises'.

Kuna kijana mmoja tulisoma naye - alipata Division 3 (Science subjects) Form VI na alipojiunga kwenye chuo chetu walikuwa na mashaka naye. Maana walihitaji wenye DivisionI au II Form IV & VI. Ila kwa vile ni masomo ya science basi walimkubali kwa shingo upande. Huyu kijana alipomaliza Philosophy (miaka 3) aliendelea na masomo mengine.

Wakati wa Philosophy, hakuwa 'among the brightest students' kwani alikuwa anapata around 60% na kwetu mwanafunzi aliyekuwa anapata kuanzia 70% ndiye alikuwa anaonekana kama 'amaong the brighest'. Huyo kijana alikuwa rafiki yangu sana na mara nyingi alikuwa anakuja kuomba msaada wa Kiingereza - akiandika paper yake alikuwa ananiletea niisome na kusahihisha lugha.

Basi tuliendelea na yeye aliamua kuchua masomo ya miaka 4 na mimi 3 katika vyuo tofauti. Alipomaliza alipata FIRST CLASS. Aliombwa aendelee kusomea masomo mengine na akakubali. Nilikutana naye Jumamosi iliyopita na alikuwa ananiambia amepata tena FIRST CLASS. Hivyo, sasa hivi siyo mchezo tena. Kilichomsaidia yeye zaidi ni bidii (seriousness katika kutumia muda wake kati ya kusoma na leisure - time management).

Ndiyo maana binafsi, nasema inategemea sababu nyingi sana. Inawezekana nikawa nimejaribu kuelezea unachohitaji au pengine nisema kitu tofauti kabisa! All the same, inategemea vitu vingi sana maana kama nilivyoeleza hapo juu mimi siyo 'generous' lakini nakumbuka secondary wanafunzi wenzangu walikuwa wananiita mwenye 'nature' - maana peformance yangu mara nyingi ilikuwa 80%-90%.

Ila ninavyojijua mimi kama sisomi sipati hizo. Ila sina 'photographic memory'. Nikishaelewa kitu kinabaki kama kilivyo. Nikijifunza leo kesho ukaniletea mtihani utanikomoa. Lakini let's say nimejifunza leo, ukatela wiki ijayo, utanikoma. Sijui memory ya namna gani hii, ila the more time goes after learning something the more I remember it better. Kwa hiyo, nikijifunza kitu darasani na kuulizwa maswali naweza nisijibu kitu, alkini muda ukipita wakati wengine wakiwa wamesahau ndipo ninapokumbuka vizuri.

Nimeona nitumie mfano wangu mwenyewe kwa vile siamini sana kama kuna watu wanaojua kitu kabla ya kujifunza (eti wenye nature). Ila kuna wale ambao wakishajifunza kitu hakitoki kwa urahisi na wengine japo inachukua muda kitu kuingia, kikishaingia basi hakitoki tena.
 
IQ ya mtu huchangiwa na mazingira na vinasaba vya mhusika.Hivyo ndugu yangu kama bado hujao basi jitahidi uweze kuja ku influence IQ ya watoto wako. Kama wewe unatafuta tu sura bila kitu kichwani ujue unatafuta kuleta kizazi chenye IQ ya chini ( probability ni kubwa).

Katika mazingira, mwanamke anayepata ujauzito halafu akawa mlevi au hapati lishe nzuri hiyo nayo huchangia kumfanya mwanae awe na IQ ya chini.Mtoto akisha zaliwa, je wazazi wanachangia vipi kuendeleza akili ya mtoto? Soma kitabu cha Joan Freeman - How to Raise a Bright Child - Utajionea mwenye ni vipi malezi na makuzi huchangia.Mzazi unatakiwa umwangalie mwanao ujue kama ni mtoto gifted ili uweze kumwendeleza zaidi badala ya kumshushia vipaji vyake.Mzazi mwelewa una uwezo mkubwa sana kuchangia kupandisha IQ ya watoto wako.
Haya ni kwa uchache tu.

Veracity! Thanks a lot for the info plus the reference.

