Kwa nguvu hii ya CHADEMA, Mwalimu Nyerere leo angekuwa HAI, angeendelea kukumbatia KADI ya CCM?

Ukweli husemwa:

Tusibweteke hapa na kuanza kumpamba Mwl Nyerere kama vile aliondoka na kuacha nchi iliyojaa neema na baraka.

Kwa nini watu hatuongei ukweli?. Mimi niwashangaa sana pale watu wanapoanza kuona mabaya tu kuanzia kwenye serikali ya awamu ya pili. Kuanzia kwa Nyerere mpaka kwa Kikwete wote ni walewale (manzi ga nyanza).

Mwl Nyerere, Kwanza siasa aliyokuwa akiiabudu alimshinda na akaamua kufunika uso wake kwa kutaka tuamini kuwa aling'hatuka. Alifanikiwa kwa hili kwa vile kipindi chake hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari kama ilivyo kwa sasa katika kumulika utendaji wa serikali kila sekunde.

Nchi aliiacha imefilisika na juu yake kukiwa na madeni ya ndani na nje lukuki.

Ondoeni hapa siasa za vibwagizo. Msingi wa Siasa za Nyerere, NDIZO ZILIJENGA JAMII HII TULIYONAYO KWA SASA.

Mheshimiwa ulotukuka leta facts acha rhetorics na nadharia, toa ushahidi wa unayosema, si umeona mimi nilivyoainisha sekta za elimu, kilimo, usafiri na hata uongozi, nikilinganisha jinsi zilivyo kuwa wakati wa nyerere na sasa. Kama unazo nondo za kupinga nilivyosema basi zilete kama hakuna si vibaya kukaa kimya.

Suala la kushindwa kwa policy za nyerere halina ubishi kwa sababu dunia nzima kila mtu alijua kuwa siasa ya kijamaa ilishindwa na ubepari baada ya Ronald Reagan kuwa raisi wa USA na nchi zote zenye mlengo wa kijamaa zilikumbwa na mwanguko wa kiuchumi na kisiasa.
Lakini usisahau kuwa Nyerere aliichukua nchi mikononi mwa wakoloni, hapakuwa na institution za kizalendo, technology ilikuwa hafifu, maeneo karibu yote ya JMT hayakuwa na barabara, maji, umeme, shule, dispensary, hospitali, hakukuwa na wataalam / wasomi, Watanzania walikuwa hawaongei lugha moja, wenye tabia na desturi tofauti tofauti, hawakuwa na shughuli zozote za maana za kuwapatia vipato zaidi ya umanamba na utumishi kwa bana kubwa mhindi na mzungu na mwarabu. How did he turn this country around???

Baada ya kuisuka Tanzania Nyerere hakuacha kupigania ukombozi na hadhi ya mtu mweusi, hatujasahau msumbiji, namibia, angola, zimbabwe, RSA, sychelles,Uganda, zanzibar nk nk. Hapa unaweza kumlaumu kwa kutumia raslimali za watanganyika kupigania ukombozi wa waafrika wengine na kutusababishia machungu ya kiuchumi. Lakini tujiuulize je tungejisikiaje kama hadi leo weusi wa zanzibar wangekuwa bado wanalamba viatu vya mwarabu na mhindi ndani ya ardhi ya asili yao waliopewa na mwenyezi Mungu??? au weusi wa RSA/zim na wazungu????? On that note i believe money was well spent. Nyerere was a special man raised at his time to accomplish what God has desired for his African creation!!!

Nyerere aliachia madaraka kinyume na desturi ya viongozi wa kiafrika wa wakati wake, muulize mugabe, US$1 ni sawa na dola ngapi za zimbabwe?? je ameacha madaraka?? Wakati wa nyerere viongozi wa afrika walikuwa ni maraisi wa maisha - Jomo kenyatta, Kamuzi banda, Mobutu, Iddi Amin, na hata wale ambao hawakutangaza waziwazi bado walikuwa wa maisha - Gaddaffi, Mubarak nk. Nyerere yuko kwenye rekodi za kimataifa kama raisi mwaafrika peke yake aliyeacha uongozi kwa hiari baada ya kuitumikia nchi yake kwa muda mrefu kabla ya siasa ya vyama vingi

Je ni kweli Nyerere aliacha uchumi ulioanguka??? siyo kweli, wakati anaondoka madarakani US$1 = Tsh 20, unemployment rate ilikuwa chini, mfanyakazi alikuwa anauwezo wa kuishi kwa mshahara peke yake, huduma kwenye sekta za serkali zilikuwa zinahadhi na viwango vinavyokidhi nk
usisahau kuwa level ya maendeleo wakati huo dunia nzima ilikuwa chini, hata ulaya kuna maeneo bado watu walikuwa kwenye nyumba za nyasi, maeneo yasiyo na maji na umeme. Maisha ya dar es salaam enzi hizo hayakuwa tofauti sana na malaysia au thailand, hadhi ya miji yao ilikuwa sawa tu na miji yetu, huu mfumuko wa maendeleo ya kasi umeanza kwenye kizazi cha internet.
 
Mheshimiwa ulotukuka leta facts acha rhetorics na nadharia, toa ushahidi wa unayosema, si umeona mimi nilivyoainisha sekta za elimu, kilimo, usafiri na hata uongozi, nikilinganisha jinsi zilivyo kuwa wakati wa nyerere na sasa. Kama unazo nondo za kupinga nilivyosema basi zilete kama hakuna si vibaya kukaa kimya. Suala la kushindwa kwa policy za nyerere halina ubishi kwa sababu dunia nzima kila mtu alijua kuwa siasa ya kijamaa ilishindwa na ubepari baada ya Ronald Reagan kuwa raisi wa USA na nchi zote zenye mlengo wa kijamaa zilikumbwa na mwanguko wa kiuchumi na kisiasa. Lakini usisahau kuwa Nyerere aliichukua nchi mikononi mwa wakoloni, hapakuwa na institution za kizalendo, technology ilikuwa hafifu, maeneo karibu yote ya JMT hayakuwa na barabara, maji, umeme, shule, dispensary, hospitali, hakukuwa na wataalam / wasomi, Watanzania walikuwa hawaongei lugha moja, wenye tabia na desturi tofauti tofauti, hawakuwa na shughuli zozote za maana za kuwapatia vipato zaidi ya umanamba na utumishi kwa bana kubwa mhindi na mzungu na mwarabu. How did he turn this country around??? Baada ya kuisuka Tanzania Nyerere hakuacha kupigania ukombozi na hadhi ya mtu mweusi, hatujasahau msumbiji, namibia, angola, zimbabwe, RSA, sychelles,Uganda, zanzibar nk nk. Hapa unaweza kumlaumu kwa kutumia raslimali za watanganyika kupigania ukombozi wa waafrika wengine na kutusababishia machungu ya kiuchumi. Lakini tujiuulize je tungejisikiaje kama hadi leo weusi wa zanzibar wangekuwa bado wanalamba viatu vya mwarabu na mhindi ndani ya ardhi ya asili yao waliopewa na mwenyezi Mungu??? au weusi wa RSA/zim na wazungu????? On that note i believe money was well spent. Nyerere was a special man raised at his time to accomplish what God has desired for his African creation!!! Nyerere aliachia madaraka kinyume na desturi ya viongozi wa kiafrika wa wakati wake, muulize mugabe, US$1 ni sawa na dola ngapi za zimbabwe?? je ameacha madaraka?? Wakati wa nyerere viongozi wa afrika walikuwa ni maraisi wa maisha - Jomo kenyatta, Kamuzi banda, Mobutu, Iddi Amin, na hata wale ambao hawakutangaza waziwazi bado walikuwa wa maisha - Gaddaffi, Mubarak nk. Nyerere yuko kwenye rekodi za kimataifa kama raisi mwaafrika peke yake aliyeacha uongozi kwa hiari baada ya kuitumikia nchi yake kwa muda mrefu kabla ya siasa ya vyama vingi Je ni kweli Nyerere aliacha uchumi ulioanguka??? siyo kweli, wakati anaondoka madarakani US$1 = Tsh 20, unemployment rate ilikuwa chini, mfanyakazi alikuwa anauwezo wa kuishi kwa mshahara peke yake, huduma kwenye sekta za serkali zilikuwa zinahadhi na viwango vinavyokidhi nk usisahau kuwa level ya maendeleo wakati huo dunia nzima ilikuwa chini, hata ulaya kuna maeneo bado watu walikuwa kwenye nyumba za nyasi, maeneo yasiyo na maji na umeme. Maisha ya dar es salaam enzi hizo hayakuwa tofauti sana na malaysia au thailand, hadhi ya miji yao ilikuwa sawa tu na miji yetu, huu mfumuko wa maendeleo ya kasi umeanza kwenye kizazi cha internet.
Asante kwa ufafanuzi ulioeleweka mkuu.
 
Back
Top Bottom