Kwa haya CHADEMA mnakosea

Kwanza nikiri kuwa mimi ni mwanachama muadilifu wa CHADEMA.Ili kukijenga ni lazima tuseme ukweli pale yanapofanyika mambo ambayo yanaweza tuharibia focus yetu ya mbio za ikulu 2015.
1.Suala la shibuda
inafahamika na kila mwanachadema kuwa shibuda ni mamluki.si mara moja anaenda tofauti na misimamo ya chama kwa lengo la kukidhoofisha.Kwa kila mwenye kufikiria vizuri hawezi kusita kuconclude kwamba shibuda anatumiwa.kuijibizana naye ni kupoteza muda,kwa nn tusipuuzie hoja zote anazotoa na kusonga mbele kuliko kujibizana naye.Ameshafaulu kuleta mfarakano BAVICHA kwani kwa jicho la haraka naona mambo sio shwari.TUACHANE NA SHIBUDA TUSIPOMJIBU ATAACHA KUONGEA.
2.Suala la lema na mawaziri wanaotaka kuhamia chadema.
Hata kama waliotajwa walikuwa wameomba kujiunga na chadema kulikuwa na haja gani kutangaza hadharani kabla ya muda muafaka....wanavokanusha hadharani tunaonekana tuna siasa za kizushi kwanini lema asisubiri mpaka siku wao wenyewe watakapotangaza kuhama CCM.Nadhani ni muda muafaka wa kupima maneno yetu kabla hatujatoa kwenye kadamnasi ili kujenga chama chetu.
NAOMBA KUWAKILISHA
Nakuunga mkono kwa 100% Ni lazima hekima na busara itumike, la sivyo makosa kama hayo ambayo chadema wanafanya yanaweza kuwaondolea imani ya wananchi. Kamwe hawataweza kushika dola kama wananchi watapoteza imani nao.
 
Sasa nyinyi mnategemea chadema kuna uongozi?

Mwenyekiti ansema hilo ni swala la kidemokrasia anakuja Katibu Mkuu anasema hilo swala si chochote.

Mwenyekiti BAVICHAa anasema Shibuda kakosa anakuja Naibu Mwenyekitiwa hiyo hiyo BAVICHAa anasema Mwenyekiti wake ndio mwenye makosa.

Hapo sasa! Uongozi utoke wapi na mumuamini nani?

CHADEMA Siasa maji 'taka'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom