Kwa nini baadhi ya watu wana akili(iq) kubwa kuliko wenzao?

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Hili ni swali linaniumiza kichwa maisha yangu yote kwa nini baadhi ya watu wamejaliwa akili sana wakati wengine ni mambumbu au wana uwezo mdogo wa uweelewa wa mambo? kielimu na hata kimaisha?

Nitafurahi kuelewa ni kwanini kunakuwa na class ya watu katika ufahamu au uelewa wa mambo.

Mifano iko mingi kutoka mashuleni hadi katika maisha yetu ya kawaida.
 
Mie naona inategemea tu na koo ya mtu au generation ya mtu. Maana kuna generation nyingine ni vilaza tu hawa wakienda shule.
 
ni sawa na kuuliza kwanini huyu ni zeru zeru?
au kwanini yule ni kichaa?
au kwa nini yule ni mweusi!

THE ANSWER:mwanasayansi atakwambia kuna GENETICAL POINT OF VIEW!

mwanajamii atakujibu ni HUMAN NATURE

mwanadini atakwambiaMIPANGO YA MUNGU
 
Kwa nini watu wengine wanene wakati wengine wembamba?

Kuna sababu za genetics, kuna sababu za mazingira.
 
Kwa nini Huyu mkuriya na yule mmasai?
Kwa nini huyu mpare na yule mchaga
Kwa nini huyu ni Mnyakyusa na yule Mfipa?...............
 
Mbona karibia wote maniuliza tena mimi maswali? nijibuni tafadhali.
 
Kwa nini Huyu mkuriya na yule mmasai?
Kwa nini huyu mpare na yule mchaga
Kwa nini huyu ni Mnyakyusa na yule Mfipa?...............

Hii ya kabila ni tofauti kabisa na swali mkuu, kabila ni jambo mtu anakutana nalo baada ya kuwa amezaliwa, kwa maana nyingine kabila mtu hazaliwi nayo(hujasikia hadithi ya yule mtoto wa kimasai aliyezaliwa na wazazi wote wafaransa ila wazazi wake walipotea mbugani huko kilicho wakuta hakijulikani ila mtoto akalelewa na jamii ya wamasai?) lakini hili la akili ni lakuzaliwa nalo na kinachofanywa na mazingira ni kuiendeleza na kushape kutokana na mazingira yenyewe.
 
Kwa nini huyu anapenda kujiexpress na huyu hapendi kujiexpress utajibiwa ni HUMAN NATURE
 
Hii ya kabila ni tofauti kabisa na swali mkuu, kabila ni jambo mtu anakutana nalo baada ya kuwa amezaliwa, kwa maana nyingine kabila mtu hazaliwi nayo(hujasikia hadithi ya yule mtoto wa kimasai aliyezaliwa na wazazi wote wafaransa ila wazazi wake walipotea mbugani huko kilicho wakuta hakijulikani ila mtoto akalelewa na jamii ya wamasai?) lakini hili la akili ni lakuzaliwa nalo na kinachofanywa na mazingira ni kuiendeleza na kushape kutokana na mazingira yenyewe.
Aiseee, kwa hiyo unaweza ukazaliwa mchaga lakini baadaye ukawa Mnyakiusa, asante kwa hili...ninavyofikiri, kabila ni asili ya Mbegu ya aliyeipandikiza na ukazaliwa, lakini haitokani na malezi! Ndiyo maana pamoja na obama kuwa Mmarekani kimalezi lakini ni Mjaluo
 
Kuna siku Dr Isack Ndodi alisema watoto wadogo wakilishwa ngano wanakuwa na akili sana. Ipo siku nitafunga safari nimtembelee ofisini kwake anipe maelezo zaidi.
 
Hili ni swali linaniumiza kichwa maisha yangu yote kwa nini baadhi ya watu wamejaliwa akili sana wakati wengine ni mambumbu au wana uwezo mdogo wa uweelewa wa mambo? kielimu na hata kimaisha?

Nitafurahi kuelewa ni kwanini kunakuwa na class ya watu katika ufahamu au uelewa wa mambo.

Mifano iko mingi kutoka mashuleni hadi katika maisha yetu ya kawaida.

Naona kama unachanganya mambo vile! Unataka kujua ni:

1. kwa nini baadhi ya watu wana akili sana kuliko wengine? au
2. kwa nini baadhi ya watu wamejaaliwa akili kuliko wengine?

Naweza kukusaidia kama issue yako ni swali la kwanza. Hilo la pili, nadhani ni mungu (kama ni wewe muumini) ndie anayeweza kusema kwa nini wengine kawapa zaidi.
 
Kuna siku Dr Isack Ndodi alisema watoto wadogo wakilishwa ngano wanakuwa na akili sana. Kuna siku nitafunga safari nimtembelee ofisini kwake anipe maelezo zaidi.

Karibu Mpwa Sinkala habari za kupotea sisi tunaendelea kujenga nchi lakini tunarudishwa nyumba hatua 3 na tunajitahidi kupiga hatua moja mbele. Huyu Ndodi yupo Magomeni Mwembe chai kama sikosei.
 
Kuna siku Dr Isack Ndodi alisema watoto wadogo wakilishwa ngano wanakuwa na akili sana. Kuna siku nitafunga safari nimtembelee ofisini kwake anipe maelezo zaidi.

wengine wanasema mtoto asipomnyonya mama anakuwa na akilu finyu....siujui tuamini lipi hapa.
 
Naona kama unachanganya mambo vile! Unataka kujua ni:

1. kwa nini baadhi ya watu wana akili sana kuliko wengine? au

Naweza kukusaidia kama issue yako ni swali la kwanza. Hilo la pili, nadhani ni mungu (kama ni wewe muumini) ndie anayeweza kusema kwa nini wengine kawapa zaidi.

Thanks

Jibu tafadhali.
 
IQ ya mtu huchangiwa na mazingira na vinasaba vya mhusika.Hivyo ndugu yangu kama bado hujao basi jitahidi uweze kuja ku influence IQ ya watoto wako. Kama wewe unatafuta tu sura bila kitu kichwani ujue unatafuta kuleta kizazi chenye IQ ya chini ( probability ni kubwa).

Katika mazingira, mwanamke anayepata ujauzito halafu akawa mlevi au hapati lishe nzuri hiyo nayo huchangia kumfanya mwanae awe na IQ ya chini.Mtoto akisha zaliwa, je wazazi wanachangia vipi kuendeleza akili ya mtoto? Soma kitabu cha Joan Freeman - How to Raise a Bright Child - Utajionea mwenye ni vipi malezi na makuzi huchangia.Mzazi unatakiwa umwangalie mwanao ujue kama ni mtoto gifted ili uweze kumwendeleza zaidi badala ya kumshushia vipaji vyake.Mzazi mwelewa una uwezo mkubwa sana kuchangia kupandisha IQ ya watoto wako.
Haya ni kwa uchache tu.
 
Back
Top Bottom