Kuwa nje ya nchi wakati wa tatizo kubwa la umeme ni ishara kuwa bado hatuna kiongozi

Yaani hali huku ni mbaya,mbaya sijuhi ni wapi imewahi kutokea hivi hapa dunia,pasipokuwepo na vita Tsunami n.k umeme unakatika kiasi hiki,sahiv umeme unakatika kila baada ya masaa2 na kurudi baada ya masaa12 hamna cha wkend wala j2,kwa uzembe wa hivi alafu viongozi hawawajibiki ni ugonjwa mbaya kuliko kisukari...

kama inawezekana watanzania sote tutenge siku tufanye maandamano twende butiama tukaombe labda mizmu ya baba wa Taifa itatusikia na kutuvusha hapa tulipo,tukiri makosa ya kuwaweka wasanii ikulu pake na atusamehe tuweze kuanza upya
 
David Cameron aliahirisha safari yake ya kutembelea nchi za Africa baada ya kashfa huko Uingereza ya The World News na magazeti ya The Sun ya Ruppert. Hapa kwetu swala la nchi nzima kuwa giza ni baya kuliko hilo la Uingereza na mimi naliona ni baya kuliko ile vita na Iddi Amin wa Uganda. Hasara nchi hii inayopata sasa itatuchukua zaidi ya miaka mitano ku-recover. Na ni mwekezaji gani atataka kuwekeza katika nchi ambayo haina umeme? Nimechukia!
 
Sioni tija!

Sioni kwenye huu mjadala.
Sioni tija kujiuliza kama tuna kiongozi wakati yeye mwenyewe hajioni kama ni kiongozi wa nchi hii.
Sioni tija kumlaumu mtu asiyejua lipi litakiwalo kufanyika.
Sioni tija kwa wanaendelea na lawama zao.
Sioni tija kumpigia mbuzi gitaa.
Sioni tija kufikiria kutakuwa na badiliko lolote
Tija pekee .....mabadiliko ya uongozi wa nchi
Waungwana tushikamane kwa hilo na sio kufanya mambo yasiyo na tija
 
Kama vipi atafute mwekezaji wa jumla ampe nchi, kila cku nasema Watanzania mliopga kura bora hata mngemchagua DOVUTWA au PITA KUGA MZIRAYI, tujue moja kwamba sio wazoevu na pia hawapanda ndege sana.
 
Tunatatizo kubwa ndani ya awamu hizi mbili. Tatizo likianzia ikulu hata mawaziri wooote ni vululuvululu.
 
Wandugu,Kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?

Kwa tabia ya watanzania, rais anaweza akaishi ughaibuni kwa raha zake na akaendelea kuwa rais. Kikwete anawajua vema wananchi anaowaongoza na ndiyo maana hana wasiwasi na tabia yake ya kusafiri kila kukicha.
 
Rais George Bush (GB)wa USA alipotembelea Tz na kualikwa Ikulu kwa chakula cha jioni alishangaa sana kuona sehemu kubwa ya jiji la Dar ipo gizani. Ikabidi amwulize mwenyeji wake, Rais wa Tz Jakaya Kikwete (JK),

GB: Imekuwaje kuna giza hapa jijini?
JK: Ah kuna kaupungufu wa nishati kidogo, na hivyo nimelazimika kuwa na kamgao
GB: Teh teh teh teh. Yaani katika karne hii nchi inakuwa na mgao wa umeme (Alicheka sana hadi machozi yakamtoka)

Baada ya miezi miwili JK alikwea pipa na kutinga USA na mwenyeji wake akamwalika White House. Wakiwa kwenye bustani ya White House JK aliona kuna sehemu ina giza karibu na hapo walipokuwa wanabarizi. JK akaona ampata mwenyeji wake na hivyo akamwuliza GB: Kumbe na huku kuna mgao?. GB akataharuki sana wakati huo JK alikuwa akivunjika mbavu kwa kicheko. Ikamlazimu GB kuwatuma makachero wake kwenda kuangalia kuliokoni kwenye eneo lile lenye giza. Baada ya nusu saa makachero walirudi na kumweleza GB eneo lile lenye giza ni UBALOZI WA TANZANIA
 
Tanzania tuna tatizo na tatizo lenyewe ni uongozi. Kiongozi wetu mkuu hana priorities kwani haoni hata mwenzie David Cameroon amerudi nyumbani baada ya kashfa ndogo tu. Mkuu wetu anaona ni heri matatizo yatokee asisikie. Sasa yuko bondeni anachekacheka huko sisi huku tunaumia! Huyu mtu atakuja kutukimbia siku moja maana anachojali ni masurufu ya safari zake tu zisizokuwa na faida yoyote kwa nchi yetu. Tuliwaambia kabla kuwa huyu mswahili hana analoweza kabla hamjamchagua 'kwa kishindo' sasa mnalalamika. Na bado! Mwenzenu anatafuta makimbilio mambo yakimzidia!
Obama hana Muda wa kukutana na Mtu kama Kikwete, Mtu aliyeshindwa kutatua matatizo ya Umeme nchi kwake ataweza kuzungumzia mambo makubwa?
 
Wandugu,Kwa mtazamo wangu, umeme ni kila kitu kwa maisha ya kisasa. Bila umeme nchi inayumba kiuchumi na katika nyanja zote za maisha ya mwananchi. Kinachonisikitisha ni kuwa katikati ya janga hili la nchi kuwa gizani kutokana na upungufu wa umeme, mkuu wetu wa nchi yupo busy na safari za nje. Mbaya zaidi safari zenyewe ni za kustarehe tu. Nimetafakari sana hali hii na kuhitimisha kuwa nchi yetu bado haijapata kiongozi. Sijui mnasemaje wadau?

Nampenda JK... lakini kwa hili.. una point ya msingi.. nani asiyeumizwa na giza?
 
Kwa tabia ya watanzania, rais anaweza akaishi ughaibuni kwa raha zake na akaendelea kuwa rais. Kikwete anawajua vema wananchi anaowaongoza na ndiyo maana hana wasiwasi na tabia yake ya kusafiri kila kukicha.

washenzi na wapuuzi ni askali wetu.....wakati wa uchaguzi shimbo alitishia jeshi kuingilia kati sasa waliyemtaka ndo huyo jk....nchi giza
 
Makosa tumeshayafanya kwanza kuruhusu demokrasia ndani ya vyama kupitisha watu wenye uwezo tata kushika uongozi wa nchi

Kosa la pili ni kukosa la kumfanya raisi ambaye tunaona hakidhi majukumu yake


Suluhisho 1. Kuweka utaratibu wa kikatiba ndani ya vyama vya siasa kuhakikisha watu wenye uwezo uliotukuka ndio wanapewa madaraka
makubwa kama uraisi

2.Kuwa na utaratibu wa kisheria ndani na nje ya bunge kuendesha kura ya kutokuwa na imani na raisi(ktk katiba mpya)
pindi itakapolazimika
 
suala la umeme halijaanza leoa kwahiyo sio dharura. Pia Raisi ana wasaidizi sio anafanya kilakitu yeye. Kukaa kwake nchini hakutomaliza mgao wa umeme
 
Back
Top Bottom