paartey
Member
- Jun 26, 2023
- 39
- 53
KWAAJILI YAKO MAIMUNA
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 01
MAWASILIANO: 0783642467
ANZA NAYO.........
Rehema mwana mama wa miaka 63 aliyejaaliwa watoto wawili wakike na wakiume ambao kwa umri huo wa mama yao tayali walikuwa ni watu wazima na kwakuwa familia yao ilikuwa ya kimasikini sana walisimama kwa pamoja kumsaidia mama yao ambaye yeye pia aliwalea watoto hao kwa shida sana tangu baba yao mzazi alipofariki.
Rajabu na shyna ndio watoto halali wa bi rehema lakini pia kulikuwa na binti aliyekuwa akiitwa maumuna.
Maimuna hakuachana umri mbali na rajabu kwani rajabu ndio alikuwa wa kwanza kuzaliwa kisha akafatia shyna hivyo basi kama maimuna angekuwa ni mtoto wa bi rehema maimuna angekuwa ni mtoto wa pili kuzaliwa....
Maimuna aliokotwa na bi rehema akiwa na umri wa miaka 12, bi rehema alimfanya maimuna kama mtoto wake na kila mtu alimtambulisha kuwa maimuna ni binti yake, lakini bado maimuna alitofautiana vingi sana na watoto wa bi rehema maimuna alikuwa na mwili mkubwa, shape ya kwenda na rangi fulani hivi wale watu wa ovyo wanasemaga karangi ka kuchanganya watu, alikuwa mweupe kiufupi halafu alienda hewani (mrefu ) na umbo lake liliwachanganya wanaume wengi Sana wa pale mtaani kwao uswazi, tofauti nyingine ambayo maimuna alikuwa nayo ukiambatanisha na wenzie maimuna alikuwa mvivu mno yaani kwenye kazi mvivu sana anachojua ni kula kulala lakini pia kuna kile kitu ambacho kinaitwa uchoyo kwa maimuna tunatoa uchoyo tunaweka roho mbaya .
SONGA NAYO......
Bi rehema alikua mgonjwa sana kwa kipindi iko kutokana na umri kwenda ukichanganya na unene aliokuwa nao ndio kabisa presha ndio ugonjwa wake mkubwa hivyo ni alikuwa mtu wa nyumbani na watoto zake ndio walikuwa wakitafuta uku na uku
"Maimuna mama kaniletee maji ya kunywa binti yangu "
"We nawe unachosha sasa aaah kila muda kutuma tu kwani uwezi nyanyuka....."
Alifoka maimuna baada ya bi rehema kumuagiza maji
"Nisaidie tu binti yangu Nisaidie jamani "
"Tusisumbuane...."
Alijibu maimuna na aliona kama anachoshwa aliinuka na kuondoka eneo ilo maimuna alichokuwa anakijua ni kuchezea simu yake tu hakuna kitu kingine anaweza kufanya
"Maimuna....."
Aliita bi rehema na muda huo alikohoa mfululizo na hakupata msaada, alijikaza na kufata maji ya kunywa mwenyewe na baada ya kunywa akajisikia nafuu....
Majila ya jioni alirudi shyna na na beseni lake la mboga mboga na matunda
"Shikamoo mama...."
"Marahaba za utokako ??"
"Aaah uko hali mbaya mama kama uonavyo matunda kama yote Yamebaki lakini pia nashukuru ata mboga zimeisha....."
"Mungu mkubwa pole mwaya na mchoko naona una vumbi hadi usoni mwanangu "
"Mama nawe vumbi kawaida, maimuna yuko wapi ??"
"Eeeh sijui kaenda wapi, kaninunulia vichipsi hapa nimekula naona katokomea "
"Kikubwa amekununulia kitu cha kula, vipi dawa ??"
"Eeeeh nimesahau kunywa mwayaa niletee "
"Ona mama nawe kama mtoto lakini maimuna anajua muda wako wa Dawa "
"Aaah maimuna anachoka na yeye si unaona usafi wa nyumba na kila kitu "
"Lakini ni majukumu yake ye amekataa kubeba beseni la mboga basi nyumbani anatakiwa kitimiza wajibu wake....."
"Mambo madogo hayo...."
"We bibi, maimuna kakununulia chipsi saa ngapi ?? Me si ndo nimekupa miogo hapo na kukufanyia usafi ??"
Alidakia mama rukia ambaye alikuwa ni jilani yao wa karibu sana na kuishi nao vizuri wakawa kama ndugu muda mwingi alikuwa karibu kumtazama bi rehema pale tu watoto zake wanapokuwa wameenda kutafuta
"Aaah jilani utani gani bhana
..."
"Mama ebu kaa kimya umesema usafi umefanya wewe ?? Maimuna alikuwa anafanya nini ??"
"Yuko bize na simu yake "
Shyna alichukia sana na kumuangalia mama yake kwa hasira lakini hakumlaumu wala kumfokea kwani ni mkubwa wake na hakutaka kumkosea mama yake alibaki na hasira zake.
