Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 7,621
- 16,373
Habarini wana jamiifoorums
Leo mida ya saa 7 nilitoka gheto nikaelekea zangu mwenge vinyago kwenda kucheki ishu fulani hivi. Na wakati naondoka gheto nilipita dukani nikanunua maji. Nikafika mwenge maji yakiwa yamebaki kidogo nikafanya ishu yangu niliyokuwa nimefuata nikaanza na nikamalizia pia maji yaliyokuwa yamebaki kwa chupa.
Kimbembe kikaja ni wapi naitupa hiyo chupa, nilijaribu kuangalia sehemu ya kutupa lakini sikuona. Nikasema ngoja nitembee kutoka pale nilipokuwa kuelekea makumbusho kwa kutumia barabara ya bagamoyo huenda nikapata pa kuhifadhi ile chupa. Cha kushangaza nimetembea kutoka mwenge hadi makumbusho stand sijaona sehemu maalum ya kuhifadhi uchafu. Ikabidi niibinyebinye ile chupa niiweke kwenye mfuko wa suruali ili nikaiweke katika chombo cha takataka gheto. Sasa hivi nipo kwenye gari na chupa langi mfukoni kisa tu hakuna sehemu za umma za kuhifadhi uchafu. Na hii si mara ya kwanza, nimeshawahi kurudi na maganda ya machungwa, mifuko ya rambo, na uchafu mwingine kwa kuwa sikuona mahala pa kutupa.
Ushauri wangu: Mamlaka ya majiji na miji iangalie uwezekano wa kuweka trash bins (sijui ndo huitwa hivyo😀😀😀) kila baada ya mita 100 au 150 hasa pembezoni mwa barabara, hii itasaidia kupunguza tatizo la uchafu kutupwatupwa hovyo. Kuweka sheria bila kuweka miundombinu wezeshi ni bure kabisa.
Nakumbusha: niko na chupa la maji mfukoni hapa😀😀😀😀