Kuyafanya Meno Yenye Rangi Kuwa Meupe (Teeth Whitening)

apo sijakuelewa...

[U]internal bleaching: inside out[/U]
dentist anatoboa tundu kwenye pulp chamber, halafa anasafisha,anaziba na root canal inakuwa-filled na material fuluni hivi ya mpira(rubber-like substance) pia anaweka perioxide gell kwenye pulp chamber ili hiyo gel iweze kufanya kazi moja kwa moja ndani ya jino kwenye layer inaitwa dentin layer. hiyo perioxide inakuwa ndani ya jino kwa mda wa siku kadhaa na kutokana na changes dentist anaweza weka nyingine tena.
hii njia kama unavyoona sio simple process, kutokana na hali ya meno inaweza kutumika, meno mengine hupeteza rangi kutokana na internal straining by blood au fluids ambazo zinaweza kuvujia kwenye jino sasa hapa hii njia inafaa sana.
kwa kifupi internal straining inaweza kusabibishwa na vitu kama vile certain medications ambazo mtu alitumia wakati wa teeth formation (kwamfano tetracyline),pia mtu anaweza kuwe exposed kwenye flouride nyingi wakati wa teeth formation, pia teeth injuries zinasababisha meno kutokuwa meupe.


external bleaching: outside in
jel(hydrogen peroxide) inawekwa kwenye teeth surface, inaanza kupambana na uchafu wa juujuu mpaka jino linakuwa jeupe.
hii njia inafaa sana kwa meno ambayo yamepoteza rangi kutokana na vitu kama sigara,kahawa,vyakula vyenye spice nyingi,masala n.k
 
Naomba mwenye updates za kinachoendelea kuhusu huyu bwana anayeitwa zitto,yaani zitto-chadema,zitto-kafulila,zitto-kutembea na barua ya kujiuzuru,zitto-mama zitto,zitto-chuo,zitto-mbowe,zitto-slaa,zitto-urais
 
teh teh teh, huko chini mkuu hakufai, achana nako kabisaa....utatapika sana......

hahaha...itabidi sisi ambao hatajawahi kufika huko tufute kabisa mawazo ya kwenda huko down.
basi wanaoenda huko ni wabishi, duh!
 
teh teh teh, huko chini mkuu hakufai, achana nako kabisaa....utatapika sana......

nimekupata, tuwaachie wazoefu. Ingawa wadai ukienda chini unajiwekea guarantee ya kutokupigwa kubuti. Tunakuja na style mpya,hakuna kwenda chini na hakuna kibuti...
 
nimekupata, tuwaachie wazoefu. Ingawa wadai ukienda chini unajiwekea guarantee ya kutokupigwa kubuti. Tunakuja na style mpya,hakuna kwenda chini na hakuna kibuti...
teh teh teh, unaweza enda chini na ukala za uso! akipata mjuzi zaidi unaweza kukimbiwa vile vile....
 
Naomba mwenye updates za kinachoendelea kuhusu huyu bwana anayeitwa zitto,yaani zitto-chadema,zitto-kafulila,zitto-kutembea na barua ya kujiuzuru,zitto-mama zitto,zitto-chuo,zitto-mbowe,zitto-slaa,zitto-urais
mkuu, nadhani kwenye jukwaa la SIASA watakusaidia sana...
 
zamani wakati nilikuwa mdogo nikiwa Iringa, Njombe nakumbuka kulikuwa na mti mmoja tulikuwa tunauita mdaha ulikuwa ukitafuna majani yake hata magome yake mdomo, I mean ulimi unakuwa na rangi nzuri ya orange kama umekunywa mirinda lakini meno yakuwa meupe pe na yanameremeta. ingawa ulikuwa ukiutafuna sana unakosa ladha ya chakula kwa muda mfupi sana then inarudi.. i wish ningeupata huu mti tena nafikiri hii ni dawa nzuri sana ya meno walioko Njombe mtujuze.
 
zamani wakati nilikuwa mdogo nikiwa Iringa, Njombe nakumbuka kulikuwa na mti mmoja tulikuwa tunauita mdaha ulikuwa ukitafuna majani yake hata magome yake mdomo, I mean ulimi unakuwa na rangi nzuri ya orange kama umekunywa mirinda lakini meno yakuwa meupe pe na yanameremeta. ingawa ulikuwa ukiutafuna sana unakosa ladha ya chakula kwa muda mfupi sana then inarudi.. i wish ningeupata huu mti tena nafikiri hii ni dawa nzuri sana ya meno walioko Njombe mtujuze.
well noted!
 
