Kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue: Siku 100 za Rais Magufuli

Siku 100 tangu Rais Dk John Magufuli aingie madarakani. Rais Magufuli aliingia madarakani rasmi Novemba 5, mwaka jana baada ya kuapishwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano, akipokea kijiti cha kuiongoza Tanzania kutoka kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Nianze kwa kumpongeza kwa siku hizi 100, ambazo tumeamua kuzitumia kutathmini mafanikio yaliyopatikana kwa siku hizi chache tangu aingie madarakani. Hongera sana! Mheshimiwa Rais nakupa pongezi hizi, si kwa sababu mimi ni mtumishi katika moja ya taasisi za serikali, bali nakupa pongezi hizi kama mwananchi wa kawaida, maana hakika kazi yako ya siku hizi chache ulizokaa madarakani, tumeiona na mabadiliko tunayaona.

Nani asiyejua kuwa hadi hivi sasa makusanyo ya kodi yameongezeka maradufu? Kama sio wewe na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na kikosi kazi chenu, na kufanya ziara za kushtukiza Bandarini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katu kodi na mapato hayo yasingepatikana.

Hongera sana! Kama si wewe Rais, Waziri Mkuu na kikosi kazi chenu, hadi leo hii makontena yangezidi kupotea na huenda kwa siku hizi 100, tungesikia hadi meli zilizopiga nanga pale bandarini kupakua au kupakia mizigo, nazo zimepotea na hazijulikani zilipo. Pia Rais nakupa pongezi kwa kuweza kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali na taasisi zake, hasa pale ulipoagiza fedha za Sherehe ya Uhuru kwenda kufanyia upanuzi wa barabara na kununua vitanda hospitalini.

Mbali na hilo la kubana matumizi, pia ulisisitiza TRA kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kuwalipa posho wabunge nje ya malipo wanayolipwa na Bunge. Hili limefanikiwa ; na makusanyo yameongeza maradufu.

Siku ile ulipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kusalimia wagonjwa, hukwenda kumuona tu mgonjwa uliyekwenda kumuona, bali uliingia katika baadhi ya wadi hapo Muhimbili na ziara yako hiyo, umeleta mabadiliko makubwa sana yaliyopo hivi sasa.

Sisi walalahoi tulifaidika na ujio wako, maana mashine za MRI na CT Scan, si tu zilitengenezwa kwa haraka, lakini pia mashine mpya zilikuja. Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ulitoa tathmini ya siku 100 ulizokaa madarakani na kusema wameongeza mapato kwa asilimia 90.

Lakini kubwa zaidi ni huduma za afya zimeboreshwa hospitalini hapo na kuweza kunufaisha wapiga kura wako. Hakuna sekta ambayo umeigusa hadi sasa na ikashindwa kuleta tija kwa wananchi wako. Hata leo hii ukienda pale kijijini kwetu Kinyenze wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, watakuambia jinsi walivyonufaika na mpango huu wa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne.

Kwa upande wa elimu ya juu, nako ni neema tupu kwani Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika siku 100 za kuwapo kwako madarakani, umeweza kuwaongezea Sh bilioni 132. Kufuatia fedha hizo, sasa idadi ya wanufaika imeongezeka na kufikia 122,786 ambao wamepata jumla ya Sh bilioni 461.1.

Hivi karibuni uliposema unataka nchi iende, ulisisitiza kuwa itaenda na anayefikiri ataikwamisha, atakwama yeye basi nakuambia kuwa tayari nchi inaenda; Na siku utakayotimiza siku 365, basi nchi itakuwa inakimbia kwa mwendo kasi na hakuna atakayeweza kuikwamisha.

Katika upande wa utendaji kazi na uwajibikaji, nako si kwa kusema maana kila kona tunaona namna mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanavyowajibika na kuchapa kazi, kama kaulimbiu yako ya ‘Hapa Kazi Tu’ inavyojieleza.

Leo watu wanafanya kazi ; na nidhamu kwa watumishi imeanza kuonekana. Wamebaki wachache tu, ambao naamini tunapoelekea siku 365 (mwaka mmoja) wa wewe kuwa madarakani, hawa wote watanyooka.

Kama watakuwa ndio wale, wasiotaka nchi iende kwa kukukwamisha, basi najua watakwama wao na nchi itakwenda kwa kasi zaidi. Binafsi nakuombea heri na fanaka katika utekelezaji wa majukumu yako, kama kiongozi mkuu wa nchi na Mungu akulinde na kukujalia afya njema.
 
LEO Rais John Magufuli ametimiza siku 100 tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka jana, kuingia Ikulu iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam.

Katika Makala haya Francisca Emmanuel anaelezea maoni ya watu mbalimbali kuhusu utendaji wa Magufuli.

KATIKA siku 100 za uongozi wa Rais John Magufuli mambo mbalimbali ameyafanya ikiwa ni pamoja na kurudisha heshima ya utumishi wa umma, kupunguza matumizi ya fedha za serikali ambapo imeenda sambamba na kutumbua majipu. Suala la kurudisha heshima ya utumishi wa umma, Rais Magufuli anahakikisha kwamba watumishi wote wa umma, wanafanya kazi kulingana na matakwa ya jamii na sio kufanya kazi binafsi na wanazozitaka wenyewe kwa muda ambao wanajipangia.

Mara baada ya kuingia madarakani alivunja bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na utendaji usiokidhi mahitaji ya jamii. Ili kudhibiti matumizi ya serikali, Rais Magufuli alitumbua majipu mbalimbali ikiwemo katika Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) ambapo alimsimamisha kazi Mkurugenzi wake, Awadhi Massawe na kuvunja bodi ya wakurugenzi.

Mbali na TPA, Rais Magufuli alitumbua majipu ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka aliyedaiwa kushindwa kusimamia vizuri shirika hilo. Pia alimsimamisha kazi Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki na Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bashe kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye kodi ya serikali ya thamani ya Sh bilioni 80 ambapo baadaye idadi ya makontena yaliyopotea yalifikia takribani 2,780 na kukwepa kodi inayokadiriwa kuzidi Sh bilioni 600.

Hadi Desemba mwaka jana, TRA ilitangaza kukusanya kodi ya Sh bilioni 11 kwa mwezi mmoja pekee ikiwa ni fedha zitokanazo na makontena 329 ambayo yalikuwa hayajalipiwa kodi. Viongozi mbalimbali wametoa maoni yao kuhusiana na utendaji wa Rais Magufuli ambapo viongozi mbalimbali kutoka vyama vya upinzani wanasema kuwa kasi yake katika ukusanyaji wa kodi itasaidia katika kufikia malengo ya kuhudumia jamii kupitia vipaumbele vyake hususan vya elimu, afya na barabara.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Abdallah Safari anasema kuwa kodi zinazokusanywa zinaweza kuisaidia kupata huduma mbalimbali za kijamii. ‘’Kasi aliyoanza nayo inaridhisha hususan katika masuala ya ukusanyaji kodi, kwani inaleta matumaini na kwamba itasaidia katika utoaji wa huduma za jamii,’’ anasema Profesa Safari.

Pia anasema kuwa jambo ambalo Rais Magufuli anatakiwa kufanya kwa sasa ni kupitia upya mikataba ya madini na kuifanyia marekebisho ili kuboresha maisha ya Watanzania. Alitolea mfano wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwamba alipitia alifanikiwa kutoa elimu bure kwa kuwa alitumia fedha zilizopatikana kwenye madini. Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba anasema kuwa chama chake kimeridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli kwa kuwa mfumo wake upo tofauti na chama chake cha CCM.

