Kutoka Ikulu: Baraza la Mawaziri kutangazwa J'tano (kesho)

Status
Not open for further replies.
Hata mimi sijamsoma kabsaa.
kama kuharibiwa angeharibiwa Anna Makinda ambaye alitajwa sana na hatimaye akapata uspika.

Jamani tujitahidi kusoma watu vizuri. Kuna watu wamemtaja Zitto kuwa ndiye atakayeteuiwa ma mkulu kuwa waziri kwa sababu ni maswahiba. Baadaye Invisible akasema mnawaharibia watu. Ukiunganisha habari jibu liko wazi, mnamharibia Zitto, kwani hadi mtu ataje waziwazi?
 
Press-Release.jpg

Kuna kitu gani hapa kipya ambacho wamesema kama sio umburukenge tu! Wanatumia muda mwingi kutaka Watanzania wamkubali rais Mwizi hakuna lolote bali hadithi za Pwagu na Pwaguzi. Wakitoa habari kunakuwa na maswali mengi kuliko majibu . Kinachowaogopesha ni wizi mkubwa walioufanya na siku si nyingi malipo yatakuwepo.
 
Jamani tujitahidi kusoma watu vizuri. Kuna watu wamemtaja Zitto kuwa ndiye atakayeteuiwa ma mkulu kuwa waziri kwa sababu ni maswahiba. Baadaye Invisible akasema mnawaharibia watu. Ukiunganisha habari jibu liko wazi, mnamharibia Zitto, kwani hadi mtu ataje waziwazi?
Kuna mtu kamtaja 'huyo' hapa? utafungwa wewe ala!
 
Mbona taarifa iko nyepesi? Hata jana la JK kaanza na small letter k badala ya K. Pia hawasemi ni muda gani litatangazwa.
 
Tusitegemee jipya.
Lazima JK alipe fadhila kwa Mafisadi na wote waliomsaidia kuchakachua kura. Unadhani ana uwezo wa kuwatema watu hawa bila kuwaingiza katika sehemu nyeti hali akijua kuwa wanajua na walisimamia mchezo mzima wa uchakachuaji wa kura?
These people knows too much to be ignored. They are too powerful to be neglected.

Tusubiri hiyo Kesho tuone.
 
Nina maswali mengi kichwani na sipati majibu. Naomba msaada wenu wana JF.

Hivi Zitto anastahisli kuaminiwa katika upinzani kweli? au ni mti wenye maembe na kila mmoja aupopoa mawe?

SIJUI NIAMINI TAARIFA ZA KUWA YEYE NI KIBARAKA AU NIENDELEE NA IMANI YANGU KWAKE?

Imani yangu ni kuwa Zitto anaweza kuwa kiongozi mzuri sana kwa taifa hili baadae, naamini kuwa wakati wa Freeman kuachia kiti cha uenyekiti chadema utakapofika, Zitto ama atakuwa mwenyekiti au katibu mkuu na pengine akasimamishwa na chadema kuwa mgombea wake wa Urais 2015 Sasa haya majungu si ya kumwaribia kweli hii future nzuri nayoiona juu yake huko mbele?
 
Taarifa toka ikulu imekuja baada ya kuona ofisi kuu inachelewa kutangaza baraza na hakuna maelezo ya msingi.

Ktk kukurupuka ndio hivyo tena hakuna objectivity ktk hiyo taarifa.

The good or rather bad thing ni kwamba effect ya baraza kwa maendeleo ya nchi hii by design si kiivyo on positive side.

Ni kama tunavyoona mpaka leo hakuna cha baraza lakini life goes on.

Ingekuwa ni chombo muhimu as purported to be lingekuwa zamani kazini pamoja michakato yote ya kuliunda!
 
Hawa jamaa wa ikulu pamoja JK naona wana wasiwasi sana hata kulifanyia tangazo editing hawawezi. Kweli ikulu kuna vilaza wengi, 'kikwete'! What a joke!
 
Uwezekano wa jipya kuwepo ni mkubwa... Najua wengine mtashtuka ikitokea mtu wa kambi ya upinzani ataingia katika baraza jipya

Kwa kuzingatia haja ya kuendeleza umoja wa Zanzibar na Muungano wa Tanzania, chama cha CUF wameombwa kupendekeza mtu mmoja atakeyeteuliwa katika cabinet.
Ndugu zetu wa Chadema wasitegemee chochote kwani wameyakataa matokeo na hawamtambui Kikwete kama raisi wao.
 
Kwa kuzingatia haja ya kuendeleza umoja wa Zanzibar na Muungano wa Tanzania, chama cha CUF wameombwa kupendekeza mtu mmoja atakeyeteuliwa katika cabinet.
Ndugu zetu wa Chadema wasitegemee chochote kwani wameyakataa matokeo na hawamtambui Kikwete kama raisi wao.

Hata wangeyakubali, wasingeambulia kitu. Ni CUF tu ndio watafaidika na huo uteuzi.
Labda wa CHADEMA wanaohitaji uteuzi wahamie NCCR kwanza.(Watu wataguna)
 
Kupeana limitation ya kuongoza miaka 10 pekee ndio impact yake hii sasa, ingekuwa kuna kipindi kingine kitafuata naamini kigugumizi kisingekuwepo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom