Kwa hili Gazeti la Mwanahalisi liwaombe radhi Watanzania

Kubenea yuko sawa tu. Yaani hapo wote wachafu. Kuanzia Muhando na wenzie mpaka Waziri na wenzie. Wote kwa wakati wao na mahala pao ni wachafu. Hakuna anayechafuliwa hapo.
 
Mkuu hapa haitakiwi ushabiki, angalia content ya habari yenyewe. Hatukatai Gazeti ni zuri, na kwa uzuri wake ni rahisi kuamininiwa na wananchi. Ingekuwa UHURU NA MZALENDO tusingehangaika. Ila kwa hili ni vema watumie busara kuomba radhi kwani wamejichafua kutetea ufisadi

Maovu ya Mhando na watendaji wa TANESCO hayajaanza leo kuanikwa hadharani...!! Uzuri ni kwamba, katika kashfa hii ya TANESCO wamehusishwa hadi wanasiasa ambao wana majukwaa ya kuzungumza pasipo kumwogopa yeyote! Katibu Mkuu Maswi amewachana TANESCO hadharani pasipo kuumauuma maneno!! Jana, Profesa Muhongo nae amewachana hadharani pasipo kuuma uma maneno!! Sasa basi, hao ni wakati wa hao watuhumiwa kujitokeza na kuyasema mabaya ya Maswi hadharani badala ya kupita kulialia kwenye magazeti ambayo; kimsingi hakuna gazeti hata moja TZ lililo huru!! Pamoja na kudai kwamba Maswi ameteka mkataba wa tenda na kuupeleka kwa Puma Energy lakini hajatokea yeyote anayesema Maswi amelipwa shilingi ngapi zaidi tu ya kulalamika kwamba amekiuka sheria! Kama kukiuka sheria kunaweza kuokoa fedha za Watanzania basi kwangu inaweza kuwa ni heri zaidi kuliko kufuata sheria ambazo zinawanyonya Watanzania! Ukiangalia vizuri habari hiyo ya Mwanahalisi utaona wazi kwamba walichotaka kufanya ni ku-dissolve yale yanasemwa dhidi ya Mhando! Hata hivyo, ukiisoma kwa makini utakuta jinsi ambavyo confidence ya Mwanahalisi haipo kabisa kwenye habari hiyo! Kilichofanywa na kambi ya Mhando ni kwamba, baada ya kuona Raia Mwema wametoka na habari inayoeleza ufisadi wa vigogo wa TANESCO, ndipo nao wakaamua kutafuta gazeti ambalo linaaminika kidogo!!! Hakika hapa, ni ama Mwanahalsi wametumika au hawakufanya utafiti wa kutosha!!
 
ritz kashomeshwa ccm kivukoni haoni wala hasikii ni kansa ya ubongo ukishaipenda ccm maana ni sawa na dini ya mashetani hawajui kama kuna mungu wala ubinadamu

Hahaaaaa ritz kasomeshwa chuo cha mwalimu nyerere(ccm kivukoni enzi hizo) lol
 
Taarifa iliyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi kumponda Katibu wa nishati na madini imeonesha Gazeti hili liliandika bila kufanya utafiti. Ukweli halisi tumeupata siku bajeti ilipowasilishwa na Prof Mhongo. Ni vema gazeti hili liwaombe radhi watanzania. Soma habari yenyewe:

Richmond mpya wizara ya nishati

1d23274bb5fde0b0c6e9fc4cebb1be42.jpg

Na Jacob Daffi - Imechapwa 25 July 2012

maswi_304.jpg

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi anakabiliwa na lundo la tuhuma ikiwa ni pamoja na kilichoitwa kujipa mamlaka ya kuendesha Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco), imefahamika. Aidha, Maswi anatuhumiwa kushinikiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, William Mhando bila kufuata taratibu na kanuni za ajira yake.

Katibu mkuu huyo anatuhumiwa pia kukiuka baadhi ya taratibu, ikiwamo kufanya manunuzi kinyume cha sheria na kuingiza shirika katika mikataba tata. Taarifa zinasema Maswi ndiye aliyeshinikiza Mhando kusimamishwa kazi kwa maslahi binafsi. Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kuwa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco haikutaka kumfukuza Mhando hadi ipate kwanza baraka za mamlaka ya uteuzi (rais); lakini shinikizo lilitoka kwa Maswi.

Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Jenerali Robert Mboma amethibitisha kufanyika maamuzi hayo bila kufuata taratibu.
"Ni kweli, kulikuwa na hoja ya kumsimamisha kazi Mhando, lakini nilisema uamuzi usitangazwe mpaka nimpe taarifa Mhe. Rais Jakaya Kikwete; naye anipe kibali kwa sababu yule ni mteuliwa wake…lakini ndiyo hivyo tena. Ikatangazwa kabla ya Jumatatu ya 16 Julai," ameeleza.

Lakini kiongozi mmoja ndani ya bodi ya Tanesco ameeleza, "Huyu bwana ndiye amekuwa mtendaji wa Tanesco. Jambo hili na mengine ambayo bado hayajafumuka, yamemuudhi sana mwenyekiti." Akitaka kuthibitisha madai hayo, mtoa taarifa amesema Maswi ndiye anahusika na kuipa kazi kampuni ya BP (T) Ltd., ya kusambaza mafuta ya kuzalishia umeme wa IPTL, yenye thamani ya zaidi ya Sh. 28 bilioni.

Taarifa zinasema ni Maswi aliyeagiza BP kuuza mafuta yake kwa Tanesco wakati kampuni hiyo ilienguliwa kwenye zabuni; jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) ya mwaka 2004. Sakata la Richmond ambalo linaendelea kuitesa serikali, lilitokana na kampuni hiyo kupewa mkataba wa kufua umeme kwa upendeleo baada ya kushindwa kwenye zabuni.

Inadaiwa Maswi alifanya maamuzi kama hayo kwa BP, tena bila kushirikisha Mhando. Taarifa zinasema pia ni kwa "vitendo vya hatari vya aina hiyo, vya kuingiza shirika katika mgogoro wa kisheria," Jenerali Mboma ameamua kuripoti kwa Rais Kikwete.
Bali Maswi aliwaambia waandishi wa habari juzi Jumatatu, ofisini kwake, Dar es Salaam kuwa hahusiki na tuhuma hizo kwa vile alipoingia wizarani hapo mchakato huo ulikuwa tayari umeanza.

Lakini alipoulizwa na MwanaHALISI, aligoma kuzungumzia suala hilo, badala yake alitaka mwandishi kwenda ofisini kwake kuchukua taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinathibitisha jinsi Maswi alivyokuwa wakala wa BP, mratibu, msimamizi, mlipaji na mnunuzi wa mafuta hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za umma.

"Ndugu yangu, katika mazingira haya, ni nani anayepaswa kuchunguzwa kati ya katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando," amehoji mjumbe mmoja wa bodi ya Tanesco. Taarifa zinamuonyesha Maswi akipokea hati ya kabla ya malipo – Profoma Invoice – iliyoambata na ujumbe wa barua pepe kutoka meneja masoko ya BP (sasa Puma Ltd), Machumani Shebe uliosema, "…itakuwa ni vema zaidi kama utaweza kutupatia nyaraka rasmi za jambo hili kiofisi."
Anasema,

"Naomba tupate barua ya uthibitisho wa malipo kutoka wizarani kwako ili kuwa na uhakika wa malipo. Tunataka pia utupatie LPO (ankara ya malipo) ya kiwango cha mafuta kitakachosambazwa." Akiandika kwa njia ya kushukuru, Shebe anasema, "Tunakushukuru kwa kutupatia biashara hii na tunatarajia kusikia kinachoendelea kutoka kwako hivi mapema iwezekanavyo."