Mwigamba anasema kuwa hatua anazoendelea kuchukua ni kutokana na kutokuwa na mtandao uliomwingiza Ikulu. ‘’Hana deni wala mtandao wowote uliomfanya aingie Ikulu, ndio maana anachukua hatua za kupambana na ufisadi ili kuhakikisha kwamba serikali inaingiza mapato yake kama ilivyotegemewa,’’ anasema Mwigamba. Anasisitiza kuwa Watanzania wanatakiwa kuendelea kumuombea ili aweze kufanya mambo makubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Anasema jambo linalotakiwa kufanywa kwa sasa ni kufanya marekebisho ya sheria mbaya ili Rais ajaye aweze kuzisimamia sheria hizo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba anasema kuwa Rais Magufuli anatakiwa kuendelea kuwabana watendaji wasio waadilifu na wabovu ili kuweka mfumo imara wa kiutendaji kwa viongozi wa ngazi zote. ‘’Tunajua kwamba Rais hawezi kufanya shughuli zote za serikali, hivyo akiweka mfumo wa kuwa na watendaji waadilifu tunaamini mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa,’’ anasema Lipumba.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi anasema kuwa licha ya Rais Magufuli kuanza vizuri katika utendaji wake, inatakiwa wazidi kumpa muda ili kufanya mambo mazuri zaidi. Muabhi anasema kuwa katika siku 100 tangu aingie madarakani, wananchi wameweza kutathmini utendaji wake. Marais wengi wanaingizwa madarakani na matajiri ili kutimiza matakwa yao, lakini ni tofauti na Rais Magufuli ambaye anaonesha kwa vitendo kwamba si rais wa aina hiyo.

Mwanaharakati wa haki za binadamu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukweli na Maridhiano kutoka Chama cha Tanzania Labour (TLP), Joramu Kinanda anasema kuwa alipofikia Rais Magufuli amefanikiwa kwa kuwa ameonesha nia ya kufanya kitu ndani ya nchi. Kinanda anasema kuwa licha ya mazuri aliyoyafanya, bado anachotakiwa kukifanya hajakifikia kwa asilimia 100 kwa kuwa anakumbana na vikwazo vingi.

Anasisitiza kuwa ili kufanikiwa katika kutimiza adhma yake, ni lazima atende haki pamoja na kuendelea kumtanguliza Mungu mbele kwa sababu umma wa Watanzania upo nyuma yake. Anasema kuwa katika kutekeleza majukumu yake, Rais Magufuli anatakiwa asisahau kuheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaongeza kuwa wapo baadhi ya watu wanashiriki katika kuwakandamiza Watanzania lakini kwa kuwa wamejificha, hawaonekani.

Anasema Rais anatakiwa kushuka katika serikali za mitaa na kwa watu wa kawaida kusikiliza matatizo yao kwani atapata mambo mengi ambayo wananchi wanakerwa nayo. ‘’Kuna mambo mengi yanafanyika lakini ni vigumu kuyapata kwa kuwa wapo baadhi yao wanajificha na kwamba wanawakandamiza walio chini yao hivyo nao wanatakiwa watafutwe ili watumbuliwe,’’ anasema.

’’ Akitolea mfano wa bomoabomoa, Kinanda anasema kuwa maeneo ya Pugu Mnadani, serikali inayo hati ya kumiliki mnada huo tangu mwaka 1939 baadaye mwaka 1976 Nyerere alibariki kuanzishwa kwa mnada huo. Anasema kwa sasa serikali inawaona watu hao kuwa wamevamia maeneo hayo hivyo Rais anatakiwa kuingilia kati ili kujua ukweli wa suala hilo. ‘’Pia tunaomba Rais aweze kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa sababu Tanzania haiwezekani kufanya kazi bila ya kuwa na vyama,’’ anasema Kinanda.

Pia anasema kuwa suala ambalo limekuwa kitendawili kwa sasa ni la uchaguzi Zanzibar ambalo Rais anatakiwa kutumia busara kumaliza mgogoro huo. Kinanda anasema kuwa ili kutatua tatizo hilo ni lazima kuzingatia haki bila kuweka mbele maslahi ya vyama kwa kuweka muafaka sahihi wa kutatua tatizo hilo. Mbunge wa CUF Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea anasema kuwa wananchi wana imani na Magufuli kwa kuonesha kuwa analosema analitekeleza.

Mtolea anasema kuwa Rais anatakiwa kutumia nafasi yake kutatua changamoto zinazoikabili Zanzibar kwa sasa. Pia anasema kuwa kwa Jiji la Dar es Salaam, sekta ya afya inakabiliwa na changamoto kubwa licha ya hospitali za Temeke, Amana na Mwananyamala kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali za Mikoa. ‘’Hospitali hizo zimeendelea kuachwa zikihudumiwa na halmashauri huku zikikabiliwa na ukosefu wa vitanda, dawa na maslahi ya watumishi, hivyo serikali inapaswa kufanyia kazi changamoto hizo,’’ anasema Mtolea.

