Naomba kuuliza mimi ninamtu namjua amenitukana na kunikashifu kwa kunitumia sms lakini yeye anaishi shinyanga mimi ninaishi tanga je nini naweza kufanya ili hatua za kisheria nizifate??Tafadhali nisaidieni!!
Kutoa lugha ya matusi ni kosa kisheria. Kuna sheria aina Mbili moja iko ile ya kanuni za adhabu na nyingine sheria ya madhara...kwa sheria ya madhara lazima uonyeshe umedhurika na hayo matusi na pia kuna mtu mwngine zaidi ya ww amesoma huo ujumbe...kuhusu madhara haimaanishi uumie ila onyesha umedhurika kibiashara au kijamii inayokuzunguka...hapo utadai fidia na kupata pesa ya kutosha. Ukienda na sheria ya kanuni za adhabu hutapata fidia interms of cash ila uliyemtuhumu atafungwa. Naomba nikupe angalizo kwamba kudhibitisha hili itakuwa bila shaka yeyote ambayo ni ngumu so kama mtoa ushauri nakushauri uende kushtaki kwa sheria ya madhara ambayo ni rahisi kuthibitisha na mwisho wa siku utapata fidia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.