Kwa mpango huu shule binafsi zianze kufugia kuku madarasa

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,086
10,062
Moja ya hotuba zenye kutia hofu ni hii ya kiongozi wetu. Anasema vyuo vingine vitajifuta vyenyewe. Mkuu ujue kujenga shule au chuo sio pesa ya mchezo, ujue vyuo hivyo havifi kwa sababu wenyewe ni matapeli hapana. kule Shinyanga askofu wa kanisa la AIC amefukuzwa kazi baada ya shule ya kanisa kujiendesha kwa hasara na kusababisha kuuzwa na bank ya CRDB.

Kwa sasa hivi wimbi la shule binafsi kufungwa na watoto kufukuzwa shule limepamba moto, wiki iliyopita shule ya msingi Jordan imewafukuza watoto wote kisa mzungu aliyekuwa anatoa pesa amejiondoa na wamiliki hawana fedha za kuendesha shule. Ujue shule sio sawa na roli kuwa likikosa mizigo utaliegesha na kupiga greese kama Mwijage alivyoshauri.

Utaratibu wa kuwapangia wanafunzi wa vyuo ulifanywa kihuni na maamuzi yale yaliyumbisha vyuo vingi vya binafsi, wakati chuo cha UDOM wakipewa wanafunzi elfu saba tena wote wakilipiwa ada na serikali chuo kama SAUT kilipunguziwa wanafunzi kutoka elfu tatu hadi chini ya elfu moja. Tulilipigia kelele humu lakini wapi! Hakuna aliyelisikiliza haya mbona umerudi kulekule.
 
Yeye ni dereva na hizo ni kelele za abiria na alishasema hawezi kusikiliza
sasa wengine sio abiria, wanamagari yao binafsi unapoanza kuwapigia honi wakupishe unakuwa hautendi haki.
 
Hivi UD ilipoanza ilianza kwa kuwa bora kuliko vyuo vikongwe vya barani Africa na Ulaya?
 
Huyu bwana anaua sekta binafsi,anadhibiti mzunguko wa hela halafu anafikiri kujenga hostel na miundombinu pekee ndio nchi itasponga mbele?

Atatuacha watanzia tukiwa hohehahe!


Time will tell
 
Wazo la kuwaruhusu wanafunzi wajichagulie vyuo vya kusoma niona zuri sana.Litaviinua vyuo vikuu vya binafsi hasa vya taasisi za DINI kama SAUT,RUCU,ST.JOHN DODOMA,MUSILIM UUNIVERSITY MOROGORO nk. Vyuo hivi vinaaminika na wazazi kwa kutoa MAADILI BORA kwa wanafunzi. Pia walimu/lecturers huwa jirani zaidi na mwanafunza ktk kumsaidia aelewe madomo.Kumbe vyuo vya serikali ni ELIMU TU hakuna MAADILI.Walimu ni timeless. Nobody cares.Naamini kabisa wazazi wenye uchungu na watoto wao watapenda wasome vyuo vikuu vyenye kuzingatia maadili mema, ambavyo ni vya taasisi za kidini. HII NI HABARI NJEMA KWA VYUO VIKUU VYA KIDINI.
 
Sielewi. Nilidhani tcu huwa inawapangia wanafunzi vyuo kulingana na walivyochagua wenyewe na kulingana na masharti ya chuo husika.
 
Sielewi. Nilidhani tcu huwa inawapangia wanafunzi vyuo kulingana na walivyochagua wenyewe na kulingana na masharti ya chuo husika.
Mim mwenyewe sielewi mkuu, kwa hali hii nawaona wenye div 5 tena wanaingia chuo kikuu, maana sasa mwanafunz ndiye atakuwa na maamuz ya kujichagulia chuo anachopenda moja kwa moja au TCU wata-monitor vp swala hilo kuzuia admission za kihuni vyuoni?
 
Tatizo ni kuwa shule za Serikali zitaweza kutoa elimu bora na kukabili wingi wa wanafunzi
Mkuu kwa hali ilivyo vyuo vya serikali vinalemewa na wanafunzi tayari, vingi vinashida ya kutoa laboratory work nk. Hivyo sidhani kama vinauwezo wakupokea wanafunzi wengi zaidi bila kuboresha miundo mbinu na walimu. La msingi zaidi ni kuiwezesha TCU ifanye kazi yake kwa weledi na maadili na uhuru kamili.
 
Back
Top Bottom