Kwa mwendo huu wa Jeshi la Polisi ni kuichimbia Kaburi CCM!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Tujikumbushe 2005, Je wananchi ungewaambia Kikwete asipewe surport Wananchi wangekuelewa??
Wasingekuelewa, kwani walikuwa na imani naye vivyohivyo kwa Lowassa watu wanaimani naye.Mimi niwambie Jeshi la Polisi wawe makini kwani kufanya maagizo ya CCM nikutaka kuvunja amani,Na zaidi nikupandikiza chuki katika wananchi na mwisho wake, ni kuichimbia Kaburi CCM!
CCM watafunte mbinu nyingine ila kwa hili la kutumia vyombo vya dola mnaelekea kupata anguko la aibu!
Mwisho usine wenzetu afrika ya kati wanakimbia kimbia ukadhani wao walizaliwa na vita!Mambo ya lianza hivi!
 
machafuko kwenye nchi nyingi za kiafrika husababishwa na watawala kwa kutumia vyombo vya dola ili kuendelea kubaku madarakani. nimeziona hizo dalili hapa tanzania. tusidhani tanzania ni kisiwa cha amani milele..
 
Samahani mimi ni mgeni, naomba nielekezwe namna kuandika mada mpya!
 
Tatizo huko ndani ya chama chao hakuna mtu wa kumshauri mwenyekiti wao anapokwenda kombo umejaa unafiki mtupu. Sasa hivi tunaona mtoto na mama kama vile washauri wakuu wa mzee. Watu watauliza kivipi, lakini ukitembelea page ya bwana mdogo FB kwa siku nyingi aliyokuwa anayaandika ndio yanayokuja kusemwa na mzee. Mama naye akisema kitu kwenye ile NGO yake ambayo imejiingiza kwenye siasa kinyume na taratibu kinakuja kuwa kweli.
Wakubwa na viongozi ndani ya chama, mshaurini mwenzenu chama kinamfia (ambalo ni jambo la kawaida) lakini kisife na watu, na nyie muje muishi maisha mazuri tuu ya kustaafu! Nani anapenda uzeeni aishie jela au familia imesambaratika?
 
.......mungu isaidie Tanzania pia jk amalize KWA amani,tupate kiongozi chaguo LA wengi ndiye awe rais wetu KWA AMANI!
***DEMOKRASIA IFUATE MKONDO WAKE TUNAJUA IKIFINYWA TU ALIYEIFINYA ATAKUWA ADUI NAMBARI MOJA WA WATANZANIA
 
Si labda anaona raha tu kuandika

Kama ni wa upande wetu ukawa tumfundishe

Fanyeni ivo bhana, hata mimi nataka kujua ni vip maada inaandikwa. Nilitaka kumuweka hewani mwanajamii forum mmoja anaitwa Fukara, kanitapeli elf 50 kwa kujidai anaweza kuniunganishia huduma ya dstv supesport!
 
Ninachotaka kuandika cha kwanzani; WALINZI WA HAKI WANAPOLALA FOFOFO! Nisaidieni jamani ili nami nilisaidie taifa langu.
 
Fanyeni ivo bhana, hata mimi nataka kujua ni vip maada inaandikwa. Nilitaka kumuweka hewani mwanajamii forum mmoja anaitwa Fukara, kanitapeli elf 50 kwa kujidai anaweza kuniunganishia huduma ya dstv supesport!

Ulitegemea nini kwa Fukara?
 
Samahani mimi ni mgeni, naomba nielekezwe namna kuandika mada mpya!
Fungua jukwaa unalotaka kuandika mada yako, kwa mfano Jukwaa la Siasa au Uchaguzi Tanzania, kisha utaona kidude kimeandikwa POST NEW TOPIC, hapo utaclick kuna itatokea page mpya utaandika kichwa cha mada kuu then utaandika contents zako kwa chini.
NB: Epuka mada za kusifia ccm na Magufuli, lete mada nyingi za kusifia UKAWA na LOWASA.
 
Back
Top Bottom