Wadau naomba kuuliza kama kuna yeyote anayefahamu kliniki nzuri ya meno iliyopo Dar es salaam ambapo unaweza kwenda kusafisha meno .

Ninataka nisafishe meno yangu na kuwa meupe.
 
Nenda kwa Doctor Gupta pale around clock tower na Nkurumah street,has very long experience and profession manner.
 
Nenda kwa Doctor Gupta pale around clock tower na Nkurumah street,has very long experience and profession manner.

Haha nillipoona jina Gupta nimekumbuka post moja inaonyedsha ma Dr wa meno huko india wanavyoshughulikia meno ya watu lol, ni balaa, hope huyu atakuwa somehow good
 
Wakati wa muongo uliopita mahitaji ya kuboresha muonekano au kurembesha meno yameongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika nchi zilizoendelea. Hii imechochewa na kupatikana kemikali mpya za meno (dental

meterials) na vifaa kwa kasi ikiendana na kuboresha vile vya zamani. Sehemu nyingine iliyosababisha madaktari na mainjinia wa meno kuyafanya meno kuwa meupe ni sehemu ya fani ya taaluma ya meno chini ya urembeshaji wa meno, fani hii uhusika na kuboresha muonekano wa meno hasa yale yanayoonekana wakati

wa kutabasamu na kuongea. Inahusisha matibabu kama kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe, kunyoosha meno yaliyojipanga vibaya pamoja na kukarabati meno yaliyovunjika na yale yaliyoumbika visivyo (malformed teeth). Huko Uingereza na sehemu nyingine za magharibi wanawake walio wengi wanatumia maelfu ya paundi/euro kuboresha muonekano wa meno yao hali ambayo inaanza pia kuingia huku kwetu.


Nini husababisha meno kugeuka rangi?
Meno kugeuka rangi husababishwa na kimojwapo au muunganiko wa vitu vifutavyo: -


Vyakula na vinywaji kama vile vinyaji vyenye kaboni, wine na sigara.
Utumiaji wa maji yenye kiwango cha juu cha madini aina ya magadi (fluoride) na utumiaji wa magadi katika kulainisha vyakula wakati wa kuandaa vyakula vigumu kama maharage na makande. Utafiti uliofanywa na Prof.

Mabelya na wenzake nchini Tanzania umeonesha kuwa kubadilika kwa rangi ya meno kutokana na magadi kwa kiwango kikubwa husababishwa na matumizi ya magadi katika mapishi ya vyakula hasa makande kule maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro/Moshi kuliko inavosababishwa na matumizi ya maji.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ngumu za jino (enamel and dentine defects). Iwapo sehemu ngumu ya meno imeumbwa ikiwa laini ni rahisi kufyonza rangi na jino kuota likiwa limegeuka rangi au kubadilika baada ya kuota.

Matumizi ya madawa kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayajapata madini ya kutosha na hata watoto wachanga ambao meno yao hayajakomaa.
Kufa kwa kiini cha jino hasa kutoka na kujigonga wakati wa ajali au kupigana ngumi usoni (pulp necrosis), jino

likigongwa kwa nguvu damu huvuja ndani ya kiini cha jino na baadaye huchachuliwa na kutoa kemikali ambayo hupenya kwenye vitundu vidogo vidogo kwenye dentine na kujidhihirisha kama kijivu, zambarau au hata

nyeusi. Hali hii yaweza tokea mapema baada ya kupata ajali lakini wakati mwingine inaweza kuchukua miaka kadhaa hata arobaini kipindi ambapo mtu hakumbuki kuwa aliwahi kutwangwa ngumi.

Kuyafanya meno yenye rangi yasimpendeza mwenye nayo kuwa meupe
(Bleaching or teeth whitening)

Huku ni kuyafanya meno yenye rangi kuwa meupe au kuongeza weupe wa yale yenye rangi ya kawaida kufikia kiwango cha weupe atakacho muhitaji kwa kutumia kemikali maalum. Rangi ya kawaida ya meno kwa walio wengi ni uweupe kama wa maziwa (milky white). Rangi yeyote nje ya hiyo si ya kawaida (abnormal color or discoloration).


