Kutoka Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Musoma: Prof. Muhongo atangaza nia ya Kugombea Urais

Huyu Prof ndio raisi atakayetutoa hapa kwa kweli, tatizo ni sisi watanzania na uvivu wetu na tusivyopenda kuambiwa ukweli sijui ka ccm watampitisha ila kwa quality hadi sasa kawaacha mbali sana ccm wengine
 
Nimekuambia mimi siyo mtoto mwenzako! Hapa ni JF tunazunguma mambo muhimu siyo FB! Huyo unayempigania kwanza simfahamu, pili hana faida kwangu kwani hanipi mlo wangu, ninajitegemea na familia yangu!

Lo hahahahhaha eti humfahamu ungehangaika kuingia humu na kukomenti??? Unamjua sana na wewe ni mmoja wa wakwepa kodi ambao mnawayawaya na kugwayagwaya. Ulijuaje fb yanazungumzwa mambo ya kitoto kama hushindi na watoto wenzio huko??? Tupishe bana!!
 
Muhongo nakukubali kwa C.V yako coz ww ndo msomi number one bongoland BUT uraisi tuachie ww gombea ubunge mzee, hizo ndo level zako.
 
CCM imetufikisha pabaya, haijawahi kutoa kiongozi aliyefukuzwa kwa rushwa, anaweza kusimama bila uoga kutangaza nia ya urais.
Matatizo anayoyataja,yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri, leo anadai anayajua kwa nini hakusaidia kupambana na rushwa, umaskini na maji?

Tatizo mhimili Judiciary umekamatwa na ikulu sasa inakuwaje!ndio maana hao watuhumiwa wa ufisadi wanatafuta urais kama kinga.
 
Kwani Albert Einstein alitangeneza ajira ngapi?
kwani Mie nimesema Albert alikuwa kilaza tena kwa mazingira yake? Je unajua kwanini nimesema Muhongo naye ni kilaza tu Ukicompare na Mbowe? Anaingiza madarasa yake kwenye siasa? Halafu anasema kasoma hadi mwisho wa kisomo ndo mnatumia kigezo hicho kuwa ni msomi usomi wake umekusaidia nini wewe?
 
hata udiwani huyu Profesa hafai. Mimi sijawahi kusikia duniani kote msomi anayejikweza! Kawaida ni jamii inamwona, inamkuza. Huyu eti mimi ni mtafiti, mimi ni mkweli! anatuaibisha sana. Huyu anapaswa atafutiwe Nchi yake, yeye na yule Bw Mdogo Mchemba, moja atakuwa Raisi mtafiti, na mwingine Waziri Mkuu Mchumi Daraja la Kwanza ambaye aliwahi kubeba zege na kukurupishwa kuchukua Masters na BOT ya nchi ya Tza

Heeeeee aisee umekula maharage ya wapi wewe?? Kwa nini asijisifie? Unataka asifiwe akifa? Hata mie ningekuwa nimetoboa kama.yeye ningeringa, MUNGU kampa akili mwache aringie bana, nyie mnaojificha na elimu zenu inaonekana mnatambua kuwa mmebebwabebwa tu. Mwache ajivune bana acha wivu
 
Mkuuuu umenivunjaje mbavu mie mwenyewe leo nimeonja kiazi kwa hamu

Profesa hataki watu washindie mihogo asubuhi mchana jioni. Hii itamsaidia hata yule aliyesema akiingia ikulu atakula mihogo tu walau abadilishe menyu hahahhahaha!!! Kisayansi zaidi. Majungu kwake mwiko
 
Usinidharau mkuu,hata mimi nina hoja!
sasa kwamfano kusema tulime michikichi ni kazi au yule mwingine alisema atakuza uchumi wa kisekta,haya anayoongea prof Muhongo,yote prof Jay wa mitulinga alishayasema.sioni kazi hapo

Yani wewe aisee utoto unakusumbua. Umeshasema ni profesa wa mitulinga hahahahha. Profesa muhongo ni mwanajiolojia si mwanamitulinga hahahahaa. Yani hata kutofautisha hapo umeshindwa.
 
kwani Mie nimesema Albert alikuwa kilaza tena kwa mazingira yake? Je unajua kwanini nimesema Muhongo naye ni kilaza tu Ukicompare na Mbowe? Anaingiza madarasa yake kwenye siasa? Halafu anasema kasoma hadi mwisho wa kisomo ndo mnatumia kigezo hicho kuwa ni msomi usomi wake umekusaidia nini wewe?

Una hoja dhaifu sana, watu wavivu kama wewe usiyejihangaisha kusoma na kudadisi huwezi ona faida za muhongo katika nchi hii. Nyie leo ndo aliwasema kuwa kila kitu mnaingiza siasa, halafu umamfananisha boss wako na muhongo kweli??? Hahahaha ndio maana tunaendelea kuwa masikini. Badala ya kulalamika na wewe nenda shule bana.
 
