Kuvalia mara moja moja Nguo ya ndani ya Mpenzi wako husaidia kuongeza Kismati maishani mwako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,656
109,056
Mganga mmoja maarufu anayetokea Mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa ( jina lake linahifadhiwa ) ameibuka na kusema kuwa hakuna Kismati / Bahati ambayo Mwanaume anaweza kuipata kama angalau akijiwekea utaratibu wa kila wiki angalau Kuvaa Chupi / Nguo ya ndani ya Mpenzi wake na kwenda nayo katika Shughuli zake.

Mganga huyo alienda mbele zaidi na kusema kwamba amekuwa akiwapa mbinu hii Wanaume wengi na imeweza sana kuwasaidia huku wengi wakimshukuru kwa kusema kuwa hapo nyuma maisha yao yalikuwa ni magumu ila mara baada ya kuanza utaratibu wa angalau Kuvaa Chupi za Wapenzi wao maisha yamebadilika kwani kuna vismati / bahati fulani sasa zinawapata.

Ni imani yangu kubwa sana kwamba baada ya kuwaleteeni hii taarifa sasa wale wenzangu na Mimi tunaobeti Ligi Kuu ya Uingereza, tunaofanya Kazi katika Machimbo ya Migodi, tunaofanya Biashara mbalimbali, wenye wadaiwa wetu Sugu na wale wengine wote wenye mahitaji mbalimbali ya Kimaisha kuanzia sasa mtajitahidi angalau hata ndani ya siku tatu za wiki mtakuwa mnavaa Chupi / Nguo za ndani za Wapenzi wenu na kuchanja nazo mbuga katika mihangaiko yenu.

Siku zote Mjumbe hauwawi na Shikamoo Mganga!

Nawasilisha.
 
Yani nivae bikini au chupi kisa kismati!!!Hahahaahh

bora niwe hohehae tu.

Mkuu kwahiyo umeshajitoa mhanga Kufa masikini hivyo? Kwani ukiivaa kisirisiri kuna Mtu huko mjini au kitaani atakayejua kuwa umeivaa? Mimi nakushauri na nikuombe tu kwamba jaribu kuvaa mara moja moja hali yako hiyo ya Shida itaanza kubadilika taratibu na hatimaye kutusua Kimaisha.
 
Ramli chonganishi ,chochezi kwa wchochewaji!

Any way, nyota ya ushoga inaanza vivyo hivyo. Mtapata mnachokitafuta.
 
Akili za watanzania zimejikita kwa waganga tu, shida nini?

Unajifanya Kuwachukia Waganga wakati mgongoni mwako, Kifuani, tumboni, matakoni / makalioni, ulimini na hadi katika Ugoko wako kumejaa tu chale za Uganga halafu kwakuwa upo hapa unajifanya Kuzuga na kuwadhihaki. Ninavyojua katika Watanzania Milioni 50 ambao hawana hizi Chale cha Waganga labda ni hawa Watoto tu waliozaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali zetu mbalimbali nchini.

Tuache Unafiki Waafrika na hasa Watanzania tunajuana wenyewe Kimila, Kindumba na Kiuganga.
 
Mkuu kwahiyo umeshajitoa mhanga Kufa masikini hivyo? Kwani ukiivaa kisirisiri kuna Mtu huko mjini au kitaani atakayejua kuwa umeivaa? Mimi nakushauri na nikuombe tu kwamba jaribu kuvaa mara moja moja hali yako hiyo ya Shida itaanza kubadilika taratibu na hatimaye kutusua Kimaisha.
hahahaha mkuu japo kisirisiri ila nitakuwa Najistukia yanataka moyo sana
 
Unajifanya Kuwachukia Waganga wakati mgongoni mwako, Kifuani, tumboni, matakoni / makalioni, ulimini na hadi katika Ugoko wako kumejaa tu chale za Uganga halafu kwakuwa upo hapa unajifanya Kuzuga na kuwadhihaki. Ninavyojua katika Watanzania Milioni 50 ambao hawana hizi Chale cha Waganga labda ni hawa Watoto tu waliozaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali zetu mbalimbali nchini.

Tuache Unafiki Waafrika na hasa Watanzania tunajuana wenyewe Kimila, Kindumba na Kiuganga.
wewe umechanjwa chale?
 
Zitaanza kesi ndani ya nyumba mara oooho chupi yangu siioni kumbe baba fulani kavaa

Kama ukiivaa na ikawa inaleta mrejesho chanya wa kimaisha Mpenzi wako naamini hatokuwa anakulaumu ila tatizo uwe unafululiza kuzivaa halafu maisha bado ni yale yale tena ndiyo magumu yenye mrejesho hasi hapo nadhani ndiyo utamkoma huyo Mpenzi wako.
 
Watu wakiiona watajua unabanduliwa.....................mi hiyo kitu siwezi hata kwa dawa...siyo kismati ni gundu
 
Kama ukiivaa na ikawa inaleta mrejesho chanya wa kimaisha Mpenzi wako naamini hatokuwa anakulaumu ila tatizo uwe unafululiza kuzivaa halafu maisha bado ni yale yale tena ndiyo magumu yenye mrejesho hasi hapo nadhani ndiyo utamkoma huyo Mpenzi wako.
Anaweza akawa anafurahi kwa sababu anajua ukivaa chupi yake huwezi kwenda kuchepuka
 
Back
Top Bottom