Kwa mwendo huu, wapinzani mtasubiri sana

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Nawasihi sana Vijana mlio na matarajio ya kile mnachokiita UKAWA kwamba mtachukua Nchi kwa siku za karibuni mfute kabisa mawazo hayo kwa
ni itawachukua muda mrefu kufikia ndoto hizo kwa sababu zifuatazo:-

(a) Hakuna Kiongozi wa Upinzani mwenye nia ya dhati wala mipango ya kwenda IKULU. CDM walikuwa wanakaribia kwenda IKULU kama siyo tama yao ya kutoandaa Mgombea anayekijua Chama chao na mwenye uzoefu wa kutosha katika Siasa za Upinzani. Ndio maana walikosa kujiamini na kuitupa LULU yao dakika za majeruhi.

(b) Hakuna mikakati ya Kisiasa itakayowashawishi wananchi wavipe ridhaa Vyama hivyo kwa kuwa badala ya kunadi Sera wanapoteza muda kunadi makosa ya CCM ambayo hata wao wakiingia madarakani watayafanya tu.

(c) Mtandao wa Upinzani kwenye ngazi ya Vijiji, Kitongoji na Mtaa bado ni dhaifu tofauti na CCM ambayo ina balozi wa nyumba kumi. Kura za Lowassa hazikutokana na Wananchi kuipenda UKAWA bali chuki zao baada ya mtu waliyeamini ni Mgombea bora na aliyekuwa amewekeza kwa muda mrefu kukatwa dakika za majeruhi. Sasa CCM kumetulia na kura za namna hiyo hazitapatikana tena 2010. Natabiri hata kura milioni 2 Wapinzani hawatapata 2020.

(d) Kujichanganya kwa Wapinzani kuhusu Sera wanazosimamia. Angalau wakati wa Dr. Slaa wananchi walijua alichokuwa akikisimamia na wananchi walianza kumuamini. Kwa sasa hata Katibu Mkuu sijui anaitwa nani hata Wananchi hawamjui kabisa na sijui anafanya kazi gani. Ushauri mzuri kwa Vijana ni kwamba msipoteze nguvu zenu mahali ambapo hamtavuna chochote.Rejeeni CCM maana ndio Chama kilichoaminiwa, kinachoaminiwa na kitakachoendelea kuaminiwa kwa muda mrefu mbeleni.

UKWELI NI KWAMBA HAKUNA UPINZANI WA KWELI TANZANIA NDIO MAANA HATA BUNGENI BADALA YA KUJIBU AU KUPAMBANA NA HOJA ZA CCM WABUNGE WENU WANAKIMBIA NA KUSUSA MAANA HAWANA CHA KUONGEA. WANAPIGANIA HOJA ZA OVYO KAMA BUNGE KUONESHWA "LIVE" BADALA YA KUIBANA SERIKALI IPELEKE MAJI, BARABARA, UMEME, HUDUMA ZA AFYA, ELIMU N.K .

AMKAENI VIJANA MSIKUBALI KKUDANGANYWA KUANDAMANA NA KUPAMBANA NA DOLA MAANA HAMTOFANIKIWA ZAIDI YA KUPATA MADHARA NA VIONGOZI WENU HAWATAWASAIDIA KAMWE!!
 
Hivi katibu mkuu wa CDM sio Mbatia? Na msaidizi wake Salum Mwalimu? Wanafahamika mbona!!
 
WanaCCM mmepagawa na nini hasa?
Unavyosema wabunge wa UKAWA hawataki kupambana ndani ya bunge ni pororjo zisizo na msingi kwakuwa nilishuhudia bila chenga wabunge 250 wa CCM walishindwa kujibu page 30 za Lema hali iliyopelekea uongozi wa bunge kuingilia kati kuiokoa CCM.
 
Kura zetu 2020 zipo kwenu tunasubiri kwa hamu mumkabidhi kiti magufuli,aanze safisha wasaliti tuwachukue!
 
Hiyo point ya kwanza ni kweli..hata lowassa alisema "Lengo kuu la upinzani ni kushika dola"...kwa lugha nyingine..lengo sio kusaidia watanzania
 
WanaCCM mmepagawa na nini hasa?
Unavyosema wabunge wa UKAWA hawataki kupambana ndani ya bunge ni pororjo zisizo na msingi kwakuwa nilishuhudia bila chenga wabunge 250 wa CCM walishindwa kujibu page 30 za Lema hali iliyopelekea uongozi wa bunge kuingilia kati kuiokoa CCM.
HIZO NI HOJA ZA KITOTO. PAGE ZA LEMA ZINASAIDIA NINI KUONDOA MATATIZO AU KERO ZA WANANCHI? AMKA KIJANA. KUWA SERIOUS!
 
Umenena vyema tena kwa hoja nzito mtoa uzi huu,ni ukweli mtupu kwamba kwa sasa hakuna chama imara cha upinzani,ama hakuna muungano imara,kwani UKAWA kwisha,chama kimoja kimoja kwisha,mfano kilichokuwa kikidhaniwa kuwa chama kikuu cha upinzani CDM imebainika uimara wake unategemea makosa ya upande wa pili lakini hawana mpango kazi wa kila siku,ndiyo maana wakisikia bunge halionyeshwi live,wanahamia huko,wakati hawana matawi huko vijijin,ruzuku zao,zinaishia ufipa,mie naona hawako serious,huwezi chukua nchi kwa chama ambacho hakijasambaa na ambacho hakiko serious,naungana nawe CCM haina mpinzani bado,tuseme ukweli na walipomuingiza Lowassa ilikuwa sawa na kumwagia maji ya moto kwenye nyumba ya nyasi ukitaraji,moto utokee
 
Ni kweli haziwezi kupatikana tena 2010.....kwa kuwa tunaenda mbele na haturudi nyuma
 
Nyie subirini muone kinachofuata. Traffic Polisi wameruhusiwa kupokea 5000 za kubrash viatu, manesi nao watadai ya kununulia gloves, mahakimu wa mahakama nao watatitaka tuwape za kupeleka suti dry cleaner nk nk.
Rushwa ndogo ndogo inarudi kwa ruhusa maalumu iliyotolewa na hapo ndio wananchi wa kawaida mtawajua 2020 au 2019 local gavt
 
Nyie subirini muone kinachofuata. Traffic Polisi wameruhusiwa kupokea 5000 za kubrash viatu, manesi nao watadai ya kununulia gloves, mahakimu wa mahakama nao watatitaka tuwape za kupeleka suti dry cleaner nk nk.
Rushwa ndogo ndogo inarudi kwa ruhusa maalumu iliyotolewa na hapo ndio wananchi wa kawaida mtawajua 2020 au 2019 local gavt
Hizo porojo zenu hazitajenga Upinzani. Nyie subirieni tu mkono wa binadamu udondoke ili muokote!
 
Mtatapatapa sana. Mara upinzani dhaifu, mara upinzani unakufa, mara mnapiga marufuku shughuli za siasa mpaka 2020. Yote mnafanya na kusema nyie tu. Mashujaa na wenye hofu kubwa ni nyie nyie, Sasa sisi mnataka tuwasaidieje??
 
Mtatapatapa sana. Mara upinzani dhaifu, mara upinzani unakufa, mara mnapiga marufuku shughuli za siasa mpaka 2020. Yote mnafanya na kusema nyie tu. Mashujaa na wenye hofu kubwa ni nyie nyie, Sasa sisi mnataka tuwasaidieje??
Huna cha kutusaidia zaidi ya kujitambua na kuachana na Siasa za Kilaghai. Hujachelewa bado. Karibu CCM
 
Back
Top Bottom