MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Naona kuna changes kubwa sana barani Afrika juu ya chaguzi kuu za nchi mbali mbali barani Afrika,watu wameshavichoka vyana tawala na vikongwe,hawana imani navyo tena, wanaona kama ndivyo vilivyochelewesha maendeleo ya nchi hizo.
Tuliona Nigeria hali ilivyokua, tumeshuhudia chaguzi ndogo kule Afrika kusini chama cha ANC kilivyopoteza, tumeona Zambia walivyoponea chupu chupu japo nao walikua katika utawala wa upinzani juzi , Ya Gambia tumeyaona na Leo hii Ghana tunaona hali ilivyo.Vyama vikongwe vya muda mrefu kwa sasa havina Sera tena, viebaki kutegemea nguvu za dola kwa kutumia mabavu na vimebaki kuendelea kuogoza kwa mazoea tu.
Ikumbukwe kua huku kwetu Tanzania CCM imebebwa na jina la mtu mmoja tu na sio chama chenyewe,sijui akiondoka huyo mtu mmoja CCM watakua katika hali ipi, siuuoni uhai wa CCM tena.Inawezekana kabisa kua kuna watanzania ambao wamekwishachoshwa hata na jina lenyewe ambalo limekuwepo masikioni tangu nchi ipate Uhuru.
Nawapa moyo sana vijana ambao wanachipukia katika Sasa waliopo ndani ya CCM lakini wakae wakijua kua ni muda wowote Kamba inaweza kukatika, kama wewe bado ni damu mpya ya siasa ndani ya CCM na una maono marefu ya mbali, kwakweli uhai wa CCM u mashakani labda wabadili jina chama ili kionekane kipya. Matumaini yako ndani ya chama hiki kikongwe hayawezi kutimia, sio rahisi kutimia. Ni bora kuongeza nguvu kujenga vyama ambavyo havina muda mrefu ambayo wananchi wanayo matumani huenda vikawa na ukombozi kutoka shida wapatazo na sio CCM ambayo haijawahi kuleta mabadiliko yanayoridhisha toka nchi ipate Uhuru.
Kuna mwalimu Wangu mmoja wa biology aliwahi kiusema kua "ukizaliwa uapitia hatua zote za maisha,utazeeka na mwisho utakufa tu" Hivyo CCM kwa umri wa CCM sasa ni sawa na mzee,kimeshazeeka ni mzee ambaye sasa hata maradhi makali yakimkumba matumaini ya kuishi ni madogo sana.