Watu km mhongo wanajua hata TADEA haiwezi ikuwapitisha kugombea uras ila lengo lake ni mambo mawili. Moja anatangaza kwa ajili ya ubunge ili akikosa aseme si mmeona nilitanganza na urais? Lakini pili anatafuta fisadi mwenzake kama Lowassa ili baadaye amteue kwenye madili yao ya pale TANESCO.

we kinabo acha kuongea sana,,, yule jamaa nakuapia hakiamungu ni mchapakazi sana politics aside.. mi binafsi ile no. naikubali sn na nawalaum sana watz maana we keep on getting rid of the people who can do the job.. historia itatuhukum siku moja
 
KAULI MBIU: TUKUZE UCHUMI. TUONDOE UMASIKINI
-
Prof. Sospeter Muhongo

Waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya ESCROW, Profesa Muhongo anatangaza nia moja kwa moja kutoka Musoma.

Tujumuike pamoja.

- Muhongo ameshapanda stejini anawasalimu wahudhuriaji.

==============

''Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika. Siko hapa kumlaumu mtu au kumshambulia mtu, kwa sababu ukimlaumu mtu umasikini bado uko palepale.

Nikisema historia yangu yote muda hautatosha. Kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taaluma nimefikia mwisho. Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.

Nimefanya utafiti kwa miaka 30, chama cha majiologia wa Marekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu. Pia kwa waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.

Kwenye uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.

Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Ni lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.

Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa linanyemelewa na uvivu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa kujiamini. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi.

Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.

Lazima tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni Finland''.

- Anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia ikiwemo India, Brazil, China na Kenya. Sipendi sana kujilinganisha na Kenya kwa sababu sote ni maskini.

Anaendelea...

''Dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa Tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dola bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule mihogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.

Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi.

Naombeni ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa lisiongezeke, mwenye dawa ya umaskini ndani ya CCM, CHADEMA, NCCR ni profesa Muhongo tu. Elimu kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani darasa limerundikana ukafundisha.

Anaeweza ni mimi tu sababu wengine utafiti wanausoma kwenye magazeti tu.

Wana CCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu! Tutatumia rasilimali, madini yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu. Mimi ndio nimetengeneza ramani ya madini ya Tanzania, Africa na duniani nikiwa vice president. Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa uzalendo, ningeweza kuja na ramani na kuiuzia serikali.

Mimi mtu hanidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio dunia ya kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu mnichague. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.

Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye mikono ya uhakika kwa Profesa Muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko chuo kikuu cha Dar es Salaam na nimefanya maisha yangu yote.

Mapato ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu na bunge litakua linaidhinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti. Mtanzania yoyote asiwe na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya watanzania.

Mimi sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba sipendi wawekezaji wa ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe na umeme. Na umeme wa bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara, muda umefika tusijidharau, lazima tushinde.

Lazima watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe wanatumia umeme, tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua mbele professa Muhongo ametimiza ahadi ya CCM, hata ilani mpya inayokuja mtekelezaji atakaetekeleza kwa uhakika ni Profesa.

Ni lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana nazo na nyie wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa sababu hamjui haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu. Wakulima na wafugaji ni mwisho wa kuuana chini ya Prof. Muhongo, tatizo sio ardhi, ni teknolojia.

Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu''.
 
Sielewi anachozungumza kuhusu uanachama wa CCM kwani chama hicho kilizaliwa tarehe 5 Mwezi Febraury mwaka 1977. Siku hiyo kulikuwa na sherehe mbili, ile ya kwanza ikiwa ni miaka kumi ya Azimio la Arusha ambayo kitaifa ilifanyika Dar es Salaam asubuhi, halafu mchana ule ikafanyika sherehe ya uzinduzi wa CCM ambayo ilifanyika kitaifa kule Zanzibar. Katibu Mtendaji wa CCM wakati huo alikuwa Msekwa, ambaye ndiye pia aliye-draft katiba ya CCM. Malipo ya kadi ya CCM ya Muhongo aliyofanya mwaka 1975 yakiwa na muhuli wa Chama cha Mapinduzi yanatia utata kidogo hasa ukizingatia kuwa kujiunga na chama cha mapinduzi wakati huyo haikuwa automatic kutoka TANU bali mtu alitakiwa ahuidhuruie mafunzo ya siasa kwa miezi mitatu.
 
Tukiweka ushabiki pembeni, Prof. Muhongo an IQ kubwa sana. Ila kwa kuwa siasa ya bongo kwa sasa imetawaliwa na ukanda (hasa ukaskazini) ndani na nje ya CCM,atasakamwa sana. Na hataungwa mkono,mengine mbwembwe tu.
 
