Kutoka Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Musoma: Prof. Muhongo atangaza nia ya Kugombea Urais

Alishindwa kuzuia Escrow ndiye atakayelinda rasilimali zetu? Muongo kama jina lake lilivyo
 
Tatizo wa Tanzania wanependa unafiki wa ki Communist, yani kikumunisti ni kitu chako lakini unakiogopa na kujifanya sio chako. Ukiongea ukweli unakuwa arrested kama hawawezi basi unajigamba. Hiyo inferiority complex ya watanzania, mtu kuongelea CV yake eti unamajigambo. Nchi zingine ukiomba kazi na ukashindwa kuisifia CV yako, kazi hupati ng'oo, utapiga teke barabarani na CV yako kwapani ukiogopa kujisifia mpaka ukome.
 
Sidhani kama nchi hii sasa tunashida na wasomi? Waliopo kwenye system full ma prof,ma Dr watu wamejaa master's na diploma, lakini ni majizi kufa, mafisadi yasiyofaa,
Shida yetu tunahitaji mzalendo mwenye kuweza kulinda rasilimali zetu na Kugawa keki ya Taifa kwa usawa,
Tunahitaji rais ambae atakuja kutuunganisha kama Taifa ambalo lina mipasuko iliyojaa, sijaona mpaka sasa katika watia nia wote bado naendelea kuchuja, kura yangu bado iko mfukoni
 
Wadau,
Mwenye hotuba ya Kutangaza nia ya Prof. Muhongo atuwekee. Tutashukuru tukipata video.
 
Muhongo nakukubali kwa C.V yako coz ww ndo msomi number one bongoland BUT uraisi tuachie ww gombea ubunge mzee, hizo ndo level zako.

Kudadake na wewe Kilaza hivi? Ndo.mnataka kutuletea.marais Mburula? Ubunge My foot. Ubunge mpe ding yako mchovu mchovu ...
 
Tukiweka ushabiki pembeni, Prof. Muhongo an IQ kubwa sana. Ila kwa kuwa siasa ya bongo kwa sasa imetawaliwa na ukanda (hasa ukaskazini) ndani na nje ya CCM,atasakamwa sana. Na hataungwa mkono,mengine mbwembwe tu.

Hiyo IQ umeipimaje? Je, unajua IQ inapimwaje? Ni nani amekuambia kuwa "IQ kubwa sana" ni kiashiria kuwa atakuwa Rais bora? Kwa nini asifanye utafiti na kufundisha Chuo Kikuu? Prof. Muhongo ni mwenyeji wa kusini? What I know is that Prof. Muhongo is an academic - a geologist to be specific. Huku kwingine anaganga njaa tu na kujidhalilisha kama maCCM wengine.
 
Tatizo wa Tanzania wanependa unafiki wa ki Communist, yani kikumunisti ni kitu chako lakini unakiogopa na kujifanya sio chako. Ukiongea ukweli unakuwa arrested kama hawawezi basi unajigamba. Hiyo inferiority complex ya watanzania, mtu kuongelea CV yake eti unamajigambo. Nchi zingine ukiomba kazi na ukashindwa kuisifia CV yako, kazi hupati ng'oo, utapiga teke barabarani na CV yako kwapani ukiogopa kujisifia mpaka ukome.

Mkapa umeongea point. Tatizo wana vyeti feki so ni ngumu kujigamba.. Mwenye magamba yake halali lazima ujigambe bwana ndio maana wanaitwa Wasomi... Wanajiamini na wanaweza ... Mburula ataanzia wap muda wote anawaza akikamatwa na cheti bandia itakuaje na division Five yake ... Hata kama mim najigamba maana naweza kuingia Popote...
 
KAULI MBIU: TUKUZE UCHUMI. TUONDOE UMASIKINI - Prof. Sospeter Muhongo


Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.



Kama ndiyo huyo Muhongo mnamfagilia na yeye pia anajifagilia eti amesoma mpaka mwisho basi ni kilaza na wa kuogopwa kama ukoma.
 
kauli mbiu: Tukuze uchumi. Tuondoe umasikini - prof. Sospeter muhongo

View attachment 256444

waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya escrow, profesa muhongo anatangaza nia moja kwa moja kutoka musoma.

Tujumuike pamoja.


- muhongo ameshapanda stejini anawasalimu wahudhuriaji.

==============

''niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika. Siko hapa kumlaumu mtu au kumshambulia mtu, kwa sababu ukimlaumu mtu umasikini bado uko palepale.

Nikisema historia yangu yote muda hautatosha. Kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taaluma nimefikia mwisho. Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.

Nimefanya utafiti kwa miaka 30, chama cha majiologia wa marekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu. Pia kwa waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.

Kwenye uasisi mwaka 1976, ccm inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya ccm tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.

Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini mwl alitueleza. Ni lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.

Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa linanyemelewa na uvivu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa kujiamini. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi.

Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro mauritania na chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.

Lazima tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni finland''.

- anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia ikiwemo india, brazil, china na kenya. Sipendi sana kujilinganisha na kenya kwa sababu sote ni maskini.

Anaendelea...

''dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dola bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule mihogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.

Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi.

Naombeni ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa lisiongezeke, mwenye dawa ya umaskini ndani ya ccm, chadema, nccr ni profesa muhongo tu. Elimu kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani darasa limerundikana ukafundisha.

Anaeweza ni mimi tu sababu wengine utafiti wanausoma kwenye magazeti tu.

Wana ccm mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu! Tutatumia rasilimali, madini yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu. Mimi ndio nimetengeneza ramani ya madini ya tanzania, africa na duniani nikiwa vice president. Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa uzalendo, ningeweza kuja na ramani na kuiuzia serikali.