Katika kuonesha kuikubali kasi ya Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano, waliikubali hotuba ya Rais huyo ambayo aliitoa wakati wa kuzindua Bunge la 11. Pia wameomba wananchi wanaowawakilisha kuendelea kumuombea Rais Magufuli ili aweze kutimiza malengo yake na kumlinda dhidi ya maadui na wale wote wanaochukizwa na utendaji wake mzuri.
 
MARA tu baada ya kuingia Ikulu, Rais John Magufuli alitembelea Wizara ya Fedha na Mipango ili kujionea shughuli zinazofanywa na wizara hiyo nyeti katika uchumi wa nchi yetu na huku pia akiwa na neno moyoni.

Wizara ya Fedha ndiyo ambayo inasimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) na kuyapangia bajeti inayotokana na kilichokusanywa pamoja na misaada au mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo. Ni kwa kutambua hili, na kwa kuzingatia ahadi zake wakati wa kampeni ambazo ili zifanikiwe zinahitaji fedha, ndio maana Rais akiwa na saa chache toka aingie Ikulu akalazimika kuzuru katika wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi wakuu wa wizara, kipindi hicho akiwa ni katibu mkuu wa wizara na watendaji wenzake.

Alitoa maagizo ya namna ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, akasisitiza pia waongeze ukusanyaji wa mapato ya serikali ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kuwalipa posho wabunge nje ya malipo wanayolipwa na Bunge. Ziara hiyo ya ghafla ilimwezesha Rais kutoa maagizo kwa watendaji wa Wizara ya Fedha kuhakikisha kuwa wanavunja haraka mtandao wa wakwepa kodi, na kwamba wizara itoe maelekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili ikusanye kodi halali za serikali kwa mujibu wa sheria.

Kwa nia ya kudhibiti mianya ya wakwepa kodi, Rais Magufuli alisisitiza kuwa katika serikali anayoiongoza, hakuna mkubwa yeyote atakayeruhusiwa kutoa ‘kimemo’ kwa TRA kwa lengo la kusamehe ulipaji kodi halali za serikali. Hatua hii ilidhihirisha namna Rais Magufuli, siyo tu anavyokerwa na uzembe unaoweza kujitokeza katika ukusanyaji kodi halali za serikali bali pia kuhakikisha kwamba serikali anayoiongoza haitakuwa na mchezo katika suala zima la ukusanyaji mapato na udhibiti wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Katika kuhakikisha kwamba alichokuwa anazungumza hatanii, siku chache baadaye, Serikali ya Rais Magufuli ikabaini upotevu wa makontena 329 ambayo yalitoroshwa kwenye bandari za nchi kavu (ICD) bila kulipiwa ushuru na kuikosesha Serikali zaidi ya Sh bilioni 80. Kilichotokea hapo ni Rais kumsimamisha Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade na makamishna wengine wa TRA wakasimamishwa kazi sambamba na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kutumia madaraka vibaya.

Rais Magufuli hakukomea hapo, aliendelea kuwabana wakwepa kodi na baadaye akakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara ambako aliwataka walipe kodi stahiki za Serikali. Akatoa siku saba kwa waliokwepa kodi kupitia utoroshaji wa makontena wawe wamelipa kodi hiyo.

Sehemu kubwa ya kiasi hicho kilichokuwa kimeshapotea kilipatikana. Kutokana na juhudi hizo baadaye Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata, alisema malengo ya ukusanyaji kodi yaliyofikiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni baada ya kazi nzuri ya Rais kuwabana walipa kodi ambapo kwa mwezi Desemba ilivuka lengo la ukusanyaji mapato kutokana na kukusanya Sh trilioni1.4.

Ongezeko la makusanyo hayo kwa mujibu wa Kidata ilikuwa ni wastani wa Sh bilioni 490 kwa mwezi ikilinganisha na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba ambayo yalikuwa ni kati ya Sh bilioni 850 na 900. Makusanyo hayo yamekuwa yakiongezeka kuelekea kwenye Sh trilioni 1.5 kwa mwezi na hakuna ubishi kwamba mafanikio hayo yametokana na mikakati mizuri ambayo Rais wa Awamu ya Tano tangu aingie madarakani ameiweka, ikiwemo kuteketeza mianya ya upotevu wa mapato.

Akizungumzia hali ya uchumi na mapato ya nchi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Servacius Likwelile, anasema Serikali imeweza kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo bila ya kutegemea fedha za wahisani kutokana na makusanyo ya mwezi Januari mwaka huu. Dk Likwelile anasema Rais Magufuli alisisitiza suala la kuongeza makusanyo ya mapato ya kodi, kwa kuwataka wale wote wanaostahili kulipa kodi walipe, ili fedha hizo zifanye kazi ya maendeleo ya taifa.

Anasema kwa msisitizo huo, makusanyo ya mapato ni mazuri na kwamba mwelekeo ya makusanyo ya Januari mwaka huu hadi sasa ni zaidi ya Sh trilioni moja na kwamba mategemeo ni kufikia Sh trilioni 1.5 na ana uhakika lengo hilo litafikiwa na kuvuka. Katibu Mkuu huyo anasema kutokana na mfumo mzuri uliowekwa hivi sasa wa kubana matumizi yasiyo na tija na kuweka vipaumbele kwenye mambo muhimu, serikali imeweza kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo na hivyo utegemezi wa wahisani kuwa mdogo.

Anasema kwa mwezi Januari mwaka huu serikali imetenga Jumla ya Sh bilioni 318.406, fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi yote ya maendeleo ambayo imepewa vipaumbele. Miradi hiyo ya vipaumbele ni pamoja na elimu, afya, maji, barabara, umeme na kulipa madeni na pensheni za wastaafu. “Suala la kujivunia ni kwamba tunaweza kutoa fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi yetu ya maendeleo, fedha za wahisani za nje ni kidogo sana.

Mfano kwa mwezi huu Januari, fedha za nje ni Sh bilioni 71.2, wakati fedha za ndani ni bilioni 318.406”, anasema Dk Likwelile. Faida ya ukusanyaji kodi makini na ubanaji matumizi imejitokeza katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na serikali kulipa makandarasi wa ujenzi wa barabara huku ikiahidi kwamba kufikia Juni wote watakuwa wamelipwa na kufufua miradi iliyosimama.

Katika muktadha huo, wiki hii kwa mara ya kwanza Mahakama ya Tanzania ilipokea asilimia 100 ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya kuhakikisha wanafanikisha huduma za utoaji wa haki kwa wananchi. Hii ilikuwa ni baada ya Serikali kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli kwa kuipa Mahakama Sh bilioni 12.3 aliyoahidi Siku ya Sheria, Februari 4, mwaka huu ili kutekeleza miradi yao ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anasema idadi ya watu wanaolipa kodi kwa sasa hapa nchini bado ndogo, kwa maana ya kwamba wanaopaswa kulipa kodi ni wengi kuliko wanaolipa, hivyo amewaagiza wafanyabiashara wote kujisajili wapatiwe namba ya mlipa kodi (TIN). Pia amewataka waache tabia ya kufanya udanganyifu kwa kuwa na vitabu vingi vya utunzaji wa kumbukumbu za biashara.

Sambamba na hilo amewaagiza wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanatoa stakabadhi na suala hilo lisiwe hiyari. Amewataka wote watumie mashine za EFDs na serikali inaendelea na mpango wa kununua nyingine ili wagawiwe bure. Anawataka wafanyabiashara kutoa taarifa kwa Kamishna Mkuu wa TRA kama kuna mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) au wa halmashauri ya wilaya ambaye atadai hongo au atawanyanyasa wakati wa kudai kodi.

Katika kutekeleza hilo, waziri huyo amewapatia namba zake pamoja na za kamishna na kuwataka waache tabia ya kutoa rushwa ili wasilipe kodi. Dk Mpango pia anawataka wafanyabiashara waache kufanya biashara za magendo ambazo zimeshamiri katika pwani ya bahari ya Hindi na kwenye Ziwa Victoria, badala yake wafanye biashara halali. “Tumewadhamiria na tutapambana na magendo hayo. Tunajua kuna watumishi kama polisi wanashiriki kusindikiza magendo hayo, ila nasema hatutamwogopa mtu,” anasisitiza Waziri Mpango.