Intelligence+ arrogance= ignorance. Listeing is more important than talking; if that was not true, God would not have given us two ears and only one mouth.
 
KAULI MBIU: TUKUZE UCHUMI. TUONDOE UMASIKINI - Prof. Sospeter Muhongo

View attachment 256444

Waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya ESCROW, Profesa Muhongo anatangaza nia moja kwa moja kutoka Musoma.

Tujumuike pamoja.

- Muhongo ameshapanda stejini anawasalimu wahudhuriaji.

==============

''Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika. Siko hapa kumlaumu mtu au kumshambulia mtu, kwa sababu ukimlaumu mtu umasikini bado uko palepale.

Nikisema historia yangu yote muda hautatosha. Kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taaluma nimefikia mwisho. Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.

Nimefanya utafiti kwa miaka 30, chama cha majiologia wa Marekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu. Pia kwa waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.

Kwenye uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.

Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Ni lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.

Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa linanyemelewa na uvivu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa kujiamini. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi.

Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.

Lazima tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni Finland''.

- Anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia ikiwemo India, Brazil, China na Kenya. Sipendi sana kujilinganisha na Kenya kwa sababu sote ni maskini.

Anaendelea...

''Dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa Tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dola bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule mihogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.

Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi.

Naombeni ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa lisiongezeke, mwenye dawa ya umaskini ndani ya CCM, CHADEMA, NCCR ni profesa Muhongo tu. Elimu kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani darasa limerundikana ukafundisha.

Anaeweza ni mimi tu sababu wengine utafiti wanausoma kwenye magazeti tu.

Wana CCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu! Tutatumia rasilimali, madini yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu. Mimi ndio nimetengeneza ramani ya madini ya Tanzania, Africa na duniani nikiwa vice president. Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa uzalendo, ningeweza kuja na ramani na kuiuzia serikali.

Mimi mtu hanidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio dunia ya kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu mnichague. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.

Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye mikono ya uhakika kwa Profesa Muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko chuo kikuu cha Dar es Salaam na nimefanya maisha yangu yote.

Mapato ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu na bunge litakua linaidhinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti. Mtanzania yoyote asiwe na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya watanzania.

Mimi sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba sipendi wawekezaji wa ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe na umeme. Na umeme wa bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara, muda umefika tusijidharau, lazima tushinde.

Lazima watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe wanatumia umeme, tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua mbele professa Muhongo ametimiza ahadi ya CCM, hata ilani mpya inayokuja mtekelezaji atakaetekeleza kwa uhakika ni Profesa.

Ni lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana nazo na nyie wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa sababu hamjui haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu. Wakulima na wafugaji ni mwisho wa kuuana chini ya Prof. Muhongo, tatizo sio ardhi, ni teknolojia.

Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu''.

Jamaa yuko vizuri sana.
 
attachment.php

CCM inazidi kudhibitisha kwamba ni chama kikomavu na chenye hazina kubwa ya viongozi wa ngazi zote na usemi kwamba "bila ya CCM imara taifa litayumba" unazidi kudhihirika!

Mmoja kati ya wengi wanaoendelea kutangaza nia ya kupeperusha bandera ya CCM kwa ngazi ya urais ni Prof. Sospeter Muhongo na, kwakweli, kwa kifupi amenifurahisha sana kwa mambo yafuatayo:

1) Siasa za majitaka kwake ni mwiko na hana muda wa kushambulia watu wengine zaidi ya kuainisha matatizo yetu na kutuonyesha njia ambayo anaamini, tukimpa urais, ataitumia kutufikisha Kanaan, nchi yenye maziwa na asali!

2) Kwa muda mfupi sana ameweza kuweka wazi changamoto zinazotukabili na njia ya kuzitatua!
.
.
.
WAGOMBEA WETU WENGINE WANA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA PROF. MUHONGO NA SIONI SABABU YA VITA NDANI YA CHAMA ZAIDI YA KUMPATA MBORA MIONGONI MWA VIONGOZI WETU WOTE !

TUNAWAPENDA VIONGOZI WETU WOTE MLIOTANGAZA NIA NA TUNAWATAKIA KHERI KWENYE MCHAKATO HUU MUHIMU KWA TAIFA!
 
Heeeeee aisee umekula maharage ya wapi wewe?? Kwa nini asijisifie? Unataka asifiwe akifa? Hata mie ningekuwa nimetoboa kama.yeye ningeringa, MUNGU kampa akili mwache aringie bana, nyie mnaojificha na elimu zenu inaonekana mnatambua kuwa mmebebwabebwa tu. Mwache ajivune bana acha wivu

LIMURA RIMESOMA!HHAHAAHAHA. Tatizo waswahili wanarionea wivu kwa kusema fact na ukweli.
harina mchezo hiri, ritawakomesha wavivu na vilaza na vihiyo tetetete...
 
Back
Top Bottom