Mnaosema kwenye maisha kuna bahati

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Nasimulia hapa true stori ya maisha yangu huenda ikamsaidia mwingine hasa anayepita njia nilizopita.

Ipo hivi, mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto tisa (tuliohai tupo sita nashukuru MUNGU kwa zawadi hii ya uhai) kati ya watoto tisa mimi tisa watano ni kiume na nne wa kike, katika kua yangu nikiwa mtoto nilikuwa na matumaini makubwa sana ya maisha na mafanikio kupitia shule (baba yangu alilkuwa mwalimu so alinisisitiza sana kusoma na asante darasani nilikuwa na uwezo wa juu.

Namba moja nimeshika sana darasani hadi A level, (nazani umefahamu kitu ukiwa na uwezo mzuri shule halafu mtoto wa mwalimu unapendwa na walimu)

Nilipomaliza A level matokeo yalitoka vizuri one yangu point 7, nikachaguliwa kujiunga mzumbe sikumbuki vizuri jina la course iliikuwa human rosource and public administration, baada ya kuchaguliwa mzumbe nikaona sio poa hiyo course ikabidi niende chuo kingine ambacho TCU walinipangia course ya sheria (LLB)
Kipindi nasoma LLB nilikuwa nina imani kubwa ya kutoboa maisha kupitia shule, picha linanza baada ya kumaliza chuo, nilianza kwa kuomba kazi ya sheria kwenye makampuni huko napekeka barua sijibiwi, nikaona noma nikabadili upepo nikanza kuomba nafasi kwenye law firm kila nikipita humo nambiwa wamejaa hakuna nafasi (mara unasikia rafiki zangu nipo law firm flan dada yangu kaniunganisha na wakili flan)

Siku zinaenda nazidi kupauka kurudi nyumbani naona noma hapo naishi kwa binamu (namshukuru shemeji yule mwanamke hakuwahi kuninyanyasa) mzee unangalia tv inachosha ee bwana mademu wamekata si nakawa najishikiza kwa beki tatu nakula mzigo tu hapo(namshukuru yule beki alikuwa msaada sana kipindi kigumu kile)

Kuna mwaka zikatoka nafasi jeshi la polisi niliomba interview kurasini nikatoswa (wenzangu wakakapata kumbe wana connection) zilitoka nafasi jkt nikakosa (jamaa yangu wa karibu ananionyesha form na interview hajafanya) mzee zikatoka nafasi magereza na zimamoto kote mzee nikakosa) utumishi nimefanya sana interview nikawa sipati kazi kabisa,so baada ya kuona ramani haisomi ilibidi nikubali kurudi home (hapo wenzangu wengine wapo law school na wengine wanapishwa)

Niliporudi home kipindi hicho mzee wangu anaumwa sukari inamtafuna hatari, katika mazungumzo baba aliniambia nibaki home nisimamie miradi yake na kipindi hicho miradi yake imechoka kweli (Kabaki na mashamba hayalimwi, mifugo iyobaki ni ngombe wawili, isuzu limepaki juu ya mawe halitengeneziki biashara kaisha funga, so hapo home maisha yanaenda kwa kukusanya kodi za nyumba (nyumba zilikuwepo za kutosha wapangaji kama 36, na misada toka kwa kaka zangu (my dad was unsung hero pamoja na kuwa alikuwa mwalimu alitengeneza sana njia (namuombea aliko apumzike na naumia hajakula pesa yangu) miezi michache mbele mzee akafariki.

Baada ya mzee kufariki kikao cha familia kikamua nibaki home atleast nimtunze mama na ikiwezekana nisimamie miradi, by the time mzee anafariki kacha deni hapo bank kama milion kumi, so baada ya kikao na wanafamilia wakatawanyika wakaniacha hapo home dah mashamba yapo mtaji wa kulimia huna, gari utatengenezea nini, ukiwafuata wapangaji wanakujibu jeuri eti baba yako alikuwa hatudai kama wewe, nikaona isiwe tabu nikipat pesa ni kunywa bia flani zilikuwa zinaitwa eagle.

Katika kula pombe siku moja nimekutana na jamaa flani ni mwalimu, yule mwalimu tukafahamiana then akaniambia yeye ni mwalimu wa postgraduate, so nikamuliza uliza kuhusu ajira za ualimu jamaa akanifungukia, thanks ule ulikuwa msimu wa kuomba vyuo mzee nikaomba open universty nakapata hiyo course ya postgraduate, mzee ada natoa wapi ikabidi niuze vipuli vya machine ya kukoboa na kusaga mahindi nikapata pesa kama 1.5 m hiyo imeuzwa bi mkubwa hajui, mzee nikanza kusoma nilifanya siri sikuwahi mwambia mtu hata mmoja nilikuwa naona noma lawyer unasoma ualimu.