Mimi mtu hanidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio dunia ya kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu mnichague. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.

Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye mikono ya uhakika kwa profesa muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko chuo kikuu cha dar es salaam na nimefanya maisha yangu yote.

Mapato ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu na bunge litakua linaidhinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti. Mtanzania yoyote asiwe na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya watanzania.

Mimi sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba sipendi wawekezaji wa ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe na umeme. Na umeme wa bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara, muda umefika tusijidharau, lazima tushinde.

Lazima watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe wanatumia umeme, tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua mbele professa muhongo ametimiza ahadi ya ccm, hata ilani mpya inayokuja mtekelezaji atakaetekeleza kwa uhakika ni profesa.

Ni lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana nazo na nyie wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa sababu hamjui haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu. Wakulima na wafugaji ni mwisho wa kuuana chini ya prof. Muhongo, tatizo sio ardhi, ni teknolojia.

Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu''.

rais ajae huyo hapa
 
Una hoja dhaifu sana, watu wavivu kama wewe usiyejihangaisha kusoma na kudadisi huwezi ona faida za muhongo katika nchi hii. Nyie leo ndo aliwasema kuwa kila kitu mnaingiza siasa, halafu umamfananisha boss wako na muhongo kweli??? Hahahaha ndio maana tunaendelea kuwa masikini. Badala ya kulalamika na wewe nenda shule bana.
Wewe mwenyewe ni dhaifu na hoja yako lazima iwe dhaifu.Hivi inakuaje mtu na akili zako unadanganyika kirahisi na Prof Muhongo,Miaka 50 ya uhuru wananchi hawana uhakika na mabomba ya maji ye anasema ataweka mabomba ya gesi kila nyumba.Anasema kastep down uwaziri ili watu waonje machungu,hivi huyi mtu ana akili kweli,hivyo hivyo basi hata akiwa rais hatakuwa na mipango endelevu mipango yake itakuwa ni ya miaka kumi tu.Kama hakuweka mipango endelevu kwenye nishati ataweza kwa nchi? Prof Muhongo abaki hukohuko kwenye miamba huko ndo ni best lkn sio huku kwenye Urais.Kwenye Urais simwiti Prof Namwita kilaza tu.Alipokuwa Waziri alisema hakuna mgao wa umeme,je ni kweli hakukuwa na mgao wa Umeme? Jiongeze ndugu acha uvivu kwa kufikiri
 
Kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taaluma nimefika mwisho.

Kama naweza kutunza kadi ya CCM toka mwaka 77 hadi sasa basi mimi ndio naweza kutunza raslimali zenu.

Africa ina nchi 54, mimi nimeenda 52

Nataka tule mihogo na viazi kwa hamu, sio kwa shida.

Mwenye dawa ya umaskini ndani ya CCM, CHADEMA au NCCR ni mimi Prof Muhongo tu.

Nimefanya utafiti kwa miaka 30.

Anayeweza ni mimi tu, maana wengine utafiti wanausoma kwenye magazeti.

WanaCCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu!

Mimi mtu hanidanganyi, unakuja tunajadiliana.

Ilibidi nitoke serikalini kidogo mpate machungu mnichague.

Tutajenga mabomba nchi nzima kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.

Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi.

Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta hela ndani na nje, ambacho sina ni ninyi kuniteua tu...

💪💪💪👏👏👏
 
Jamaa yuko vizuri sana.

Huyu Prof. ni bingwa wa kurodhesha nchi alizotembelea na professional experience yake. Kuwa "mwanasayansi wa dunia"(whatever this mean) si sifa ya kuwa Rais wa Tanzania au nchi yeyote ile for that matter. If anything, Rais mzuri ni mwanasiasa mzuri (na si mwanasayansi mzuri).

Kutembelea nchi 51 kati ya 54 za Africa haina maana kuwa wewe ni mwaminifu. Wako wezi wengi tu wanazunguka nchi mbalimbali duniani. Wauza unga wanazunguka dunia nzima. Je, ina maana hawa maharamia ni waaminifu?

Zaidi ya kujisifia, uwezo wa huyu Prof. kujenga hoja ni mdogo sana. Mwigulu Nchemba anamzidi kwa mbali sana. Kueleza qualifications zako arrogantly bila ku-demonstrate ni namna gani utatoa leadership kutatua matatizo yanayoikabili nchi hii na wananchi wake ni kupoteza muda. Tunatafuta Rais wa nchi. Hatutafuti geologist aliyebobea na anayejua ramani ya madini na gesi ya nchi nyingi duniani. Rais wa nchi atawatumia geologists waliopo kupata ushauri wa kitaalamu atakapohitaji. Si lazima Rais wa Tanzania awe geologist.

Kama unafahamiana naye mpatie ushauri. Anapofanya siasa ajue audience yake si professional geologists. Kila mara anajisahau anafikiri anagombania kuongoza chama cha geologists. It takes a lot more to lead a country than being an accomplished geologist.
 
this guy is a really deal sema tu sioni akipata nafasi ila gee is miles better than all other candidates
 
Hiyo IQ umeipimaje? Je, unajua IQ inapimwaje? Ni nani amekuambia kuwa "IQ kubwa sana" ni kiashiria kuwa atakuwa Rais bora? Kwa nini asifanye utafiti na kufundisha Chuo Kikuu? Prof. Muhongo ni mwenyeji wa kusini? What I know is that Prof. Muhongo is an academic - a geologist to be specific. Huku kwingine anaganga njaa tu na kujidhalilisha kama maCCM wengine.

Unataka afanye mara ngap huo utafit
 
Back
Top Bottom