Alitoa mboga za majani na kuanza kuandaa, lakini alionesha wazi kabisa kuwa alikuwa na hasira na muda mfupi tu akaingia maimuna yaani muda wote na simu yake alipomuona shyna akaweka simu yake mfukoni haraka
"Eeeh umerudi ngoja nikusaidie kupika...."
Shyna alimtazama tu kisha akatabasamu
"Pumzika umechoka sana kufanya usafi lakini pia kupika mchana na kila kitu nitapika "
"Jamani we ndo unachoka sana mdogo wangu Sawa nitafanya umetembea Juani siku nzima...."
Yaani hapo shyna hasira ndio ilikuwa ikiongezeka lakini mwisho wa siku shyna ndio alipika maimuna alifurahia hiyo ofa....
Majila ya saa 6 usiku rajabu ndio aliwasili nyumbani akiwa amechoka sana kwakuwa nyumba yao ilikuaa tu ya nje akatoa fungo yake na kufungua mlango kisha kuingia ndani muda mfupi hodi ikasikika mlangoni mwake
"Atakuwa nani usiku huu "
Alijiuliza rajabu lakini ni kama mtu wa nje alisikia hivi akaitika
"Ni mimi shyna fungua...."
Aliposikiwa kuwa ni dada yake haraka akatoka nje mawazo yake walimpeleka mbali sana aliamini uenda mama amezidiwa, maana shynaa na maimuna ndio walikuwa wakilala na bi rehema ...
"Mbona saa hizi kuna shida ??"
Aliuliza rajabu baada ya kufungua mlango
"Ndio ...."
"Shida gani mama anaendeleaje yuko sawa....??"
"Achana na mama yuko sawa na amepumzika, ni kuhusu maimuna tabia zake zinazidi kunikela kila siku "
"Lakini kuhusu yeye si ulinipigia tukaongea jamani au kuna kingine ??"
"Ilo ilo we unaona ni dogo yaani afanyi chochote sasa fikilia isingekuwa mama rukia mama angekula nini leo ?? Halafu mambo ya kuniambia nimuache kwakuwa ni mkubwa kwangu sitaki yaani ni mkubwa sawa lakini ukubwa wake wa kijinga mno...."
"Nitazungumza nae kesho niko ofu "
"Eeeh kwa mara ya kwanza umepata ofu "
"Yaaah wameongezeka wahudumu wawili si unajua upande wa wahudumu wa bar tulikuwa wawili tu sasa yupo wanne...."
"Kwakweli kesho upate usingizi mzuri kaka yangu "
"Nitalala nikirudi mtaani maana nitaingia kuuza matunda "
Nyie hii familia hata kama ndio masikini ila ilibarikiwa umoja na akili ya utafutaji yaani kwa uzuri wa rajabu kwa watu ninaowajua mimi hakuna mtu angeweza kubeba beseni la matunda na kutembea nalo.
Basi dada na kaka walimaliza mazungumzo yao na kila mtu akaingia chumbani na kulala....
Asubuhi kama kawaida walisaidiana kuchota maji na kufanya usafi mwingine ilikuwa ni asubuhi sana na majila ya saa 1 asubuhi maimuna akabeba beseni la mboga na rajabu akabeba beseni la matunda wakaingia mtaani....
Majila ya saa 7 maimuna akarudi na beseni la mboga likiwa vilevile yaani aliuza mafungu mawili tu
"Eeeh nimechoka jamani...."
Alizungumza baada tu ya kushusha beseni la mboga
"Weeeeh mboga zote hizi na umerudi nyumbani....??"
Aliuliza shyna maana alishangazwa na kitendo cha maimuna kuwao kurudi akiwa na mboga nyingi sana....
"Wateja wamekuwa shida sana"
"Ndio maana nilitaka kwenda mimi uko mtaani "
Alizungumza shyna kwa hasira akaingia ndani na kumuaga mama yake kisha akabeba beseni na kuingia tena mtaani
"Na rangi hii nipigwe na jua mie...."
Muda huo huo alilambwa Kofi moja zito la mgongoni
...
"Mama.....🥹"
Alishtuka na kuita mama
"Maimuna wewe huoni umuhimu wa hii kazi sio ?? Unajali rangi yako tu si ndio ??"
Alifoka bi rehema na aliamua kusimama sasa kama mama na siku hiyo alikuwa na afueni...
"We nawe usinisumbue unanifananisha me na vipanya vyako
......"
Yaani maimuna alikuwa na dharau ya waziwazi kwa bi rehema akiamini kuwa hakuna kitu anaweza akamfanya, lakini kwa rajabu na shyna alikuwa akiwaigizia na kujifanya mtoto mwema...
Bi rehema aliendelea kulalamika maimuna akamsukuma bi rehema ambaye alianguka kama mzigo kisha yeye akaingia ndani
"Maimuna unaniua mtoto wewe...."
Alilia bi rehema...
"Tena koma me sio binti yako
...."
Alizungumza maimuna uku akitokomea mtaani kwenda kuzulula....
ITAENDELEA