Kuwa na rangi isiyo ya kwaida hasa kwa meno ya mbele linaweza kuwa tatizo kubwa la urembo na kumsumbua mhusika kisaikolojia. Kuyafanya meno kuwa meupe kumelenga kuwaondolea wahusika tatizo hili japo mafanikio yake yanategemea kiwango cha rangi isiyo ya kawaida.


Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia kemikali, kunaweza kubadili yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kutoka yale yaliyoathirika kwa kiwango kidogo mpaka cha kati.


Kufanya meno yawe meupe kwa kutumia kemikali huunguza (oxidises) rangi ya jino na kuiondoa. Kemikali zinazotumika zina hydrogen peroxide 30%-35% na baadhi carbamide peroxide 10%. Kemikali hizi huweza kuondoa rangi zilizosababishwa na vyakula, vinywaji, dawa za tetracycline, rangi kidogo iliyotokana na utumiaji

wa madini ya magadi kwenye vyakula au kwenye maji (mild fluorosis) na meno yenye rangi ya njano au kijivu itokanayo na umri kuwa mkubwa. Inaweza pia kuondoa rangi itokanayo na uvutaji wa sigara na matumizi ya ugoro. Kwa wavutaji wa sigara sharti waache pindi watumiapo kemikali hizi kwani muunganiko wa hydrogen

peroxide na kemikali zilizopo kwenye moshi wa sigara unahisiwa kuongeza madhara zaidi ambayo tayari moshi wa sigara husababisha kwenye mwili wa binadamu. Haishauriwi kwa akina mama wanaonyonyesha kutumia dawa hizi pamoja na kwamba hakuna madhara yanayojulikana mpaka sasa.

Teeth%20Whitening%201.jpg

Kuboresha weupe kwa kutumia chemikali

Kupiga meno viraka (Veneering)
Hii hufanyika kwa kuondoa sehemu ndogo ya juu ya jino kwenye enamel kama 0.5-1mm na baadaye kupandika dawa yenye rangi nyeupe kulingana na mgonjwa anavyotaka mwenyewe. Picha inayonesha meno yaliyobadlika rangi kutokana na magadi kabla na baada ya kupigwa viraka

Teething%20Whitening%202.jpg

Kabla ya kiraka. Na Baada ya kupigwa kiraka(veneer)
Kumbuka: kuna rangi zaidi ya 26 nyeupe ambazo miongoni mwake mgonjwa anaweza kuchagua anayoitaka.


Kuyafanya Meno Yenye Rangi kuwa Meupe (Teeth Whitening)
 
Wapi hapa Dar wanatoa huduma hiyo??twaihitaji saana vyakula vinasababisha meno kuchafuka na kuwa njano kabisa!!
 
Ushauri: Kumbuka matumizi ya Colgate na Whitedent pia siyo sahihi sana kwani zina flouride nyingi ambayo haitakiwi mwilini. Wapo watu wanaweka mswaki mdomoni na kuangalia kipande cha habari katika TV hadi kikiisha ndo anaendelea kusafisha meno. wapo pia watoto wanaopenda Colgate na wakati mwingine huwaambia kina mama wawaongezee kwani ni tamu na mama kutojua madhara humimina tu kwenye mswaki na kumwambia aende kusafisha meno. Fluoride tuipatayo kwenye maji inatosha kabisa ktk mwili na ikizidi huathiri pia IQ(Intelligence Quotient) ya mtoto. Kutokana na ubaya wa Fluoride iliyopo imeandikwa kuwa inatakiwa kutumia Colgate/Whitedent bila kumeza na isizidi dk 1. Watu hawazingatii hilo na wala hawafahamu. Mimi nashauri kama una uwezo wa kununua dawa isiyo na fluoride iitwayo Forever Bright toothgel ni bora ikawa ndo unaitumia nyumbani sbb haina fluoride, huacha meno yako yaking'aa na pia huondoa harufu mbaya mdomoni, kama fizi zina shida huondoa tatizo na pia vidonda mdomoni. Vilevile ukimeza haina madhara na ni dawa pia kama tumbo linasumbua. Inaweza kutumika kuondoa fungus pia. gharama yake ni chee sana kulinganisha na matumizi yake. Ni sh 13000/- tu. Tuwasiliane kwa healthwealthfirst@gmail.com pia 0713889162
 
Back
Top Bottom