Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 663
Hata ukiwa naye kwenye mahusiano we sio namba moja kwake.
Mwanamke ambaye bado anatafuta mwanaume.
Mwanamke wa hivyo atakuumiza kichwa.
Atakua na wewe kwa maslahi fulani tu wala si upendo. Atakutumia tu. Akishapata anachokitaka atakuacha, unabaki na maumivu.
Utamjuaje? Dalili kubwa ni hizi.
Hana mipaka na wanaume.
Anaruhusu wanaume kuwa naye kirahisi.
Anaruhusu wanaume wengine wamshike/ wachombezane ovyo.
Licha ya kuwa na mahusiano na wewe, lakini haoni ubaya kujiachia kwa wanaume wengine.
Utaona anatoka na wanaume wengine ili ajisikie raha/ ili ajione kuwa wanaume wengine pia wanamuhitaji. Na kama analewa nao ndo vibaya zaidi.
Mwanamke wako kuombwa namba sio jambo baya.
Ila kinachofuata baada ya kuombwa ndo tatizo linapoanza.
Utaona anatumia muda mwingi kwa wanaume wengine kuliko wewe.
Ukiona hivyo, anza kuchukua tahadhari. Muulize nini shida, au malengo yake yakoje, au kama umemkosea ujue mapema.
Kuliko kujiweka kwa wanaume wengine.
.
Mawasiliano ni magumu.
Inapelekea kutoelewana hata kwa mambo madogo.
Atakwepa mazungumzo yanayohusu mahusiano.
Hatotaka muongelee mambo mazito.
Kiujumla hatokua tayari kujifungua kwako. Na kuongea mambo ya msingi na wewe. Mambo yanayohusu hisia zenu pamoja.
Ukiona hivyo ujue anajiona yupo singo. Na hakutaki kimahusiano.
Pia, utaona kitu kidogo tu anakasirika, ananuna au anaanza kuropoka.
Muda mwingine anaweza kukuambia kabisa kuwa ‘we haumbabaishi na anapendwa na wanaume wengine uko’. Au chochote chenye maana hiyo.
.
Atajitangaza.
Anaendelea kujiweka sokoni atongozwe.
Kujitangaza kwa mwanamke ni kwenye urembo wake.
Atajiweka mrembo kwingine zaidi ya akiwa na wewe.
Atajipendekeza kwa wengine zaidi ya kwako.
Pia atajiachia kwenye mitandao zaidi ya akiwa na wewe. Ujue we sio namba moja kwake. Bado anataka mwanaume mwingine zaidi yako.
Safari za kutoka zinakua nyingi. Ili akutane na watu wengine. Na wewe hautapata muda naye.
Hana muda na wewe.
Mkipanga mtoke, anakua na visingizio vingi.
Mkiwa pamoja haweki nguvu zake kwako, ana mambo yake.
Ukitoka naye hana muda nawe, anapepesa macho kwingine muda wote.
Au yupo kwenye simu yake muda mwingi. Ujue kabisa kwake anaona hakuna haja ya kuwekeza nguvu kwako.
Mnaweza mkafanya na mapenzi na akakuacha hewani. Mkafanya na akaondoka muda huohuo. Ujue hajioni kwenye mahusiano nawe.
Ukiona hayo mwambie tu “unataka/ unasema unataka kuwa na mimi lakini matendo yako ni kama vile upo singo na unajitangaza kwa wanaume wengine, siwezi kuwa na mtu kama wewe kwenye mahusiano, heri nikuache ukajiachie uko”. Na kama atataka kujirudi, ajirudi kwa vitendo si maneno.
Muda mwingine ukiona hizo dalili na ulikua naye vizuri kimahusiano, ujue kuna sehemu mlipishana. Hivyo anatafuta mbadala wako mapema. Hapo umuulize tu mlipokosana na uanze kufanya kama ulivyofanya zamani mpaka akakupenda, au ujue mapema na uachane naye.
Jiepushe moyo wako usizame kwa mwanamke wa hivyo. Na hata ukiwa naye cheza kama anavyocheza yeye.