Mara baada ya kupata ujumbe huo kutoka BP, Maswi alimwandikia ujumbe naibu mkurugenzi mtendaji wa Tanesco anayeshughulikia uzalishaji, Boniface Njombe, tarehe 12 Julai 2012 kumwamuru kuandaa malipo hayo haraka iwezekanavyo. Barua ya Maswi kwenda kwa Njombe, ilinakiliwa kwa Mhando na Decklan Mhaiki, ambaye ni naibu mkurugenzi wa shirika anayeshughulikia usambazaji umeme.
Kwa kasi ya aina yake, siku hiyohiyo ya 12 Julai, Njombe alimwagiza Anetha Chengula wa idara ya uhasibu, kuandaa malipo kwa kile alichoita, "Utekelezaji wa maelekezo ya Maswi."

"Bila shaka unakumbuka juu ya jambo hili. Tupo wizarani hapa na tumepokea hati malipo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini iliyotoka Puma (BP) watakaosambaza HFO kwa ajili ya mitambo ya IPTL," ameeleza Njombe katika barua yake kwa Chengula. Amesema, "Malipo hayo yatafanywa na wizara ya nishati na madini kama ambavyo tulikubaliana. Hivyo unatakiwa kuandaa malipo ya mafuta hayo haraka kwa msambazaji na unijulishe."

MwanaHALISI lilipomuuza Mboma kuhusu madai hayo, alikiri kuwa shirika lake halijawahi kuipa kazi kampuni ya BP. Alisema, "Mimi ninachofahamu ni kwamba TANESCO ina-deal (inashughulika) na makampuni yale matatu yaliyokuwa na sifa. Sifahamu jingine nje ya hapo."

Mbali na kulazimisha kulipwa fedha hizo, Maswi amedaiwa kuzuia Sh. 36 milioni kutoka Wizara ya Fedha (Hazina) ambazo ni sehemu ya fedha zilizoombwa na Tanesco serikalini. Tanesco iliomba, tarehe 22 Septemba 2011, Sh. 136 bilioni kwa ajili ya gharama za kuendesha mitambo ya dharura ya umeme. Ilitarajia kuzirejesha baada ya kupata mkopo wake mkubwa wa Sh. 408 bilioni ambazo shirika hilo liliahidiwa.

Akiwa kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, Maswi anadaiwa kukata Sh. 36 bilioni na kuipa Tanesco Sh. 100 bilioni. Inadaiwa alitoa maelezo kuwa kiasi kilichokatwa kitafuta mkopo wa Sh. 20 bilioni katika benki ya CRDB. Katika barua yake ya 28 Septemba 2011 yenye kumb. Na. AB.88/286/01/15 kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Maswi anaeleza kuwa kiasi kilichobaki cha Sh. 16 bilioni kingetumika kununulia mafuta mazito kwa mitambo ya IPTL kwa mwezi Oktoba 2011 kutoka Puma/BP.

Mhandisi Mhando alisimamishwa kazi 13 Julai 2012 pamoja na maofisa watatu waandamizi – Naibu Mkurugenzi, Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Manunuzi, Harun Mattambo kwa kilichoitwa "madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu."

Gazeti toleo lenye makala hii

Nani anayo cv ya kubenea jamani,atuwekee hapa
 
Hili gazeti ni bingwa la kuandika udaku na majungu siku zote uwa naliweka kundi moja na KIU, UWAZI. leo baada ya bajeti kusomwa limeabika kwa majungu.

Ukweli daima unauma hususani kwa wale wasiopenda kuambiwa ukweli mngekuwa na uwezo wakuyafuta mngeanza na mwanahalisi,raia mwema na tanzania daima jambo leo lina damu yenu.Uzuri wa wananchi wa leo wanauwezo wa kumbembua pumba na mchele. Ritz zile enzi za Always boss is right zilishapitwa na wakati.Hizo bil 3 ambazo unasema Maswi ameokoa ni sawa ila mgao wake utakapo wekwa hadharani utashangaa.Baada ya Mhando kuanikwa the next ni Maswi ni mengi hatuyajui wait n see
 
