Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!
Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.
Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;
1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo
2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama
3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20
4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.
5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.
6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.
7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.
8. Zipo Kata ambazo hazina mawasiliano ya simu
9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.
10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu
11. Na mengine mengi madogo madogo.
Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo:
1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?
Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga.
Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!
Nawasilisha!