Baada ya kumaliza ilibidi nifanye mchakato wa kwenda Dodoma tamisemi, nikakutana na mlinzi nilipanga kweli yule msukuma ikabidi aniunginesh n jamaa flani pale tamisemi (lengo l kwenda tamisemi ni kuwa ajira zikitoka nipangwe jombe habari ya kuwa mwalimu mwanza halafu salary laki nne na nusu sikutaka kabisa)

Ule mwaka nimemaliza post ni 2014 nambiwa ajira za ualimu hakuna labda kwa sababu ni uchaguzi zinaweza kutoka ila walimu wamejaa, dah nikawa naona noma naumia na siri yangu na bi mkubwa kaishavurugika kagundua machine imeuzwa, anawambia kaka zangu nipishe pale home dah maana naharibu mali za marehemu tu, thanks 2015 ajira zilitoka yule jamaa wa dodoma alinifanyia mpango nikapata huu mkoa wa Njombe.

Nilopoanza kazi niliamua kuuza msitu wa pine mmoja na kufufua shamba la parachichi. Hiilo shamba nilikuwa nalifahamu mimi tu kwa sababu baba alikuwa amenionyesha mali zake zote, na alishanitambulisha kwa wafanya biashara wenzake. kiufupi najiuliza bahati ni zipi sababu mtaji wangu wote wa kwanza ulikata with no reason, baada ya kuanza biashara, thanks nilianza vizuri na nikapata mentor aliyenifundisha biashara za kupeleka mazao nje ya nchi Na kuingiza yasiyokuwepo, nimeuza kiazi, mchele na nimeingiza karanga n kitungu swaumu , changamoto ninayokutana nayo ni kuwa kila ninayekaa naye kwenye hizi biashara ananishauri nitafte dawa kujilinda na kulinda biashara( hadi sasa sipo tayari na kweli mtaji haukui aisee ) , ukiwa unaleta mizigo hapa tanzania jamaa wanaoitwa mamlaka za serikali wanapenda rushwa sana na kuweka kauzibe hakuna watu wa hovyo kama wanaojita serikali , kutapeliwa kupo nje nje kuziwa mzigo ulioharibika nimewahi uziwa karanga gunia 25 kati ya gunia ya gunia 60 zilikuwa mbovu, kiufupi huku changamoto ni nyingi kuliko mtaji hasa bahati ipo wapi 2. maisha ya kazini ( walimu ni watu wenye majungu ever) mwalimu unamsaidia ( anakukopa unamkopesha) then anatengenez kashfa nimekutana visa vya kijinga shuleni acheni tu , sijawahi kupata hata senti tano nje ya salary yaani no seminar, no kusimamia , no kumark mitihani ( necta) , 3. shambani ni kugumu sana kipindi hiki yes unauza ulichozalisha je cost za uzalishaji zipoje, so najiuliza where is bahati mbona kila pesa ninayosaka ina vikwazo sana kiufupi maisha yangu nikipata buku kuwa nimefanya kazi, sijabahati kusaidiwa kila nilichonacho ni matokeo ya jitahada zangu binafsi
 
Japo kuandiki kuna chosha lakini ukifupisha stori yako huku ukielekea lengo la stori huwa inapendeza sana.
 
Maisha kwa ujumla wake sio ya njia moja kwamba yanyooke tu au yapande tu au yawe na kona kona nyii la!

Kupanda kushuka ni kanuni msingi ya maisha, kuanza vizuri na kumaliza vizuri si kwa kila mtu, kuanza vizuri na kumaliza vibaya kupo na kadhalika kuanza vibaya kisha ukamaliza vizuri kupo pia, kwa hiyo mapito yoyote sio mapya wala ya mwisho au ya kipekee bali kila mmoja wetu ana Kutana nayo.
 
Hii michezo ya 'itaendelea' inatukwaza Sana yaani.

Hivi hamjui hata mama anapita humu, hamuoni vibaya kumsumbua na kumkwaza mama??

Aaaa!ghh
Itaendelea iko kichwani mwako, mleta uzi haimhusu.
 
Nasimulia hapa true stori ya maisha yangu huenda ikamsaidia mwingine hasa anayepita njia nilizopita.

Ipo hivi, mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto tisa (tuliohai tupo sita nashukuru MUNGU kwa zawadi hii ya uhai) kati ya watoto tisa mimi tisa watano ni kiume na nne wa kike, katika kua yangu nikiwa mtoto nilikuwa na matumaini makubwa sana ya maisha na mafanikio kupitia shule (baba yangu alilkuwa mwalimu so alinisisitiza sana kusoma na asante darasani nilikuwa na uwezo wa juu.

