Usiogope unaweza kujenga na kumiliki kituo cha kujaza mafuta ya vyombo vya moto vijijini cha gharama nafuu

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,331
8,254

Mahitaji ya mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka, ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama "boda boda".


Hata hivyo, maeneo mengi ya vijijini yamebaki kutokuwa na vituo vya mafuta kutokana na ukweli kwamba, wawekezaji wa biashara ya mafuta ya petroli wenye mitaji mikubwa husita kujenga vituo vya kuuzia mafuta Vijijini kwa kuona hakuna biashara ya kutosha.

Matokeo yake, wafanyabiashara wenye mitaji midogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta katika maeneo hayo. Huingia kwenye biashara ya mafuta ya petroli bila uelewa wa kutosha, kutokana na mitaji yao midogo na kutokuwa na uzoefu, wafanyabiashara hawa huanza kufanya biashara ya mafuta kwa kutumia miundo mbinu hafifu na isiyo salama kama vile kununua na kuhifadhi mafuta kwenye mapipa, madumu ya plastiki na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

Uhifadhi wa mafuta kwenye mapipa na madumu ya plastiki ni hatari kwa Usalama, Afya na Mazingira. Ni dhahiri kuna matukio mengi ya moto ambayo yamesababishwa na uhifadhi wa mafuta majumbani au kwenye vibanda vya biashara, ajali hizo za moto, zimegharimu maisha ya watu na kuharibu mali. Pia, wafanyabishara katika maeneo hayo wako hatarini kupata magonjwa ya kansa ya ngozi kutokana na kushika mafuta wakati wa kutoa huduma hiyo, kwa upande mwingine, mafuta hudondoka ardhini na kuharibu mazingira.

Kuhifadhi mafuta kwa kutumia vyombo vya plastiki kunaharibu ubora wa mafuta hasa, mafuta ya petroli. Mafuta na vyombo vya plastiki vina asili moja, ubora wa mafuta ya petroli unaweza kuathiriwa na vyombo vya plastiki na pia mwanga wa jua. Hivyo, vyombo vya moto vinavyo tumia mafuta yanayohifadhiwa kwenye vyombo vya plastiki viko hatarini kupata madhara kwa sababu ya kutumia mafuta ambayo hayana ubora unaohitajika.

Biashara ya mafuta ya petroli ni muhimu sana, lakini ni hatari ikiwa itafanyika kiholela bila kufuata misingi ya usalama na viwango. Hivyo ni vyema mafuta ya petroli yakahifadhiwa na kuuzwa kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo. Lengo ni kulinda usalama, afya, ubora wa mafuta na mazingira.

Moja ya miundombinu ambayo inatimiza lengo tajwa hapo juu ni vituo vya mafuta vya kuuzia mafuta. Sababu kubwa ni kuwa, kwenye kituo cha mafuta, matenki ya kuhifadhia mafuta yanafukiwa chini ya ardhi. Hivyo, hata moto ukitokea si rahisi mafuta yaliyo ndani ya matenki hayo kulipuka.

Mada hii imelenga kutoa maelezo kwa kifupi juu ya ujenzi wa vituo vya gharama nafuu kwa kuelezea vitu muhimu na vya msingi vinavyotakiwa kuzingatiwa wakati wa kujenga kituo cha mafuta pamoja na makadirio ya gharama ya kukamilisha ujenzi wa kituo. Vilevile, mada hii inaelezea kanuni za ujenzi wa vituo vijijini ambazo zilitungwa mahsusi kwa ajili ya kupunguza gharama za uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini.

Lengo la mada ni kuona ya kwamba, watu wa Vijijini wanakuwa na haki sawa na watu wa Mijini katika upatikanaji wa bidhaa ya mafuta kwa hali ya ubora na usalama unaohitajika na kwa bei nafuu.

Ni matumaini ya kwamba, mada hii itatoa mwanga kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa mafuta ya petroli nchini namna ambavyo uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini unavyoweza kufanywa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watumiaji wa mafuta hayo kupata huduma nzuri zaidi na salama bila kumuathiri mfanyabiashara wa mafuta unayeamua kuwekeza Kijijini.

Mahitaji na Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Ujenzi.
lli uweze kujenga kituo unatakiwa kuzingatia yafutatayo:

(i) Uwe na 'kiwanja ambacho Mamlaka husika (mfano: Halmashauri ya kijiji) imeridhia kitumike kwa ajili ya biashara ya kituo cha mafuta. lli kukidhi viwango vya usalama (safety distance requirements), kiwanja kinachofaa kujenga kituo cha mafuta kinatakiwa angalau kiwe na ukubwa wa mita za mraba 400.

(ii) Uwe angalau na tenki moja (1) la kuhifadhia mafuta. Kama utauza aina zaidi ya moja ya mafuta, matenki yaongezeke sawia. Tenki liwe na ujazo wa angalau lita 4,500 au 5,000.
Uwe na pampu yenye mkono mmoja au miwili kulingana na aina za mafuta.

(iii) Bomba nne(4) za chuma za inchi nne (inchi ) na urefu wa mita tano (mita 5) kwa ajili ya kujengea paa (canopy). Pia, utahitaji bomba za inchi moja au inchi 1.5 na bati kwa ajili ya kenchi na kuezeka. Bomba za kenchi zinatakiwa kuwa na urefu wa mita saba (mita 7).

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa ujenzi:

(a) Matenki ya kuhifadhia mafuta yanatakiwa kufukiwa chini ya ardhi. Inatakiwa umakini wakati wa kuchimba na kuweka tenki chini ya ardhi. Kwa sehemu ambazo maji ya ardhini (water table) yapo karibu, ni vizuri matenki yakajengewa zege.

(b) Matenki yapakwe rangi ya kuzuia kutu. Pia, matenki yanatakiwa yafukiwe na mchanga kwa ajili ya kuzuia kutu.

(c) Kituo kinatakiwa kisakafiwe na zege imara la angalau inchi nne (inchi 4). Eneo mahsusi la kusakafia ni eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta. Eneo linalozunguka pampu liwe na ukubwa wa angalu mita za mraba 45 (yaani upana mita 6.4 na urefu mita 7). Eneo la kushushia mafuta linatakiwa liwe na ukubwa wa angalau mita za mraba 16 (yaani upana mita 4 na urefu mita 4) ili gari la mafuta liweze kusimama kwenye zege hiyo wakati wa kushusha mafuta.

(d) Eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta ijengewe mitaro ambayo inayoelekea kwenda kwenye chemba ya kuchuja mafuta na maji (Oil/water separator). Chemba ya kuchuja mafuta na maji inatakiwa iwe na vyumba vitatu. Kila chumba kiwe na urefu wa mita moja (mita 1), upana mita mbili (mita 2) na kina mita moja (mita 1). Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo. Usitumie zege, ili iwe rahisi wakati wa kusafisha.

(e) Kituo kinatakiwa kiwe na paa imara (canopy). Paa linatakiwa kuwa na urefu wa mita 5.

(f) Ni vyema kutumia wahandisi wa ujenzi au mafundi wenye uzoefu wa ujenzi wa vituo vya mafuta.

Makadrio ya Gharama za Ujenzi wa kituo cha kujaza mafuta.

(i) Ardhi/kiwanja: gharama kwa aina moja au mbili za mafuta inategemea thamani ya ardhi ya sehemu husika.

(ii) Matenki angalau mawili yenye ujazo wa lita 5,000 kwa bei ya sh 5,000,000 Tsh kila moja.

(ii) Pampu moja mpya yenye uwezo wa kuuza aina mbili za mafuta 15,000,000 Tsh.

(iii) Kusakafia kwa zege eneo la kuuzia na kushushia mafuta takribani mita za mraba 61 kwa: Gharama kwa aina moja ya mafuta 5,000,000 Tsh na kwa aina mbili za mafuta 5,000,000 Tsh.

(iii) Kujenga paa (canopy): Gharama kwa aina moja au mbili za mafuta 5,000,000 Tsh.

Angalizo gharama hizo zinaweza kubadilika kutokana na hali halisi ya soko.

Tahadhari: Usijenge kituo bila kufuata kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo.