Mkuu mie sio bendera fuata upepo ebu niambie wewe mwenye uchungu na nchi hizo tuhuma na makosa ya Eliakim Maswi yako wapi mie nachofahamu huyu Katibu Wizara Nishati na Madini Eliakim Maswi uamuzi wake umeokoa bilioni 3 kwa kila juma pesa ambayo ilikuwa inakwenda mifukoni kwa wajanja.

kwa hili kaka tupo pamoja
mafisadi ni lazima wakemewe,tusiwape nafasi kabisa,kama wameweza kuwarubuni wabunge ili wampige chini waziri na katibu wake,je watashindwa kuwanunuwa akina mwanahalisi?
 
Ingawa ni habari za kumtetea mhando! Hakika hizi habari si za uwongo ni za kweli kabisa. hii imetokana na sheria zete kuwalinda wafanyakazi hata kama wanafanya wizi au uzembe. Kwa alichofanya Maswi ni kama vile uku mitaani ukikamata mwizi choma moto ingawa sheria haziruhusu. hivyo Maswi kamchoma moto Mhando kwa ubadhirifu ingawa sheria zinambana. Swali la kuwauliza mwanahalisi ukiona mtu anahujumu uchumi makusudi utamwacha eti sheria inamlinda? Hongera Maswi maana huyu Daffi ndiye angekukaanga baadaye kama ungeacha uchafu huu utendeke!
 
Taarifa iliyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi kumponda Katibu wa nishati na madini imeonesha Gazeti hili liliandika bila kufanya utafiti. Ukweli halisi tumeupata siku bajeti ilipowasilishwa na Prof Mhongo. Ni vema gazeti hili liwaombe radhi watanzania. Soma habari yenyewe:

Richmond mpya wizara ya nishati

1d23274bb5fde0b0c6e9fc4cebb1be42.jpg

Na Jacob Daffi - Imechapwa 25 July 2012

maswi_304.jpg

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi anakabiliwa na lundo la tuhuma ikiwa ni pamoja na kilichoitwa kujipa mamlaka ya kuendesha Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco), imefahamika. Aidha, Maswi anatuhumiwa kushinikiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, William Mhando bila kufuata taratibu na kanuni za ajira yake.

Katibu mkuu huyo anatuhumiwa pia kukiuka baadhi ya taratibu, ikiwamo kufanya manunuzi kinyume cha sheria na kuingiza shirika katika mikataba tata. Taarifa zinasema Maswi ndiye aliyeshinikiza Mhando kusimamishwa kazi kwa maslahi binafsi. Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kuwa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco haikutaka kumfukuza Mhando hadi ipate kwanza baraka za mamlaka ya uteuzi (rais); lakini shinikizo lilitoka kwa Maswi.

Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Jenerali Robert Mboma amethibitisha kufanyika maamuzi hayo bila kufuata taratibu.
“Ni kweli, kulikuwa na hoja ya kumsimamisha kazi Mhando, lakini nilisema uamuzi usitangazwe mpaka nimpe taarifa Mhe. Rais Jakaya Kikwete; naye anipe kibali kwa sababu yule ni mteuliwa wake…lakini ndiyo hivyo tena. Ikatangazwa kabla ya Jumatatu ya 16 Julai,” ameeleza.

Lakini kiongozi mmoja ndani ya bodi ya Tanesco ameeleza, “Huyu bwana ndiye amekuwa mtendaji wa Tanesco. Jambo hili na mengine ambayo bado hayajafumuka, yamemuudhi sana mwenyekiti.” Akitaka kuthibitisha madai hayo, mtoa taarifa amesema Maswi ndiye anahusika na kuipa kazi kampuni ya BP (T) Ltd., ya kusambaza mafuta ya kuzalishia umeme wa IPTL, yenye thamani ya zaidi ya Sh. 28 bilioni.

Taarifa zinasema ni Maswi aliyeagiza BP kuuza mafuta yake kwa Tanesco wakati kampuni hiyo ilienguliwa kwenye zabuni; jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) ya mwaka 2004. Sakata la Richmond ambalo linaendelea kuitesa serikali, lilitokana na kampuni hiyo kupewa mkataba wa kufua umeme kwa upendeleo baada ya kushindwa kwenye zabuni.