Namba moja nimeshika sana darasani hadi A level, (nazani umefahamu kitu ukiwa na uwezo mzuri shule halafu mtoto wa mwalimu unapendwa na walimu)

Nilipomaliza A level matokeo yalitoka vizuri one yangu point 7, nikachaguliwa kujiunga mzumbe sikumbuki vizuri jina la course iliikuwa human rosource and public administration, baada ya kuchaguliwa mzumbe nikaona sio poa hiyo course ikabidi niende chuo kingine ambacho TCU walinipangia course ya sheria (LLB)

Kipindi nasoma LLB nilikuwa nina imani kubwa ya kutoboa maisha kupitia shule, picha linanza baada ya kumaliza chuo, nilianza kwa kuomba kazi ya sheria kwenye makampuni huko napekeka barua sijibiwi, nikaona noma nikabadili upepo nikanza kuomba nafasi kwenye law firm kila nikipita humo nambiwa wamejaa hakuna nafasi (mara unasikia rafiki zangu nipo law firm flan dada yangu kaniunganisha na wakili flan)

Siku zinaenda nazidi kupauka kurudi nyumbani naona noma hapo naishi kwa binamu (namshukuru shemeji yule mwanamke hakuwahi kuninyanyasa) mzee unangalia tv inachosha ee bwana mademu wamekata si nakawa najishikiza kwa beki tatu nakula mzigo tu hapo(namshukuru yule beki alikuwa msaada sana kipindi kigumu kile)

Kuna mwaka zikatoka nafasi jeshi la polisi niliomba interview kurasini nikatoswa (wenzangu wakakapata kumbe wana connection) zilitoka nafasi jkt nikakosa (jamaa yangu wa karibu ananionyesha form na interview hajafanya) mzee zikatoka nafasi magereza na zimamoto kote mzee nikakosa) utumishi nimefanya sana interview nikawa sipati kazi kabisa,so baada ya kuona ramani haisomi ilibidi nikubali kurudi home (hapo wenzangu wengine wapo law school na wengine wanapishwa)

Niliporudi home kipindi hicho mzee wangu anaumwa sukari inamtafuna hatari, katika mazungumzo baba aliniambia nibaki home nisimamie miradi yake na kipindi hicho miradi yake imechoka kweli (Kabaki na mashamba hayalimwi, mifugo iyobaki ni ngombe wawili, isuzu limepaki juu ya mawe halitengeneziki biashara kaisha funga, so hapo home maisha yanaenda kwa kukusanya kodi za nyumba (nyumba zilikuwepo za kutosha wapangaji kama 36, na misada toka kwa kaka zangu (my dad was unsung hero pamoja na kuwa alikuwa mwalimu alitengeneza sana njia (namuombea aliko apumzike na naumia hajakula pesa yangu) miezi michache mbele mzee akafariki.
Baada ya mzee kufariki kikao cha familia kikamua nibaki home atleast nimtunze mama na ikiwezekana nisimamie miradi, by the time mzee anafariki kacha deni hapo bank kama milion kumi, so baada ya kikao na wanafamilia wakatawanyika wakaniacha hapo home dah mashamba yapo mtaji wa kulimia huna, gari utatengenezea nini, ukiwafuata wapangaji wanakujibu jeuri eti baba yako alikuwa hatudai kama wewe, nikaona isiwe tabu nikipat pesa ni kunywa bia flani zilikuwa zinaitwa eagle.

Katika kula pombe siku moja nimekutana na jamaa flani ni mwalimu, yule mwalimu tukafahamiana then akaniambia yeye ni mwalimu wa postgraduate, so nikamuliza uliza kuhusu ajira za ualimu jamaa akanifungukia, thanks ule ulikuwa msimu wa kuomba vyuo mzee nikaomba open universty nakapata hiyo course ya postgraduate, mzee ada natoa wapi ikabidi niuze vipuli vya machine ya kukoboa na kusaga mahindi nikapata pesa kama 1.5 m hiyo imeuzwa bi mkubwa hajui, mzee nikanza kusoma nilifanya siri sikuwahi mwambia mtu hata mmoja nilikuwa naona noma lawyer unasoma ualimu.

Baada ya kumaliz ilibidi nifanye mchakato wa kwenda Dodoma tamisemi, nikakutana na mlinzi nilipanga kweli yule msukuma ikabidi aniunginesh n jamaa flani pale tamisemi (lengo l kwenda tamisemi ni kuwa ajira zikitoka nipangwe jombe habari ya kuwa mwalimu mwanza halafu salary laki nne na nusu sikutaka kabisa)

Ule mwaka nimemaliza post ni 2014 nambiwa ajira za ualimu hakuna labda kwa sababu ni uchaguzi zinaweza kutoka ila walimu wamejaa, dah nikawa naona noma naumia na siri yangu na bi mkubwa kaishavurugika kagundua machine imeuzwa, anawambia kaka zangu nipishe pale home dah maana naharibu mali za marehemu tu, thanks 2015 ajira zilitoka yule jamaa wa dodoma alinifanyia mpango nikapata huu mkoa wa Njombe.

Nilopoanza kazi niliamua kuuza msitu wa pine mmoja na kufufua shamba la parachichi. Hiilo shamba nilikuwa nalifahamu mimi tu kwa sababu baba alikuwa amenionyesha mali zake zote, na alishanitambulisha kwa wafanya biashara wenzake.
Na uanasheria wako ulishindwa hata kukusanya Kodi ya pango? Unategemea kuajiriwa tu!
 
so hapo home maisha yanaenda kwa kukusanya kodi za nyumba (nyumba zilikuwepo za kutosha wapangaji kama 36, na misada toka kwa kaka zangu
Sasa wewe ni maisha bora kwa watanzania wengi teyari ulikuwa na pakuanzia.
 
Back
Top Bottom