Kutoka namba 15 hadi namba 5 Afrika, Rais Samia amerudisha heshima ya Diplomasia ya Uchumi na Utalii wa Mikutano ya Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,119
49,843
Hakuna neno unaloweza kutumia ila kusema Heshima ya Tanzania kwenye Majukwaa ya Kimataifa imerejea na Sasa Nchi inatafsiri Kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi Kwa njia ya Mikutano ya Kitalii.

Kabla ya Rais Samia kuingia madarakani Tanzania ilipoteana na kupotea kabisa kwenye Ramani ya Dunia na Afrika kwenye nyanja ya diplomasia ya Uchumi na Utalii wa Mikutano ambapo Kwa mara ya mwisho iliporomoka Hadi kufikia namba 15 Kwa Afrika.

Kumbi zake za mikutano Maarufu kama AICC,JKICC na mahoteli Maarufu ya Kitaliikama Ngurdoto,Impala,Naura Springs nk yalianza kupata hasara Hadi kufikia kuuzwa huku wamiliki wakipata pressure na wengine kufa kutokana na hasara,kufa Kwa utalii na kubambikiwa Kodi na harassments walizofanyiwa awamu Ile.

Ila Mungu si athumani akamleta Mama wa Taifa Samia ambae alifanya kazi kubwa ya kubadili image mbaya iliyojengeka na Sasa matumaini yamerejea tena.

Haraka haraka Tanzania ikaanza kupata Watalii,makongamano ya Kimataifa na Biashara kuanza kurejea Upya kiasi kwamba Sasa Nchi ikapanda kutoka nafasi ya 15 Hadi Nafasi ya 5 Afrika ikitanguliwa na Nchi za South Africa, Morocco,Rwanda, Egypt kisha Tanzania.

Kwa Sasa ni nadra sana mwezi kupita bila Kumbi zetu kupata mikutano ya Kimataifa ya Kanda nk na Kwa Sasa zimeanza kujiendesha Kwa faida kutoka kula hasara miaka 5 iliyopita.
20230915_091445.jpg

Aidha Ili kujidhatiti Serikali imepanga kujenga kumbi nyingine zaidi kwenye Mikoa ya Dar,Dodoma na Arusha ambapo Kwa kuanzia Imeanza ujenzi wa Ukumbi mkubwa wa pili Afrika wa KICC Jijini Arusha na inakusudia kupanuka zaidi na kuboresha ukumbi mkubwa JKICC Ili Kila mmja uwe na uwezo wa ku accommodate washiriki zaidi ya 3,000 na Kuifanya Tanzania kuwa namba 3 Afrika.Ni aibu Tanzania kupitwa na Rwanda.

Hongera sana Rais Samia Kwa kazi nzuri chini ya Kijana wa Mikakati Ephraim Mafuri na kazi iendelee 👇

View: https://youtube.com/watch?v=T7ab8tXKRxo&si=ONofJ6xaQx-b8JCf
 
Sawa ni vizuri sana sie kutambulika kimataifa, ili hili lina saidiaje bibi yangu kule Ikwiriri anae kosa huduma ya afya kijijini?
 
Hili linamsaidia Rais Samia kuelekea uchaguzi ujao ndio maana umeona mleta mada ameelekeza sifa kwa Samia, kazi ya mleta mada ni kumsifu Rais Samia na si kuelezea matatizo ya wananchi.
 
Mikutano ya porojo haina TIJA. Watu wafanye kazi bana. bla bla za majukwaani ndo zimezaa wataalamu wengi kupindukia ambao ni hodari sana kwa .... POROJO .... anasa wanozoishi zinafadhiliwa na masikini wa Tanzania ambao inaelekea wengi wameridhika na porojo na uswahili! Wabobezi wa kuchonga wamo mioyoni mwao, wanakubalika. Mfano wa yule jamaa wa majuzi huko Rufiji. Ni kiongozi wa ngazi za juu. Yaani, we acha tu!
 
Hakuna kazi inafanyika bila vikao,starehe ni sehemu ya kazi ndio maana Kuna biashara ya starehe.

Porojo ni sehemu ya Ajira ndio maana Kuna watu wamejiajiri kuchekesha,wanahitaji kumbi na sites za kuchekesha watu.

Mwisho mwaka huu mikutano ya kimataifa inaenda kuingizia Taifa sh.Bil.48(in terms of dollars) ambazo ni za direct Bado wanufaika kwenye biashara za malazi,vyakula,muziki nk
 
Hili linamsaidia Rais Samia kuelekea uchaguzi ujao ndio maana umeona mleta mada ameelekeza sifa kwa Samia, kazi ya mleta mada ni kumsifu Rais Samia na si kuelezea matatizo ya wananchi.
Linamsaidiaje Rais Sasa hapo? Hizo pesa zinazoletwa na hao Wageni zinaenda Kwa Rais? Punguza kuwa mbumbumbu.
 
Hakuna neno unaloweza kutumia ila kusema Heshima ya Tanzania kwenye Majukwaa ya Kimataifa imerejea na Sasa Nchi inatafsiri Kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi Kwa njia ya Mikutano ya Kitalii.