Ila kuna watoto wanazaliwa katika mazingira magumu hata kusoma ni shida na bado ni bright sana, na wazazi wao hata darasa 1 hawakufika. Lishe pia ilikuwa duni nk. Au unakuta baba ni prof na mama ni dr. mtoto akitoka hapo hoi kbs darasani hamana kitu na unakuta ni wote katika huo uzao so these are question which have been always disconcerting me.
 
Nguli, jaribu kutofautisha kati ya akili na ujuzi. Kuwa prof ama doc, haina maana kwamba una IQ ya zaidi (ni ujuzi zaidi kuliko akili!). Au kutokusoma hakuna maana kwamba IQ yako ipo chini. Nina imani kuna unafahamu watu wengi tu ambao hawajagusa darasa hata moja lakini mambo wanayofanya ni makubwa kuliko hata hao maprofesa. Hivyo ni dhahiri kwamba mtoto wa Prof anaweza kuwa na IQ ndogo kuliko yule wa mkulima.
 
Veracity! Thanks a lot for the info plus the reference.

Ila kuna watoto wanazaliwa katika mazingira magumu hata kusoma ni shida na bado ni bright sana, na wazazi wao hata darasa 1 hawakufika. Lishe pia ilikuwa duni nk. Au unakuta baba ni prof na mama ni dr. mtoto akitoka hapo hoi kbs darasani hamana kitu na unakuta ni wote katika huo uzao so these are question which have been always disconcerting me.
Nitajaribu kukujibu kwa kifupi kama hivi:
1. Tofautisha kati ya elimrasmi na isiyo rasmi - kuna wazee vijijini hawajafika hata darasa moja..ila wana maarifa na busara kuliko hata professor.Hii ina maanisha kuwa wanazo za kuzaliwa nazo na pia wameweza kuyatafsiri mazingira yao na kuweza kuchota kutoka visima vya maarifa.Huenda wangeingia madarasa tuliyoingia sisi ingekywa balaa!Binafsi huwa napenda kila ipatapo nafasi kuwasikiliza wazee kama hawa na kujichotea moja mbili - huwa nawaona wao ni maprofessor na mimi mwanafunzi tena njuka.
2.Kuna watoto wa maprofessor nao ni vilaza wa kutupwa... ila ukichunguza sana utagundua kuwa hao na makuzi ya watoto wao.Wako bize na consultancies na miradi mingine ya kusaka noti.Kama wanafuatilia basi ujue huyu mtoto anakosa kitu fulani.Nimegundua kuwa huku kwenye nchi zetu kuna matatizo mengi huwa wazazi hawafuatilii na hii hupelekea udumavu wa akili kwa watoto.Kuna Attention Defficiency Disorder - uncontrollable kid,, hasikii wala ku pay attention na ni ngumu kutulia (Attention Deficit Hyperactivity Disoder (ADHD) , AUTISM na mengine..wazazi wala hawana habari kama yana dawa au suluhisho.
Hii ni kwa uchache..
 
Look the secret to Jews' intelligence, we can learn from them <http://shahidpages.wordpress.com/2009/03/31/why-jews-are-intelligent/>

Since I spent about 3 year in Israel for internship in few hospital there, It came to my mind about doing thesis/research of "Why the Jews are Intelligent?" It goes without denial that Jews are ahead in all aspect of life such as engineering, music, science and most obvious in business where nearly 70% of world trade/business are held by the Jews such as cosmetic, fashion, food, arms, hotels and film industries (Hollywood and others).
During the 2nd year, in December 1980, and I was about to go back to California, this idea came to me and I was wandering why God gave this gift/ability to them, is this a coincidence or is it man-made that could be produced like the goods from a factory. My thesis took about 8 years to gather all the information as accurately as possible, like the food intake, culture, religion, initial preparation of pregnancy and etc and I would compare them with other races.

Let's start with initial preparation of pregnancy. In Israel, the first thing I noticed is that the pregnant mother would always sing and play piano and would always try to solve mathematical problems together with the husband, and I was very surprised to see the mother always carry math books and sometimes I would help her to solve some problems, I would asked, "Is this for your child in the womb?" she would answer "Yes to train the child still in the womb so that it would be a genius later on". She would solve the problem without let-up until the child is born.

Another thing I noticed, is about the food, she loved to eat almonds and dates with milk, for lunch she would take bread and fish without the head, salad mixed with almonds and other nuts, they believed fish is good for the development of brain and the fish's head is bad for the brain. And also it is like the culture of the Jews for pregnant mothers to take cod liver oil.

When I was invited for dinner, I always noticed that they always like to eat fish (flesh and fillet) and no meat, according to their belief, meat and fish together will not give any benefit to our body. Salad and nuts is a must, especially almonds.
They would always eat fruits first before the main meal. Their belief if you eat the main meal first (like bread or rice) then fruits, this will make us feel sleepy and difficult to understand any lesson you learn in school.

In Israel, smoking is a taboo, if you are their guest, don't smoke in their house, they would politely ask you to go out for a smoke. According to scientist in university of Israel, nicotine would destroy the main cell in our brain and will affect the genes and DNA, resulting in generation of moron or defective brain. So all those smokers, please take note (Ironically, the biggest producer of cigarettes is&#8230; you know who.. make your own guess).

The food intake for the child is always under the guidance of the parent, first, the fruits with almonds, followed by cod liver oil. In my assessment, the Jewish child, most of them knew 3 languages, ie Hebrew, Arabic and English, since childhood they would be train in playing piano and violin, it is a must. Accordingly, it is believed that this practice will increase the IQ of the child and will make him a genius. And according to Jewish scientist, the vibration of music would stimulate the brain and that is why there are lots of geniuses among the Jews&#8230;
Since grade 1 to 6, they would be taught business mathematic and science subjects would be their first preference. For comparison I could see the children in California, their IQ is about 6 years back. And Jewish children were also involved in athletics such as archery, shooting and running, accordingly it is believed that archery and shooting would make the brain more focus on decision and precision.

In high school, students are more inclined to study science, they would create products, indulged in all sorts of projects , although some looks very funny or useless, but all attention is given seriously especially if it is armaments, medicine or engineering, the idea will be introduced in higher institute in polytechnics or universities.

Business faculty will be given more preference, in the last year of university, the students in business would be given a project and practically they can only pass if their group (about 10 in a group) can make profit of USD1 million. Don't be surprised, this is the reality and that is why half of the business in the world is held by the Jews, who design the latest Levis, it is being designed in the Israel university by the faculty of business and fashion.

Have you seen them how they prayed, they always shake their heads; accordingly they believed this action will stimulate and provide more oxygen to the brain, same thing with Islam where you need to bow down your head. Look at the Japanese, they always bow down their heads as their culture, lots of them are smart, they love sushi (fresh fish), is this a coincidence?

In New York, the commercial/trading center for the Jews are based in New York, catering for the Jews only, if they had any beneficial idea, their committee will give free interest loan and will make sure the business prosper. Due to this, starbuck, dell computer, cocacola, DKNY, oracle, levis, dunkin donut , Hollywood films and hundreds other businesses were under their sponsorship. Jewish graduates from faculty of medicine in new york were encouraged to register with them and allowed to practice privately with this free interest loan, now I knew why most hospital in new york and California always lack of specialist doctors.

Smoking will lead to generations of moron. During my visit to Singapore in 2005, made me surprised to see smokers are regarded as an outcast and the price of a pack of cigarettes is about USD 7, like in Israel it is a taboo and their form of government is similar to the Israelis. And that is the reason why most of their universities are of high standard, even though Singapore is only as big as Manhattan.

Look at Indonesia, everywhere people are smoking, and price of a pack of cigarette is very cheap only USD0.70 cts. and the results with millions of people, you can count the number of universities, what product they produced that can be proud of, technology.. never&#8230; can they speak other than their own language, why it is so difficult for them to master English language for example, all this is due to smoking, think for yourself.

In my thesis, I do not touch in respect of religion or race, why the Jews are so arrogant that they were being chased around since the time of Pharaoh until Hitler, for me it is about politic and survival, the bottom line is, could we produce intelligent generations just like the Jews. The answer could be in the affirmative that needs change in our daily habits of eating, parenting and I guess within 3 generations, it could be achieved. This I could observe in my grandson, for example at the age of 9 he could write a 5-page essay on "Why I love tomato"

May all of us be in peace and succeeded in producing a future generations of genius for the betterment of humankind no matter who you are.
 
Jiulize kwanza akili ni nini?, unatumia vigezo/measurement gani kupima akili?,
 
Ndugu yangu nimesoma maelezo ya wachangiaji waliopita kweli mengi, kama sio yote, ni mazuri. Nami pia nimeongeza ufahamu kwa kile kidogo nilichokuwa nakijua. Ila napenda kutoa nyongeza kwa yale yaliyoainishwa.

Kwa mtazamo wangu naliangalia hili jambo katika sura mbili, moja ni ya kisayansi na pili ni ya kiimani. Mimi nitagusia suala la kiimani kwani kisayansi mengi yamekwisha ongelewa.

Binadamu tunaamini kuwa kuna nguvu iliyotuumba. Katika kuumbwa huko binadamu tunatofautiana sana. Na utofauti huo ni mpango mzuri wa nguvu iliyotuweka hapa duniani. Kila mtu ana uelekeo wake aliopangiwa katika maisha. Hii haiondoi fikra na mipangilio ya kimaisha binadamu anayofanya. Fikra na mipangilio hiyo ipo kwa ajili ya kuboresha na kuhakikisha ule mpango mzuri aliopangiwa na muumba wake unakamilika.

Wengi tumepita shule na tunaishi na jamii zetu. Utakuta watu wawili wanakwenda shule, mmoja anakuwa mzuri sana darasani, anafaulu sana mitihani lakini mwingine kila siku anashika mkia. Hapo ndipo watu wanakosea kujaji suala la akili za watu. Wengi watasema yule anayefaulu sana basi ana akili sana na yule ambaye anashika mkia hana akili. Kama ukiwachukua watu hawa wawili ukawapeleka kwenye ufundi wa magari utakuta yule aliyekuwa anashika mkia anafanya vizuri sana kushinda yule anayefaulu darasani. Hapo hapo yule anayefaulu sana ukampeleka kwenye udaktari ukakuta anafanya vizuri sana.

Kwa mfano huo hapo juu, binafsi ninaamini kuwa kila binadamu kaumbwa kwa aina yake. Kila mtu kuna sehemu ni mzuri sana na anafanya vizuri tofauti na sehemu zingine, hii ni kutokana na jinsi tulivyoumbwa. Kila mtu ana kipaji chake kinachotambulisha uwezo wa akili yake, kuna madaktari, viongozi, wanamichezo, walimu, mafundi wa aina mbalimbali n.k. Ni mara chache sana utakuta mtu ana ujuzi zaidi ya mmoja lakini kuna ujuzi ambao amebobea zaidi.

Tatizo watu wanaonekana sio wazuri kwenye sehemu mbalimbali ni kutokana tu mtu anaingia kwenye ujuzi ambao yeye binafsi hana kipaji nao. Na wengi wetu tumo kwenye huu mkumbo. Hatufahamu ni wapi tunatakiwa kuwa. Hii inachangiwa sana na malezi pamoja na mazingira tunayokulia kwa ujumla wake.

Mwisho naweza kusema kuwa suala la akili ya mtu linategemea ushauri wa kisayansi kama wachangiaji walivyoainisha na pia utambuzi wa kipaji gani mungu alichokuumba nacho, basi siku zote utaonekana wewe ni mwerevu.

:yo:"Unexamined life is not worth living", by Socrates.:amen:
 
jibuni swali hili hapa: kwanini kuna watoto kutoka family masikini, hawali samaki wala nini they are bright, why?
 
Kuna mabango ya waganga wakienyeji yanaonyesha kuna dawa za kuongeza akili darasani..! Je umeshawahi kukutana na mtu anatumia dawa hizi? IQ iko ki-nature zaidi. Haijalishi umetoka familia gani
 
Back
Top Bottom