Jogoo akiwika hufanya hivyo kwa manufaa ya kuku wenzake, lakini wapo viumbe hunufaika na tukio la uwikaji. Simba akiunguruma hufanya hivyo kwa manufaa yake yake lakini wapo viumbe hunufaika na muungurumo huo kwani nyati na pundamilia huchukua tahadhari.
Katika maisha ya siasa ujanja ni nyenzo muhimu kuliko akili ya siasa. Siasa za ushindani ni kufuatitilia matukio na sauti mbalimbali unazozisikia na kujaribu kuzipa maana katika malengo yako ya kisiasa. Fanyeni hivyo kwa kuwasikiliza wema na wabaya ili mufike salama katika mapambano ya siasa. Msimchinje jogoo kwa kuwanyima usingizi wako watu wanasikilizia sauti ya jogoo kuwika waanze safari, msimtupie mawe simba akiunguruma, wapo watu wanataka aungurume karibu ya mashamba yao kila wakati ili wanyama wengine wasije kuharibu mazao yao.
Sasa ndio wakati muafaka kwa CDM kusikiliza na kufanyia kazi kila walisikialo ili mjipange ipasavyo, jogoo watawika karibu na mnapolala, simba wataingia katika makundi yenu, pumba zitakuwa pamoja na mahindi, dhahabu na udogo vyote na viwe mali yenu lakini msivitumie bila kuvichambua na kwa wakati muafaka
ALUTA CONTINUA, SUCCESS IS EMINENT