Kwa anayewafahamu hawa financialfreedomtz

Jolebatawi

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
549
230
Wana JF hawa financialfreedomtz walitoa tangazo lao la ajira lililokuwa linasomeka kuwa "Are you a graduate?" sasa hawa jamaa wamenipigia simu niende kwenye interview leo saa tisa pale shinyanga motel ila bado sijafahamu hawa watu wanajihusisha na nini hasa hapa tanzania! hivyo kwa anayewajua hawa jamaa naomba atiririke hapa ikiwezekana na mishahara yao huwa ikoje?
ASANTE
 
Uliombaje ajira kwa usiowafahamu? Na hiyo barua ya maombi utakuwa uliandika nini? Ktk interview swali mojawapo laweza kuwa unaielewaje hiyo organisation, sasa utajibu nini?
 
...Duh! hizi thread nyingine! Great Thinker unaomba kazi kwenye shirika ambalo hujui linashughulika na nini halafu unakuja kutuuliza sisi shirika uliloomba kazi linashughulika na nini?? Kwanza wakijua ni wewe hata hio Interview waliyokuitia wataifuta!
kweli hii nchi ni Muungano wa Zimbabwe na Tanzania One Nineteen Sixty Four a.k.a 11964...
!
 
hii kubwa kuliko.....only in Tanzania.....halafu leo ni siku ya kazi....?
 
wadau hawa jamaa hata tangazo lao lilikuwa too short coz walitaka watu wenye degree yoyote na wenye knowledge kidogo ya bussiness *ila hawakujieleza vizuri kuwa wao wanadeal na nini hasa na walihitaji muombaji atume cv tu na si vinginevyo ndio maana nimeuliza hivyo.
 
Wana JF hawa financialfreedomtz walitoa tangazo lao la ajira lililokuwa linasomeka kuwa "Are you a graduate?" sasa hawa jamaa wamenipigia simu niende kwenye interview leo saa tisa pale shinyanga motel ila bado sijafahamu hawa watu wanajihusisha na nini hasa hapa tanzania! hivyo kwa anayewajua hawa jamaa naomba atiririke hapa ikiwezekana na mishahara yao huwa ikoje?
ASANTE

Hapo kwenye RED wewe mwenyewe unajidhihilisha jinsi ulivyo kilaza, au mwenzetu wewe ni mmoja kati ya wale tunaowasema wanapata kazi kwa vi MEMO?
 
Hujui wanashughulika na nini sasa interview utafanyaje. Wakisema wanashughulika na kufundisha ushoga utafanyeje sasa. We nenda kwenye interview then utakuja utuelezea wanashughulika na nn sawa? Good luck.
 
Hahahahahahah!!!! Unachekesha saana wewe kilaza yawezekana inch yako iko east cost!!!! Ukiwa na maana inchi yako iko ukanda pwani ya mashariki!!
 
wadau hawa jamaa hata tangazo lao lilikuwa too short coz walitaka watu wenye degree yoyote na wenye knowledge kidogo ya bussiness *ila hawakujieleza vizuri kuwa wao wanadeal na nini hasa na walihitaji muombaji atume cv tu na si vinginevyo ndio maana nimeuliza hivyo.

...Tangazo lao kuwa short na kutoeleza wanashughulika na nini ndio ilikuwa sababu tosha kwa wewe Great Thinker Kuacha kuwagusa hata kwa Upondo wa Futi Mia, sembuse kuwaandikia na kuwapa CV yako!!
 
kimsingi hao ni wasanii tuuu, hata mimi naweza andika tangazo la kazi hapa na nikasema nahitaji graduates then nikalipost zoom tanzania najua watu wataomba tu kazi kwahiyo usjsumbue kwanza leo ni siku ya sikukuu how come ukafanye interview leo!! wizi mtupu
 
Wana JF hawa financialfreedomtz walitoa tangazo lao la ajira lililokuwa linasomeka kuwa "Are you a graduate?" sasa hawa jamaa wamenipigia simu niende kwenye interview leo saa tisa pale shinyanga motel ila bado sijafahamu hawa watu wanajihusisha na nini hasa hapa tanzania! hivyo kwa anayewajua hawa jamaa naomba atiririke hapa ikiwezekana na mishahara yao huwa ikoje?
ASANTE

Watakuwa wanahitaji machinga wakuuza dawa ya meno ya aloe vera buku buku nk sasa wanajua graduate lazima atabuni jinsi ya kuuza. Hata hivyo kwanini interview inafanyiwa kwenye motel? ogopa sana
 
Back
Top Bottom