Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Kuuza lango la uchumi wa nchi au kutafuta wanahisa ni usariti mkubwa katika kuvunja katiba ya nchi: Bandari ni mali za watanzania wote hatuna wanahisa (shareholders) na hatuhitaji wanahisa.
Waraka wa wazi kwa waheshimiwa wabunge
Nakala kwa waheshimiwa viongozi wa dini
Nakala kwa taasisi ya Mwalimu Nyerere chini ya Mzee Joseph Butiku
Nakala kwa wasomi wote nchini
Nakala kwa umma wa Watanzania
Nakala kwa wapenda amani Duniani kote
Jumuiya ya Wanazuoni Nchini ambao tumekaa pamoja kutoka vyuo vikuu mbalimbali kutimiza wajibu wetu kama katiba ya Nchi inavyotaka pamoja na ya Chama Tawala iliyoridhi misingi ya TANU kwamba nitajielimisha kwa uwezo wangu wote kwa manufaa ya nchi yangu na Elimu yangu ni kwa manufaa ya Taifa.
Wanazuoni tunaanza kwa kutumia busara na kujenga hoja mahususi kupinga nchi yetu kuuzwa kienyeji kwa kisingizio cha mashirikiano ya Nchi yetu na Nchi za Falme ya Kiarabu. Hoja zetu ni kama ifuatavyo;
Kwanza; Bandari zetu zote ni mali za Watanzania zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuna ubia na mtu yeyote wala Taifa lolote.
Baada ya kusoma kwa kina mkataba wa kubadilisha uendeshaji wa Bandari zetu na kufuatilia hoja mbalimbali za wanaunga mkono na wanaopinga.
Wanazuoni tunapenda kutoa tafsiri sahihi ya kinachoitwa mkataba kuwa ni kuuza Nchi kwa bei rahisi sana na kuingiza mwanahisa mpya kwenye umiliki wa Bandari zetu ambao hutakuwa umiliki wa milele na ukiliziwa na Bunge utalindwa na sheria za Kimataifa huwezi kuuvunja na ukifanya hivyo Nchi itaingia kwenye vita maana kila upande wa umiliki wa Bandari utatumia jeshi kulinda haki zake za kiuchumi (economic interests).
Hoja yetu ya msingi hapa kuwa tutapoteza umiliki ambao tulipewa na Mungu “Sovereign ownership of the ports”. Wanazuoni tunasikitika kwani serikali zilizotangulia zote zimewekeza sana kwenye maboresho ya Bandari zetu kwa kiwango cha juu mno kwa viwango vya Afrika.
Ni ujinga (ignorance) wa kiwango cha juu sana kujilinganisha na Nchi za Falme za Kiarabu (Emirates au Dubai) ambazo zinamilikiwa na falme au koo. Ni rahisi sana Mabeberu wa Kimarekani kujificha kwenye kivuli cha Falme za Kiarabu au Umoja wa Ulaya ambao wanao mkataba mbovu wa EPA uliokataliwa na Afrika.
Kumbuka Umoja wa Ulaya ulitumia pesa nyingi na muda wa miaka mingi kutaka moja ya masharti yao ya EPA ni kutumia Bandari zetu bila malipo yoyote as Free ports for European goods/products.
Ukizingatia uchumi wa Marekani na Umoja wa Ulaya upo kwenye kipindi kigumu sana kuliko wakati wowote.
Marekani na Umoja wa Ulaya wanaongezeko kubwa la umasikini, hukosefu wa Ajira na wamezidiwa na China katika uzalishaji viwandani (Manufacturing industries).
Hivyo basi, sehemu pekee ya wao kupona na kushindana na China ni kupora utajiri wa Tanzania (Afrika) na kuendeleza unyonyaji ili waweze kuwatunza wazungu wenzao kwa kuwapa sera kinga (social Protection policies).
Hii inawezekana tu kwa kuendelea kupora rasimali za Afrika na kupora uchumi wa Nchi zetu. Wanajua wakichukua Bandari zote za Tanzania watakuwa wanamiliki uchumi wa Nchi Karibia kumi zinazotegemea Bandari zetu kwa sababu Nchi yetu ipo kijiographia eneo la kimkakati sana na ndiyo moyo wa Nchi zote zinazotuzunguka.
Ukiharibu uchumi wa Tanzania na Amani ya Tanzania umeharibu uchumi wa majirani zetu, Rejea Wosia wa Baba Taifa Mwalimu Nyerere kwenye hotuba aliyotoa SADC mwaka 1984 akiwa sehemu ya kuaga kama Mkuu wa Nchi.
Hivyo, Wanazuoni tunawaomba Waheshimiwa Wabunge wetu wakatae kabisa siyo tu kubadili vipengele vya mkataba waachane kabisa kucheza na Taifa letu maana historia itawahukumu vibaya sana. Wajifunze Libya jinsi Mabeberu walivyowatumia wanasiasa na kuharibu Taifa lile.
Ukiingiza Mabeberu wa kimarekani na Ulaya kwenye umiliki wa Nchi kama wanahisa wa Bandari zetu kwa mgongo wa Madalali wa Vi-nchi vya Falme za Kiarabu vinavyomilikiwa na kuendeshwa na familia za Kifalme ujue umeuza Nchi kabisa na Rushwa waliokupa utajuta maana watakutupa mbali na kutafuta serikali ya kulinda masilahi yao.
Hiki ndicho kitakuwa kifo cha Chama Cha Mapinduzi na laana ya Waasisi na Watangulizi itatutafuna na kuwatafuna wabunge wote pamoja na spika wao. Mungu tuepushe laana hii.
Hoja ya pili ya Wanazuoni ni kwamba Uchumi wa Tanzania tangia awamu zilizopita na kuchagizwa na Awamu ya Tano imeweka Miundo Mbinu mikubwa sana ya Matrilioni ya Shilingi.
Tumejenga reli ya Kisasa na tunamiliki wenyewe hatuna ubia, tumejenga vyanzo vya umeme ili kuweza kuendesha Treini za umeme.
Tumewekeza sana kuboresha Bandari zetu kwa uwekezaji wa matrilioni ya shilingi na hatuna ubia.
Tunahitaji kuendesha wenyewe Bandari na kutumia treini ya umeme kufikisha mizigo ndani ya masaa 20 kwenye Nchi zinazotuzunguka na tutaweza kupata pesa nyingi za kulipa madeni ya miundo mbinu.
Ukiweka mbia yaani shareholder kwenye Bandari zetu hutaweza kucontrol mapato na matumizi ili uweze kulipa deni.
Hawa Madalali mabeberu wa Vi-nchi vya Falme za Kiarabu watapewa mgao wao yaani dividends na Tanzania itapewa dividends na tutakuwa wajinga kusaini mikataba kabla iliyosainiwa na Kar Peter karne za 14 na Chifu wa Msovero.
Mikataba siyo tu ya kitapeli bali ni ya kinyonyaji maana thamani ya Bandari ni kubwa mno ni Sovereign wealth na hawa madalali wa Mabeberu watatumia bandari zetu kukopa Duniani hawaji na chochote bali pesa za kuwahonga viongozi wetu pamoja na kuwapa ahadi hewa za umiliki sehemu ya shares.
Watawatupa nje kama Mobutu wa Congo zamani Zaire. Imperialists have permanent interests not permanent friends. Baada ya miaka ishirini Nchi itakuwa imeuzwa kabisa kwa Mabeberu ambao watajitanua sana na tutajiingiza kwenye mgongoro wa kuchumi wa Kimtaifa (Geo political conflicts among imperialists powers).
Tujifunze kwa Ufaransa na Nchi walizozitawala wanaendelea kuzinyonya kichumi.
Hivyo basi tunawaomba Waheshimiwa Wabunge tusikubali kupuuza ushauri huu wa wasomi na kukubali mawazo ya kijinga ya wanaojiita darasa la saba ambao hawana uelewa wa uchumi wa Dunia na vita ya kiuchumi Duniani.
Hoja ya tatu ya Wanazuoni kwa Waheshimiwa Wabunge ni kuomba kabisa kukataa kabisa kutumika kuuza Nchi. Tunapinga hoja ya kusema kuwa wenzetu wana mitaji na technolojia hivyo tutaboresha uendeshaji siyo kweli.
Hatuwezi kujilinganisha na Vi-nchi vinavyomilikiwa na familia za Kifalme ambavyo ni madalali ya mabeberu. Tutaboresha kwa viwango vyetu na tunaweza kuajili mtu yeyote kutoka Dunia kuboresha uendeshaji.
Tunaweza kuajili Mzungu, au Mhindi, au Mwarabu au Mkorea au MwaAfrika yoyote na tunaweza kununua technolojia popote duniani na kuweka mifumo ya Komputer ili kuondoa kero na Rushwa Bandari.
Ni Ujinga wa kiwango cha Uprofesa wau juu zaidi kwa kuuza Nchi kwa kumpa mtu ubia ili aweze kuendesha Bandari zetu kwa niaba. Tutakuwa tumewasaliti watanzania.