Zifuatazo ni kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vya kujaza mafuta vijijini
EWURA imeandaa Kanuni mahsusi kwa ajili ya ujenzi na biashara ya vituo vya mafuta vijijini. Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayetaka kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate kibali cha EWURA. Kupata kibali unatakiwa kuwasilisha maombi EWURA. Pia, kabla ya kuanza biashara unatakiwa kuwa na leseni ya EWURA. Leseni hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote na baada ya hapo, EWURA inafanya ukaguzi wa kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.

Je mahitaji hayo ni yepi?

Mahitaji ya kuzingatia kabla ya kujenga kituo cha mafuta

Yafuatayo ni mahitaji ya kuzingatia kabla ya kujenga kituo cha mafuta. Ili maombi yaweze kupokelewa na EWURA ni kutuma maombi kupitia mtandao .

Zifuatavyo ni nyalaka za kuambatinisha wakati wa maombi:

(i) nakala za nyalaka zifuatazo zilizothibitiswa na mwanasheria:

(a) Cheti cha utambulisho wa kulipa kodi (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA);

(b) Hati miliki au nyaraka yoyote kutoka Mamlaka husika inayoruhusu matumizi ya eneo kwa ajili ya kituo cha mafuta. Kwa maeneo ya vijijini ambayo hayajapimwa ni hati ya kimila (Mhutasari wa kikao cha kijiji unaoidhinisha uhalali wa kumiliki eneo hilo na kuruhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha mafuta);

(c) Mkataba wa pango/mauziano kama siyo mmiliki wa eneo;

(d) Kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika;

(e) Cheti cha tathimini ya athali za Mazingira (Environmental Impact Assessment Certificate) kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC). Kwa vituo vya vijijini, barua ya ukaguzi wa mazingira kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya inayothibitisha kuwa hilo ni salama na mradi huo hautasababisha athari yoyote mbaya kwenye mazingira;

(f) Kitambulisho cha uraia;

(ii) Mchoro wa kituo cha mafuta uliosainiwa na Mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahandisi (Layout Plan for the petrol station duly signed by registered engineer/district engineer);

(a) Ukionyesha vitu vyote vinavyotegemewa kujengwa kwenye kituo husika

(b) Umbali kati ya matenki, pampu na vitu vitu vyote vitakavyojengwa kwenye kituo

(iii) Ada ya maombi ambayo ni sh. 50,000 Tsh inayo ni kwa njia ya mtandao wa maombi.

Mengineyo:
(i) Kwa ushauri kuhusu maswala ya gesi na mafuta karibu.

(ii) Lakini pia kwa uhitaji wa kuandikiwa propozo za kuanzisha miradi ya vituo vya mafuta na kudizani ramani za vituo vya mafuta vidogo kwa vikubwa karibuni.

(iii) Nakukumbusha kuwa nyumba yako itakua salama endapo kama mtungi wa gesi ya kupikia (LPG) utahifadhiwa mahali penye hewa ya kutosha nje ya nyumba yako, na kupitisha mpira wa gesi kupitia ukutani au dirishani mpaka kwenye jiko lako jikoni.

(iv) Pika salama lala kwa amani bila hofu.

Mawasiliano:
Whatsap/piga +255747744895/+255687746471


Kama unahitaji msaada wa kuandika na kuhariri documents zako mbalimbali, tunayo habari njema kwako!

Bright and Genius Editors wapo hapa kukusaidia.
Tunatoa huduma za uandishi na uhariri wa documents za aina zote.

Wasiliana nasi kwa njia yoyote upendayo:

Piga/WhatsApp : +255687746471/+255612607426
WeChat ID: bandg_editors
Barua pepe: bandg.editors@gmail.com/submit@bgeditors.com/contact@bgeditors.com


Pia, unaweza kutembelea tovuti yetu www.bgeditors.com, Bright & Genius Editors kujifunza zaidi kuhusu huduma zetu na kufanya maombi yako moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu.
 
Mkuu unamaanisha kwa milion 50 naweza miliki sheli.
Vp biashara hii hutoa percentage ngap ya faida per litre
Inategemea jinsi EWURA na makampuni walivyopanga. Mfano chukua mfano huu wa mwezi may ilikua ni hii:

161.18 Tsh per lita kwa petroli

160.7 Tsh per lita kwa dizeli

159.36 Tsh per lita kwa mafuta ya taa
 
Back
Top Bottom