Asante Mungu wengi wameanza kuona. Huitaji kwenda shule au kuwa Malaika kuona how potential Prof. Muhongo is. Huitaji kujifunza vitu vingi saaana ili ujue Tanzania kama nchi tumekuwa tukikosa nini kwa mda wote huu baada ya kumsikiliza Prof Muhongo.
Nilimpigia simu mwenzangu mmoja baada ya kuangalia utangazaji nia wake nikamwambia naomba umuangalie prof .
kusema kweli ni kama Mungu ametushushia hii zawadi na kutuambia tuone tulikuwa tumekosa nini kwa miaka yote na sasa ndo ameamua kutupa.
Nazidi kuomba tena watu watu wa television na redio mrudie tena kuonyesha hii event ya prof Muhongo akitangaza nia. Naomba tena hata mnao andaa iyo midahalo please fanyeni juu chini kwenyew hii midahalo prof Muhongo awepo ili watanzania waweze kuiona hii hazina na fanyeni juu chini iyo midahalo ionyeshwe na television nyingi sana hapa nchini na irushwe na redio nyingi sana ili watanzania wapate kuiona hii hazina.
Mungu ambariki na kumlinda prof Muhongo.
Jitafutie mda tu umsikilize mkuu with your conscious mind alafu utakuja kutuambia hapa. Mungu akupe hekima na busara wakati unaangalia hiyo speech yake alafu utakuja kusema kama tumetumwa?Mmetumwa au
Naona kwa watia nia ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kupitia CCM Prof. Sospeter Muhongo amepata alama za juu , je wana-JamiiForums
Kwa hiyo nani kakuambia tunahitaji cv, ndefu tunahitaji utendaji na sio cv na vyeti, wenye vyeti na cv wako wengi, hatutaki watu wanaojisifu tz ilipofika inahitaji rais anaefanana na dictator awakimbize watanzania tufike kwenye malengo, sio kujisifu umesoma ges, yeye anaona ges tu, kuna kilimo, viwanda hambavyo havipo, tusubiri watangaza nia wote na waupinzani ndo tutajua rais ni nani bhana...
Asante sana kwa kuiweka mkuu.Video nzima ya 060615 MARUDIO YA HOTUBA YA PROF. SOSPETER MUHONGO ALIYOITOWA MUSOMA WAKATI AKITANGAZA NIA - URAIS
Source: Gonga link hii: Channel ten: https://www.youtube.com/watch?v=PMjRV4E0SAg
Kamanda safi safi kwa hii hoja yako,wengine badala ya kufanya utafiti wanafitinishwa na TV na Magazeti kuwa jamaa hafai,Jamaa anajiamini,anaongea kile kinachowezekana,na anaona mbele,kuna watu wamezoea kudandia na ushabiki,hawawezi kueleza ubaya wa huyu jamaa zaidi ya kusikia kwenye magazeti na TV.Muhongo anaongoza kwa kua na uhakika na mambo yanayotekelezeka huyu jamaa ndio atatuvusha hawa wengine chai tu
chukua tena "like" mkuu umemaliza kila kitu,huyu ni mzee wa facts bila kupepesa macho..nimetafakari kwa kina, nimemfanyia tathmini iliyotukuka na kumlinganisha na watangaza nia wenzake wote 22 mpaka leo ukiachia mbali wale wa kesho sasa ni rasmi na nasadiki kusema kuwa iwe isiwe kwa mujibu wa mathematician gentamycine 100% rais mpya ajaye wa tanzania ni profesa sospeter muhongo.
sifa zake ni nyingi na zilizotukuka na sijaona anayefanana nae kiakili na kimaono kati ya wote waliokwisha na watakaomalizia kutangaza nia. profesa muhongo ndiyo jibu la watanzania na nina imani na wana ccm wote kuwa mtampitisha huyu genius wa kitanzania ili atutawale.
profesa muhongo popote ulipo tafadhali hebu tutafutane ili niweze kukupa mikakati mingine ya kuelekea ikulu mwezi october 2015 na sasa natangaza rasmi kukuunga mkono wewe na nipo tayari kukupigia chapuo kokote kule nchini tanzania ili uweze kuwa rais wetu na nina imani kabisa kuwa utapita.
Ninachokuomba tu ni kwamba ukishafanikiwa kuwa rais usisahau kuwapa vyeo watu hawa ili kudhoofisha makundi yao. Kwa mfano ningependekeza ukiwa rais wetu wizara ya mambo ya nchi za nje au ubalozi wa tanzania nchini ujerumani mpe mzee lowassa ili imrahisishie kwenda ulaya au kupata tiba kama pakiwa na hilo hitaji lakini wizara ya afrika mashariki mteue mzee benard membe au kama vipi utampa ubalozi wa tanzania nchini libya au burundi lakini nakuomba makamu wako wa rais ( running mate ) awe jaji augustino ramadhan na iwe isiwe nakuomba waziri mkuu wako mpe mzee john pombe magufuli na hao wagombea wengine waliotangaza nia utaamua tu kuwatupa huku na kule ili wasinyong'onyee na kukuletea jicho la husuda.
Namalizia tena kwa kusema tena nikiwa na uhakika wa maono yangu yaliyotukuka kwamba ewe mheshimiwa profesa sospeter muhongo ndiyo utakuwa rais wetu na zingatia hayo yote niliyokuelekeza hapo juu na kwa mengi zaidi wewe mwenyewe au kupitia kamati yako hakikisha au hakikisheni mnanitafuta ili niwape strategies zingine zilizotukuka pamoja na mambo ya kiitifaki ambayo siwezi kuyaanika yote hapa ila ukini pm mwenyewe nitawasiliana na wewe tuweze kukutana na kufanya kazi ila ikulu kaa ukijua kuwa ni yako.
Najua wengine mtanuna na mtanuna sana na mno mwaka huu ila profesa muhongo ndiyo next prezidaa wetu na tambueni mathematician gentamycine akipenda kitu basi hata mwenyezi mungu na malaika wake wamekikubali na wamekithibitisha.
Nawatakieni maandalizi mema watanzania wenzangu wote ya kumpokea rais mpya na ajaye tanzania mheshimiwa profesa sospeter muhongo na maneno yangu haya ya leo nayasadiki kwenu.
Akhsanteni.