Anasema hatua zinazofanywa na Serikali ya Rais Magufuli ya kukusanya kodi haina malengo ya kumwonea mtu bali inalenga kuifanya nchi iweze kujitegemea na kupunguza utegemezi. Anasema yeye kama Waziri wa Fedha asingependa kuwa ombaomba kwa wahisani kutokana na kuwa na masharti magumu ambayo mengine yanadhalilisha maadili ya Mtanzania kwani wahisani wanaweza kutaka nchi iruhusu ndoa za mashoga kama inataka misaada.

Dk Mpango anasema kama alivyowahi kusema mwasisi wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, kwamba Serikali yoyote ambayo haikusanyi kodi lazima itajaa rushwa. Anaongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitamvumilia mfanyabiashara au mtu yeyote ambaye atakwepa kodi. Anasema Watanzania wengi ni masikini na hivyo lazima kodi ikusanywe ili wakombolewe kutoka kwenye lindi la umasikini.
 
nakuomba magufuli uvae viatu vya mandela na ukichoka vaa busara za nyerere,kiukwel uki2mia busara hzo,zanzbar utaiokoa,usiangalie maslah ya chama,kwan chama hakitadumu milele,angalia maslah ya taifa, plz we need peace and harmony
 
Ukimsikiliza kwa makin unajua dhamira ya kiongozi, walao tunaona wapi tunaelekea, ni vyema sasa pia akaja na mkakati wa hao wanaosimamishwa ni lini uchunguzi utakamilika, pia chanzo bado ni kimoja tu pale bandarini, uelekeo pia uende kwenye madini, kunandege kila siku zinachukua mchanga wa dhahabu kupeleka ngambo.. wawakataze ili pia mapato yaingie tz..

Ongera rais magufuri kwa kuifanya nchi kuwa na heshima,
Ila mkuu, nie natofautiana na wengi tu. Kama tungekuwa na katiba nzuri ambayo ingekuwa inamlazimisha kila mmoja wetu kuitekeleza (sio kuitetea) kama USA lingekuwa jambo jema la kutathimini siku mia hizi Rais wetu ametekelezaje na sio 'one man show'.
 
Hatumia 1000 mkuu inaanza na hatua 1, ninaamini katiba itapatikana ila kwanza hayo mambo mhim hayana budi kufanyika, USA ni advanced democratic, hatuwezi kuamka tukajikuta huko, tunaenda polepole mkuu
 
Polepole! Mkuu, tuna miaka zaidi ya hamsini tokea uhuru na muungano. Sie tukitawaliwa USA ilikuwa huru zamani lakini mpaka hapa hatujaona umuhimu wa kuwa na katiba nzuri kama hao? Nadhani hapa ni dhamira tu ya wakubwa kwani wananufaika.
 
MARA tu baada ya kuingia Ikulu, Rais John Magufuli alitembelea Wizara ya Fedha na Mipango ili kujionea shughuli zinazofanywa na wizara hiyo nyeti katika uchumi wa nchi yetu na huku pia akiwa na neno moyoni.

Wizara ya Fedha ndiyo ambayo inasimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) na kuyapangia bajeti inayotokana na kilichokusanywa pamoja na misaada au mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo. Ni kwa kutambua hili, na kwa kuzingatia ahadi zake wakati wa kampeni ambazo ili zifanikiwe zinahitaji fedha, ndio maana Rais akiwa na saa chache toka aingie Ikulu akalazimika kuzuru katika wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi wakuu wa wizara, kipindi hicho akiwa ni katibu mkuu wa wizara na watendaji wenzake.

Alitoa maagizo ya namna ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, akasisitiza pia waongeze ukusanyaji wa mapato ya serikali ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kuwalipa posho wabunge nje ya malipo wanayolipwa na Bunge. Ziara hiyo ya ghafla ilimwezesha Rais kutoa maagizo kwa watendaji wa Wizara ya Fedha kuhakikisha kuwa wanavunja haraka mtandao wa wakwepa kodi, na kwamba wizara itoe maelekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili ikusanye kodi halali za serikali kwa mujibu wa sheria.

Kwa nia ya kudhibiti mianya ya wakwepa kodi, Rais Magufuli alisisitiza kuwa katika serikali anayoiongoza, hakuna mkubwa yeyote atakayeruhusiwa kutoa ‘kimemo’ kwa TRA kwa lengo la kusamehe ulipaji kodi halali za serikali. Hatua hii ilidhihirisha namna Rais Magufuli, siyo tu anavyokerwa na uzembe unaoweza kujitokeza katika ukusanyaji kodi halali za serikali bali pia kuhakikisha kwamba serikali anayoiongoza haitakuwa na mchezo katika suala zima la ukusanyaji mapato na udhibiti wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Katika kuhakikisha kwamba alichokuwa anazungumza hatanii, siku chache baadaye, Serikali ya Rais Magufuli ikabaini upotevu wa makontena 329 ambayo yalitoroshwa kwenye bandari za nchi kavu (ICD) bila kulipiwa ushuru na kuikosesha Serikali zaidi ya Sh bilioni 80. Kilichotokea hapo ni Rais kumsimamisha Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade na makamishna wengine wa TRA wakasimamishwa kazi sambamba na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kutumia madaraka vibaya.

Rais Magufuli hakukomea hapo, aliendelea kuwabana wakwepa kodi na baadaye akakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara ambako aliwataka walipe kodi stahiki za Serikali. Akatoa siku saba kwa waliokwepa kodi kupitia utoroshaji wa makontena wawe wamelipa kodi hiyo.

Sehemu kubwa ya kiasi hicho kilichokuwa kimeshapotea kilipatikana. Kutokana na juhudi hizo baadaye Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata, alisema malengo ya ukusanyaji kodi yaliyofikiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni baada ya kazi nzuri ya Rais kuwabana walipa kodi ambapo kwa mwezi Desemba ilivuka lengo la ukusanyaji mapato kutokana na kukusanya Sh trilioni1.4.

Ongezeko la makusanyo hayo kwa mujibu wa Kidata ilikuwa ni wastani wa Sh bilioni 490 kwa mwezi ikilinganisha na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba ambayo yalikuwa ni kati ya Sh bilioni 850 na 900. Makusanyo hayo yamekuwa yakiongezeka kuelekea kwenye Sh trilioni 1.5 kwa mwezi na hakuna ubishi kwamba mafanikio hayo yametokana na mikakati mizuri ambayo Rais wa Awamu ya Tano tangu aingie madarakani ameiweka, ikiwemo kuteketeza mianya ya upotevu wa mapato.

Akizungumzia hali ya uchumi na mapato ya nchi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Servacius Likwelile, anasema Serikali imeweza kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo bila ya kutegemea fedha za wahisani kutokana na makusanyo ya mwezi Januari mwaka huu. Dk Likwelile anasema Rais Magufuli alisisitiza suala la kuongeza makusanyo ya mapato ya kodi, kwa kuwataka wale wote wanaostahili kulipa kodi walipe, ili fedha hizo zifanye kazi ya maendeleo ya taifa.

Anasema kwa msisitizo huo, makusanyo ya mapato ni mazuri na kwamba mwelekeo ya makusanyo ya Januari mwaka huu hadi sasa ni zaidi ya Sh trilioni moja na kwamba mategemeo ni kufikia Sh trilioni 1.5 na ana uhakika lengo hilo litafikiwa na kuvuka. Katibu Mkuu huyo anasema kutokana na mfumo mzuri uliowekwa hivi sasa wa kubana matumizi yasiyo na tija na kuweka vipaumbele kwenye mambo muhimu, serikali imeweza kutumia fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo na hivyo utegemezi wa wahisani kuwa mdogo.

Anasema kwa mwezi Januari mwaka huu serikali imetenga Jumla ya Sh bilioni 318.406, fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi yote ya maendeleo ambayo imepewa vipaumbele. Miradi hiyo ya vipaumbele ni pamoja na elimu, afya, maji, barabara, umeme na kulipa madeni na pensheni za wastaafu. “Suala la kujivunia ni kwamba tunaweza kutoa fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi yetu ya maendeleo, fedha za wahisani za nje ni kidogo sana.

Mfano kwa mwezi huu Januari, fedha za nje ni Sh bilioni 71.2, wakati fedha za ndani ni bilioni 318.406”, anasema Dk Likwelile. Faida ya ukusanyaji kodi makini na ubanaji matumizi imejitokeza katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na serikali kulipa makandarasi wa ujenzi wa barabara huku ikiahidi kwamba kufikia Juni wote watakuwa wamelipwa na kufufua miradi iliyosimama.

Katika muktadha huo, wiki hii kwa mara ya kwanza Mahakama ya Tanzania ilipokea asilimia 100 ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya kuhakikisha wanafanikisha huduma za utoaji wa haki kwa wananchi. Hii ilikuwa ni baada ya Serikali kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli kwa kuipa Mahakama Sh bilioni 12.3 aliyoahidi Siku ya Sheria, Februari 4, mwaka huu ili kutekeleza miradi yao ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anasema idadi ya watu wanaolipa kodi kwa sasa hapa nchini bado ndogo, kwa maana ya kwamba wanaopaswa kulipa kodi ni wengi kuliko wanaolipa, hivyo amewaagiza wafanyabiashara wote kujisajili wapatiwe namba ya mlipa kodi (TIN). Pia amewataka waache tabia ya kufanya udanganyifu kwa kuwa na vitabu vingi vya utunzaji wa kumbukumbu za biashara.

Sambamba na hilo amewaagiza wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanatoa stakabadhi na suala hilo lisiwe hiyari. Amewataka wote watumie mashine za EFDs na serikali inaendelea na mpango wa kununua nyingine ili wagawiwe bure. Anawataka wafanyabiashara kutoa taarifa kwa Kamishna Mkuu wa TRA kama kuna mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) au wa halmashauri ya wilaya ambaye atadai hongo au atawanyanyasa wakati wa kudai kodi.

Katika kutekeleza hilo, waziri huyo amewapatia namba zake pamoja na za kamishna na kuwataka waache tabia ya kutoa rushwa ili wasilipe kodi. Dk Mpango pia anawataka wafanyabiashara waache kufanya biashara za magendo ambazo zimeshamiri katika pwani ya bahari ya Hindi na kwenye Ziwa Victoria, badala yake wafanye biashara halali. “Tumewadhamiria na tutapambana na magendo hayo. Tunajua kuna watumishi kama polisi wanashiriki kusindikiza magendo hayo, ila nasema hatutamwogopa mtu,” anasisitiza Waziri Mpango.

Anasema hatua zinazofanywa na Serikali ya Rais Magufuli ya kukusanya kodi haina malengo ya kumwonea mtu bali inalenga kuifanya nchi iweze kujitegemea na kupunguza utegemezi. Anasema yeye kama Waziri wa Fedha asingependa kuwa ombaomba kwa wahisani kutokana na kuwa na masharti magumu ambayo mengine yanadhalilisha maadili ya Mtanzania kwani wahisani wanaweza kutaka nchi iruhusu ndoa za mashoga kama inataka misaada.

Dk Mpango anasema kama alivyowahi kusema mwasisi wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, kwamba Serikali yoyote ambayo haikusanyi kodi lazima itajaa rushwa. Anaongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitamvumilia mfanyabiashara au mtu yeyote ambaye atakwepa kodi. Anasema Watanzania wengi ni masikini na hivyo lazima kodi ikusanywe ili wakombolewe kutoka kwenye lindi la umasikini.
ulijua unaanzisha uzi mpya mkuuu...
loh
teh
 
Acheni Ujinga Yaandike uweke na Video hapo mnatumalizia Bando
Kwa kweli Nimecheka na maneno yako. Mkuu ukweli wa habari ndio huo. Come what may...kukubali lazima tukubalikl kwamba JPM anayaishi anayoyasema.rafiki nunua internet bundle za Halotel hutalalamika hata ukitaka kuangalia full movie ya ufunguzi wa kampeni za El pale jangwani....
 
Bravooo Magufuli.
Wananchi tuko nyuma yako.... tunajua tutasikia mengi... lkn Watanzania tulio weeengi tuko nyuma yako.
 
Tatizo ni mfumo thabiti wa uongozi wa Nchi.Kama tunataka mfumo imara,katiba ya Jaji Warioba iliyokuwa imejaa maadili irudishwe na ya Sitta/Chenge iwekwe pembeni
 
Back
Top Bottom