Inadaiwa Maswi alifanya maamuzi kama hayo kwa BP, tena bila kushirikisha Mhando. Taarifa zinasema pia ni kwa “vitendo vya hatari vya aina hiyo, vya kuingiza shirika katika mgogoro wa kisheria,” Jenerali Mboma ameamua kuripoti kwa Rais Kikwete.
Bali Maswi aliwaambia waandishi wa habari juzi Jumatatu, ofisini kwake, Dar es Salaam kuwa hahusiki na tuhuma hizo kwa vile alipoingia wizarani hapo mchakato huo ulikuwa tayari umeanza.

Lakini alipoulizwa na MwanaHALISI, aligoma kuzungumzia suala hilo, badala yake alitaka mwandishi kwenda ofisini kwake kuchukua taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinathibitisha jinsi Maswi alivyokuwa wakala wa BP, mratibu, msimamizi, mlipaji na mnunuzi wa mafuta hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za umma.

“Ndugu yangu, katika mazingira haya, ni nani anayepaswa kuchunguzwa kati ya katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando,” amehoji mjumbe mmoja wa bodi ya Tanesco. Taarifa zinamuonyesha Maswi akipokea hati ya kabla ya malipo – Profoma Invoice – iliyoambata na ujumbe wa barua pepe kutoka meneja masoko ya BP (sasa Puma Ltd), Machumani Shebe uliosema, “…itakuwa ni vema zaidi kama utaweza kutupatia nyaraka rasmi za jambo hili kiofisi.”
Anasema,

“Naomba tupate barua ya uthibitisho wa malipo kutoka wizarani kwako ili kuwa na uhakika wa malipo. Tunataka pia utupatie LPO (ankara ya malipo) ya kiwango cha mafuta kitakachosambazwa.” Akiandika kwa njia ya kushukuru, Shebe anasema, “Tunakushukuru kwa kutupatia biashara hii na tunatarajia kusikia kinachoendelea kutoka kwako hivi mapema iwezekanavyo.”

Mara baada ya kupata ujumbe huo kutoka BP, Maswi alimwandikia ujumbe naibu mkurugenzi mtendaji wa Tanesco anayeshughulikia uzalishaji, Boniface Njombe, tarehe 12 Julai 2012 kumwamuru kuandaa malipo hayo haraka iwezekanavyo. Barua ya Maswi kwenda kwa Njombe, ilinakiliwa kwa Mhando na Decklan Mhaiki, ambaye ni naibu mkurugenzi wa shirika anayeshughulikia usambazaji umeme.
Kwa kasi ya aina yake, siku hiyohiyo ya 12 Julai, Njombe alimwagiza Anetha Chengula wa idara ya uhasibu, kuandaa malipo kwa kile alichoita, “Utekelezaji wa maelekezo ya Maswi.”

“Bila shaka unakumbuka juu ya jambo hili. Tupo wizarani hapa na tumepokea hati malipo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini iliyotoka Puma (BP) watakaosambaza HFO kwa ajili ya mitambo ya IPTL,” ameeleza Njombe katika barua yake kwa Chengula. Amesema, “Malipo hayo yatafanywa na wizara ya nishati na madini kama ambavyo tulikubaliana. Hivyo unatakiwa kuandaa malipo ya mafuta hayo haraka kwa msambazaji na unijulishe.”

MwanaHALISI lilipomuuza Mboma kuhusu madai hayo, alikiri kuwa shirika lake halijawahi kuipa kazi kampuni ya BP. Alisema, “Mimi ninachofahamu ni kwamba TANESCO ina-deal (inashughulika) na makampuni yale matatu yaliyokuwa na sifa. Sifahamu jingine nje ya hapo.”