Kabla ya Rais Samia kuingia madarakani Tanzania ilipoteana na kupotea kabisa kwenye Ramani ya Dunia na Afrika kwenye nyanja ya diplomasia ya Uchumi na Utalii wa Mikutano ambapo Kwa mara ya mwisho iliporomoka Hadi kufikia namba 15 Kwa Afrika.

Kumbi zake za mikutano Maarufu kama AICC,JKICC na mahoteli Maarufu ya Kitaliikama Ngurdoto,Impala,Naura Springs nk yalianza kupata hasara Hadi kufikia kuuzwa huku wamiliki wakipata pressure na wengine kufa kutokana na hasara,kufa Kwa utalii na kubambikiwa Kodi na harassments walizofanyiwa awamu Ile.

Ila Mungu si athumani akamleta Mama wa Taifa Samia ambae alifanya kazi kubwa ya kubadili image mbaya iliyojengeka na Sasa matumaini yamerejea tena.

Haraka haraka Tanzania ikaanza kupata Watalii,makongamano ya Kimataifa na Biashara kuanza kurejea Upya kiasi kwamba Sasa Nchi ikapanda kutoka nafasi ya 15 Hadi Nafasi ya 5 Afrika ikitanguliwa na Nchi za South Africa, Morocco,Rwanda, Egypt kisha Tanzania.

Kwa Sasa ni nadra sana mwezi kupita bila Kumbi zetu kupata mikutano ya Kimataifa ya Kanda nk na Kwa Sasa zimeanza kujiendesha Kwa faida kutoka kula hasara miaka 5 iliyopita.
View attachment 2749757
Aidha Ili kujidhatiti Serikali imepanga kujenga kumbi nyingine zaidi kwenye Mikoa ya Dar,Dodoma na Arusha ambapo Kwa kuanzia Imeanza ujenzi wa Ukumbi mkubwa wa pili Afrika wa KICC Jijini Arusha na inakusudia kupanuka zaidi na kuboresha ukumbi mkubwa JKICC Ili Kila mmja uwe na uwezo wa ku accommodate washiriki zaidi ya 3,000 na Kuifanya Tanzania kuwa namba 3 Afrika.Ni aibu Tanzania kupitwa na Rwanda.

Hongera sana Rais Samia Kwa kazi nzuri chini ya Kijana wa Mikakati Ephraim Mafuri na kazi iendelee 👇

View: https://youtube.com/watch?v=T7ab8tXKRxo&si=ONofJ6xaQx-b8JCf

Naunga mkono hoja hii kitu sii mchezo!
P
 
Attachments

  • Strategy Update Editors Forum 2023.ppt
    53.2 MB · Views: 2
Kiukweli upumbavu unaufanya wewe ndio maana unaitwa chawa hata kama sio chawa kweli, haiwezekani mwananchi ukajipa kazi ya kusifia na kumtetea Rais pamoja na serikali yake kwa nguvu zote kuliko hata kuelezea changamoto zilizopo. Lengo la kufanya hivyo ni lipi hasa? Huo ndio upumbavu.
Kazi ya kuelezea Changamoto ni Yako na ukae ukikua hakuna Changamoto Mpya Bali ni zile zile na ziko known ni Suala la mda kuzitatua.

Mimi namsifia mama Kwa sababu Kwa upande wangu amenitatulia Changamoto nyingi sana tofauti na waliotangulia.Why nisimsifie? Nimsigie mama yako au Mbowe? Kwa lipi?
 
Ni kosa kufanya hivo?
Walipofanya vema wapongezwe, walipofanya vibaya wasemwe
Kwenye changamoto tuseme pia, kazi sio kupiga kelele na kuonyesha mabaya bila kusema mazuri pia, try to be positive
 
Umeeleza kweli kabisa kuwa kinachokufanya umsifie ni kwa sababu tu ametatua changamoto zako ila kibaya unataka tumuone huyu mama ni kiongozi bora na anafanya vizuri na unamtetea kisa tu wewe changamoto zako amezitatua.

Sie tukieleza changamoto zilizopo na kumkosoa tunaonekana ni roho mbaya hatumpendi tu, hivyo ndivyo ambavyo nyie mliyotatuliwa changamoto zenu mnavyotuona sie.
 
Tatizo wanaosema mazuri hawataki kusikia mabaya wanachukulia wanaosema mabaya wanamchukia Rais kwamba ni kwa sababu tu hatumpendi.

Ingekuwa tunasifia kwenye mazuri na kukosoa kwenye mapungufu ingekuwa vizuri ila sisi unakuta raia tu kajipa kazi ya kumsifia na kumtetea Rais kwenye kila jambo, yani yeye humkuti anakosoa kila kitu kwake ni sahihi tu.
 
Umeeleza kweli kabisa kuwa kinachokufanya umsifie ni kwa sababu tu ametatua changamoto zako ila kibaya unataka tumuone huyu mama ni kiongozi bora na anafanya vizuri na unamtetea kisa tu wewe changamoto zako amezitatua.

Sie tukieleza changamoto zilizopo na kumkosoa tunaonekana ni roho mbaya hatumpendi tu, hivyo ndivyo ambavyo nyie mliyotatuliwa changamoto zenu mnavyotuona sie.
Huyu ni Kiongozi Bora kabisa kuwahi kutokea
 
Back
Top Bottom