Kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue: Siku 100 za Rais Magufuli

hivi ombeni sefue si alikuwa pia katibu mkuu kiongozi enzi za mkwere!!!! mbona hakuvuma???
 
Sijawah kupendezwa kabs na Rais wang Magufuli Mungu anisameh, nature yake tu hainibariki istoshe hajafanya makubwa kama inavyosemekana usanii mwng
wewe umeisha zoeya vya kunyonga vya kuchinja huviwezi
 
Magufuli na serikali yake hawataki kukosolewa. Mbona hamuyasemi haya? Ndiyo maana wanafinya na kubinya uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wake. Tumeona serikali ya JPM ikizuia TBC kurusha bunge live kwa visingizio vya kitoto. Tumeshudia serikali hii ikilifuta gazeti la Mawio bila sababu za msingi. Na ni jana tu kivuko cha Kigamboni kilipata hitilafu nusura kizame wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakazuiwa eti mpk wapate kibali toka TEMESA. Mbona Ombeni Sefue huyasemi haya?
JK alikuwa na mapungufu makubwa ya kiuongozi lkn aliruhusu watu waseme watakavyo, waandike watakavyo na vyombo vya habari vilikuwa na uhuru kuliko sasa. Ombeni yaseme na haya.

Nyie ndio mliozoea kutafuta mabaya tuuu ili tuone nchi yetu na uongozi wetu si chochote si lolote, mbona choo cha ofisini kwenu kichafu na vilevile ile bar unayokunywa mbona ujatueleza humu. Maendeleo ni hata kama umepigwa hatua moja mbele kwenye hicho kilichofanyika kuna watu wamefaidika kimaisha sio kwa sababu nyie mmeshawahi sehemu mbaya ndio uje utuletee negative perception yako hapa
 
Wewe kama ungeuziwa nyumba hizo ungeleta ujinga eako hapa? Waliopata wamepata wacha wivu.
Sasa mbona mnahangaika na majipu? Waliopata wamepata achen wivu wa kijinga. Mnawasumbua wazee wa watu kufagia hospital, oh mara sijui nani fisadi amepata wapi hela. Huo wote wivu. Waliopata wamepata. Je hiyo ndio maana yako?
 
12688187_1039643666100091_4265644989730337886_n.jpg
 
Huku kwetu mkuu wa mkoa kakiri kwamba kwa sera hii ya Magufuli ya elimu bure, Tanzania itaendelea kubaki mkiani kwenye viwango vya ubora wa elimu Afrika Mashariki na Kati.
 
Sisi watanzania tunaojitambua tunamhurumia sana kwa kitendo cha yeye na Chama chake kusigina demokrasia kule Zanzibar. Jumuiya ya kimataifa imemtega huyu mheshimiwa na usione ajabu baada ya miezi kadhaa yakamkuta yale ya Mzee Mugabe. Yetu macho.
 
ni mbwembwe tu. watanzania walikuwa wamoja bila kujali itikadi zao. leo kule zanzibar kuna mazombi kazi yao kupiga wapinzani. je hiyo ndo heshima?
 
Hivi kumbe sakata la Zanzibar limeanzia kwa JPM!!!!
Naona ukawa bado mna hang-over
 
upinzani hautakufa kwa uongozi huu labda atumie udikteta wa kukandamiza wapinzani kufanya mikutano kama walivyoanza.
 
upinzani hautakufa kwa uongozi huu labda atumie udikteta wa kukandamiza wapinzani kufanya mikutano kama walivyoanza.
Kimwili, upinzani ulishakufa August 2015 ( mlivyomteua EL kupeperusha bendera) na kuzikwa rasmi October 2015..
Ila spiritualy/kiroho bado tuko nao
 
*AFURAHIA JINSI ALIVYOFANIKIWA KUDHIBITI KIBURI CHA WENYE FEDHA.

*KUZUIWA KWA SAFARI ZA NJE KWAOKOA SH. BILIONI 7 KWA SIKU 100.

Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano John Magufuli ametaja mafanikio ya Serikali yake ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani na kwamba imethibitisha kuwa Serikali makini na imedhamiria kutekeleza ahadi zake kwa Mwananchi.
 

Attachments

  • IMG_20160213_075934.jpg
    IMG_20160213_075934.jpg
    276.5 KB · Views: 17
  • IMG_20160213_080439.jpg
    IMG_20160213_080439.jpg
    442.6 KB · Views: 16
Back
Top Bottom