Waheshimiwa wabunge mkataba huo mpe GSM au Bharesa au Jumuiya ya Wafanya biashara Nchi watafanya maboresho na utajiri utabaki hapa hapa na usalama wa Taifa utabaki palepale.
Huhitaji kuwa Profesa wa Uchumi kuona kuwa mkataba tajwa ni utapeli wa kimataifa na kuuza Nchi kienyeji ni mjinga tu anaweza kukubali.
Hoja ya Nne kutoka kwa Wanazuoni, tunakataa Madalali wa Kiarabu wanaotumiwa na Mabeberu na wanaomiliki Vinchi vyao kupitia familia za kifalme zenye idadi ya watu ndogo na wote wananufaika na utajiri wa Nchi zao, mfano Dubai watu milioni mbili tu na wote wanatunzwa na serikali ya kifalme.
Hivyo, Social anthropology ya WaAfrika na WaTanzania ni tofauti na hao WaArabu kabisa kwa idadi ya watu na mambo mengine mengi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kihistoria.
Bunge lenye maprofesa wengi wazuri wakiwepo Prof. Kabudi, Prof. Kitila, Prof. Mkenda, Prof. Ndalichako na wengine. Halafu Bunge lenye Madaktari wa kusomea (PhD) nao ni wengi pia. Wapo Madaktari wa Binadamu (MD) nao wengi.
Wapo wasomi wa aina mbali mbali wakiwemo wachumi . Hivyo sisi Wanazuoni tunaomba mkataba wa kukodisha Bandari husipitishwe kwani ni kuuza Nchi. Hawa wasomi wakikaa kimya historia itawaukumu huko mbele ya safari.
MAPENDEKEZO
Wanazuoni tunatoa mapendekezo yafuatayo kwa Waheshimiwa Wabunge pamoja na viongozi wote ambao wamepewa nakala ya wakara huu kutoka kwa wasomi wa Taifa.
Kwanza; tunaomba kabisa Bunge lisitishe kabisa mkataba huu siyo kuboresha bali kusitisha mara moja na ktunga sheria ya kutoweka mbia yoyote kwenye Bandari zetu zote, iwe Bagamoyo au iwe yoyote. Liwepo katazo la kibunge.
Pili, tunaomba wabunge na spika wamaqshauri vizuri Mh. Rais kwa upole na uzalendo wa hali ya juu. Inawezekana washauri na wachumi wa Rais hawajaliona jambo hili kwa bahati mbaya hivyo ushauri wetu utawaamusha uzingizini.
Tatu tunashauri Treini ya Umeme ambayo Mh. JPM aliacha imekamilika kipande cha DSM na kipande chas Dodoma ilikuwa imefikia asilimia 80%.
Tunaomba mshauri Rais azindue Treini hiyo na kwenye bajeti ya mwaka huu tuwekeze kujenga reli mpaka Bandari.
Tujenge Bandari kavu kubwa Dodoma kwa kutumia SUMA JKT kwa muda mfupi na gharama ndogo ili treini ianze kubeba mizigo na kuongeza ufanisi wa Bandari bila kuweka madalali waq Mabeberu wanaokuja kwa mgogo wa Vinchi vya Falme za Kiarabu wanavyomilikiwa na Familia.
Tanzania ni Nchi yenye hadhi kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimtaifa. Tanzania ni Nchi na Taifa ambalo halimilikiwi na Familia ni Nchi solid kabisa yenye kuheshimika Duiniani tusipoteza mwerekeo tuungane na tujenge Nchi yetu.
Nne Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wetu waweze kutafuta busara za wazee wa Taifa, Mzee Joseph Butiku, Mzee Warioba, Mzee Mangula, Wastaafu wa Jeshi, Wastaafu wa Usalama wa Taifa, Marais Wastaafu, Maprofesa Wastaafu , Wasomi wabobezi kama vile Profesa Shivji na wengine wengi.
Wabunge aandaa semina huko Dodoma na Waite hawa Watanzania Wazalendo wawepe Busara zao ili mkifia maamuzi mtaweza kuliokoa Taifa.
Tano Wanazuoni tunashauri Waheshimiwa Wabunge wamuombe Mh. Rais amsimamishe kazi waziri Mbarawa kupisha uchunguzi maana wizara yake ndiyo inataka kuleta majanga ya Taifa.
Tunatanguliza Shukrani
Wenu Katika Ujenzi wa Taifa
Wanazuoni
Habari zaidi, soma: