Kakende
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 2,741
- 1,231
Kwa muda sasa Chama Cha mapinduzi kimekuwa kikitumia mgongo wa udini ili kusambalatisha kwa maksudi vyama vinavyopata umaarufu hapa Tanzania. Mfano miaka kadhaa iliyopita CUF ilipata umaarufu lakini ghafla CCM wakazusha eti ni Cha waislam, wajinga nao wakaamini. Inawezekanaje hapa Tanzania chama kikashinda kwa njia ya udini? Au kikasajiliwa wakati ni cha kibaguzi?
Baada ya kuimaliza CUF kwa upande wa bara sasa wamehamia kwa CHADEMA, baada ya kuona kuwa CHADEMA inakuja kwa kasi wamehamua kukizushia eti ni cha dini fulani na ukanda.
Watanzania ebu tuwe watu wa kufikiria kwa umakini, hivi inawezekana CHADEMA ikawa na ajenda za kidini halafu ikawa na watu kama( Freeman mbowe+Zitto Zuberi Kabwe+Abdalah Safari+Wilbroad Slaa+Halima Mdee+Arf, nk.).
Baada ya kuona tayari ndani ya CHADEMA kuna mchanganyiko wa Imani zote, wakaja na hoja ya Ukanda. Hata wakiwa bungeni wanasema eti CHADEMA ni ya kaskazini hivi kweli hata kama haukusoma , inawezekana (Arusha+Mbeya+Mwanza+Kawe+Ubungo+Iringa+Meatu+Maswa =KASKAZINI?), ebu WaTZ tuwe watu makini tusioyumbishwa.
Kwenye uchaguzi wa Igunga ilitokea CHADEMA wakamvua mkuu wa wilaya kitambaa, CCM kwa kuwalagai watu wakazusha eti kavuliwa HIJABU, lakini waislam wa Igunga kwa kuona kuwa huo ni ujinga wakasimama pamoja wakapiga kura kwa CHADEMA (CCM walitaka kuraghai waislam lakini wakafikiria kwa umakini)
Ebu jiulize CCM walikuwa wapi kukiita CHADEMA chama cha ukanda miaka ya 1995, kwanini hili swala limeanza miaka ya 2010? Tena baada ya mbunge mwislam (ZITO KABWE) kupokelewa kama shujaa pale viwanja vya jangwani kwa kuibua hoja ya RICHMOND
Kitendo cha kuwayumbisha watanzania kwa udini na ukanda ni kuwadharau watanzania, kama watatanzania hatutakuwa makini tutataishia kwenye lindi la umaskini kama ilivyo sasa ambapo cha ajabu Reli hazifanyi kazi, Shirika la ndege ATCL limesimama, TANESCO imefikia hatua ya kuzalisha umeme kwa generator, wanafunzi wanakwenda Sekondari bila kujua kusoma Nk.
Watanzania tumieni akili kuchambua mambo, msikubali propaganda vinginevyo mtaendelea kuwapa CCM kura na itawatawala milele