Regia,WC,kwanza nashukuru kwa comments zako zote,ni very positive zenye lengo la kusaidia nchi..
Katika post yako hii labda nami nikuulize unadhani nchi yetu tatizo ni kukosekana kwa fedha?Unafikiri Bunge likiwa dogo ndio haya matatizo yatakwisha?unadhani hili ndio primary solution,nifafanulie and then tujadiliane kwa kina!
Tatizo sio kukosekana kwa fedha. Ni jinsi tunavyozitumia bila kuwa na vipaumbele vyetu kama NCHI. Fedha nyingi sana zinaelekezwa kwenye siasa na wanasiasa kama wewe. Hapo nimetoa mfano wa ukubwa wa BUNGE letu la sasa na anasa zake ambazo wewe unazifahamu kwa sasa. Fikiria tuondoe viti maalum na kisha kila Halmashauri/ Manispaa/ mji uwe na Mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa kama ilivyo Igunga. Tutakuwa tumeokoa kiasi gani cha fedha kwa mwaka? Pili ni ruzuku kwa vyama vya siasa. Kama makanisa, NGOs, misikiti na asasi nyingine zinajiendesha zenyewe kwa kutumia michango ya wanachama wao na njia zingine kwanini vyama vya SIASA vipewe kodi zetu hata tusio na vyama kujiendesha? Tutaokoa kiasi gani ruzuku hii isipolipwa kwa vyama hivi?
Sio hilo tu. Angalia na serikali yetu ilivyo pana na kubwa. Angalia vyeo vya kisiasa vinavyolipwa na gharama za kuviendesha. Tunavyoigharamia SIASA ndivyo huduma za kijamii zinavyodorora kwa kasi ya ajabu halafu unamtaka Rostam atumie utajiri wake kuijenga Igunga?