Kwa mara ya kwanza, Jaribio la nchi jirani lakwama Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Jirani anatapa tapa!!

Baada ya kujenga Bandari ya Lamu akitegemea kulikamata soko la Afrika Mashariki huku akitarajia kuiwekea gati zaidi ya 30 ambazo zitaendeshwa na sekta binafsi, huku akiimarisha bandari ya Mombasa na kuweka mipango kujenga SGR kuja Tanzania na SGR nyingine kwenda Congo ili kuzimaliza kabisa bandari za Tanzania sasa amekosa raha baaada ya kusikia Tanzania ameamka na anaboresha bandari zake kwa kiwango cha kimataifa.

Ikumbukwe jirani huyu alikuwa akifadika sana na ukiritimba uliokuwepo katika bandari za Tanzania uliofanya mizigo ichelewe kutoka na meli kuchelewa kushusha bandari jambo lililopelekea wateja wengi kukimbilia katika Bandari yake ya Mombasa!!

Taarifa zaidi zinasema jirani huyu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitumia mwanya wa siasa za Tanzania kupenyeza propaganda kii telejensia ili kufelisha mipango kabambe ya kiuchumi ya Tanzania ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Mji wa kisasa kigamboni, uwekezaji wa treni ya abiria katika jiji la Dar es Salaam ili aendelee kutawala Afrika Mashariki kiuchumi sasa anatapatapa baada ya majasusi wa Tanzania kufanikiwa kukwamisha jitihada zake za kukwamisha makubaliano baina ya Dubai na Tanzania kuhusu Bandari na mkataba husika kupitishwa na Bunge la Tanzania.

Taarifa zaidi zinadai kuwa, Jirani sasa amewekeza sana katika chama fulani cha siasa ambacho kwa muda amekuwa akikifadhili na kuwafadhili wanasiasa na wanachama wake ikiwemo kimatibabu na hata kuwatoroshea kwake pale walipokumbwa na shida nchini Tanzania katika kuhakikisha kinafanya maandamano nchini Tanzania na kuleta pressure kwa wananchi ili serikali ya Tanzania isitekeleze makubaliano na kuingia rasmi mkataba na kampuni ya Dp World ili kuendeleza Bandari zake kwa kuwa anajua endapo Tanzania itafanikiwa kuingia makubaliano na DP World basi ndo itakuwa mwisho wa Bandari zake za Mombasa na Lamu

Hongereni TISS kwa kufanikiwa kuzima hili jaribio la nchi jirani. Sasa mko vizuri katika ujasusi wa kiuchumi.
 
Kuna maswali mmeulizwa mara nyingi ila hamtoi majibu..

1. Kwanini mkataba huo wa kukodisha bandari hauna kikomo cha muda, yaani ni wa milele?

2. Kwanini mkataba huo hauwezi kuvunjwa hata kama wawekezaji watathibitika kukosa uwezo?

3. Kwanini bandari za Zanzibar hazihusiki kwenye huo mkataba, bali ni bandari zoote za Tanganyika pekee?

4. Kwanini wahusika wote wakuu wa mkataba ni Wazanzibar?
 
Vifaa vya kizamani na vingine vibovu, mtandao kuwa chini, wafanyakazi kutoa huduma kama wanatoa msaada wakati ni biashara ndio unasema wakenya walikuwa wanafanya fitna.

Matatizo yetu sisi ni chanzo ni wenyewe hakuna kusingizia Kenya
Hujui usemalo. Acha Mama Tanzania aamke rasmi na kuchukua nafasi yake kama nchi yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom