nahavache
JF-Expert Member
- Apr 3, 2009
- 871
- 246
nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari jinsi suala la ugonjwa wa mh. Mwakyembe jinsi linavyopelekwa ni dhahili inaonekana kuna namna wananchi tunalazimisha tuwe wepesi wa kuamini giza ni mwanga.
Waziri huyu anasema hili mwingine anasema vile utafikili wanafanya kazi ktk serikali tofauti, ndugu wana jf kwa sakata hili nimejikuta nakosa imani kabisa na taarifa zilizosababisha vifo vya waheshimiwa wengine kwa mfano.
Mh. Kolimba.
Mh. Chacha wangwe.
Mh. Kambona.
Mh.kombe.
Mh.balali.
Na wengineo !
Hivyo basi kwa kuwa serikali yetu imekuwa na tabia ya kupotosha ukweli, naomba mwenye kujua ukweli na uhalisia wa vifo vya hawa ndugu zetu basi naomba auweke hapa.
Pia unaweza ongeza na mtu mwingine ambaye kifo na taarifa ya kifo chake havikwenda sawia.
Asanteni......!
Hakuna haja ya kuongezea. Lakini unatakiwa ukumbuke kuwa sometimes watu wanauawa kwa ajili ya amani na utulivu wa nchi. Hata kile kikosi tulichoambiwa kuwa kimemuua Osama Bin Laden, nacho kimeuawa kwa sababu ya kiusalama. Inaelekea hao jamaa uliowataja hapo juu wana siri nzito na walikuwa hawaaminiwi saana na watawala. Watu kama Kolimba, Balali, Kombe na wengineo, walikuwa na siri nzito saana.