Mbali na kulazimisha kulipwa fedha hizo, Maswi amedaiwa kuzuia Sh. 36 milioni kutoka Wizara ya Fedha (Hazina) ambazo ni sehemu ya fedha zilizoombwa na Tanesco serikalini. Tanesco iliomba, tarehe 22 Septemba 2011, Sh. 136 bilioni kwa ajili ya gharama za kuendesha mitambo ya dharura ya umeme. Ilitarajia kuzirejesha baada ya kupata mkopo wake mkubwa wa Sh. 408 bilioni ambazo shirika hilo liliahidiwa.

Akiwa kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, Maswi anadaiwa kukata Sh. 36 bilioni na kuipa Tanesco Sh. 100 bilioni. Inadaiwa alitoa maelezo kuwa kiasi kilichokatwa kitafuta mkopo wa Sh. 20 bilioni katika benki ya CRDB. Katika barua yake ya 28 Septemba 2011 yenye kumb. Na. AB.88/286/01/15 kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Maswi anaeleza kuwa kiasi kilichobaki cha Sh. 16 bilioni kingetumika kununulia mafuta mazito kwa mitambo ya IPTL kwa mwezi Oktoba 2011 kutoka Puma/BP.

Mhandisi Mhando alisimamishwa kazi 13 Julai 2012 pamoja na maofisa watatu waandamizi – Naibu Mkurugenzi, Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Manunuzi, Harun Mattambo kwa kilichoitwa “madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu.”

Gazeti toleo lenye makala hii

Pesa pesa sabuni ya roho. ukiona hivyo ujue kuna mtu alinunua siku ile ili kufunika kombe mwanaharamu apite. lakini Mungu ni mwema
 
Mwanahalisi ni gazeti bora kuliko yote Tanzania,tungekuwa na magazeti matatu tu ya aina hii maendeleo yangepatikana. Linafanya mambo yake kwa utafiti mkubwa,ona hata Usalama wa taifa umeshindwa kujibu kwa ufasaha no. za simu kama ni za watumishi wao au laa. Kwa hili naona hawana haja ya kuwaomba Watanzania radhi kwani wana uhakika na walichoandika.
 
Ritz,
Kwa mtu kama wewe ambaye una mahaba na Uhuru,Mzalendo, Tazama, na Habari leo, kamwe huwezi kuona thamani ya Mwanahalisi. Kwa Tanzania yetu hii, usipokuwa na mahaba na Mwanahalisi na Raia Mwema, basi kamwe hutoweza kufikiri nje ya box, na siku zote utaona contents za magazeti haya ni upuuzi kwako. Hili linasababishwa na uwezo wako, mazoea uliyonayo, akili yako ulivyoitune, na hasa pale yanapofunua yale maovu unayoyasapoti katika jamii, ni hakika utaichukia.
Mkuu sema ana mapenzi na magazeti hayo. Mahaba yanajumuisha kurembua pamoja na mambo mengine.
 
Jamani unajua hakuna mtu wa kumwani asilimia mia hapo> Usie ukashangaa baadaye kugundua kwamba pia kulikuwa na mizengwe kuipatia puma deal vilevile. Mimi hizi habari bado nazichukulia kwa tahadhari. Sija'side' na upande wowote bado. Lazima kuna a 'dead fish' somewhere!

Baadhi ya wabunge walitumia pesa kuteuliwa kuwa wagombea ubunge, walitumia pesa kuhonga wapiga kura ili wawachague sasa watashindwaje kupokea rushwa ili warejeshe gharama hii. Nachofurahi ni kwamba hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyosomwa na mhe. Mnyika ipo very clear kuhusu mazingira yaliyo dhahiri ya rushwa katika sakata zina la ununuzi wa mafuta unaotetewa na baadhi ya wabunge wakiwemo akina ole sendeka. Kilichonifurahisha kingine ni namna mbunge wa Rombo alivyoeleza jinsi rushwa isivyo na mipaka ya chama, kabila, rangi, itikadi, n.k. Kwa kusema hivyo, alimaanisha kwamba hata wabunge wa cdm wanaweza kuwa involved katika rushwa.
 
Back
Top Bottom