Kutoka Ikulu: Baraza la Mawaziri kutangazwa J'tano (kesho)

Status
Not open for further replies.
Uwezekano wa jipya kuwepo ni mkubwa... Najua wengine mtashtuka ikitokea mtu wa kambi ya upinzani ataingia katika baraza jipya

..sifa na tabia zifuatazo

-mjeuri
-si msikivu
-mpenda sifa binafsi
-hujikanganya na kutetea jambo hata kama anaona anaharibu
-kwa ufupi ni mtata
 
Uwezekano wa jipya kuwepo ni mkubwa... Najua wengine mtashtuka ikitokea mtu wa kambi ya upinzani ataingia katika baraza jipya

waambie kabisa ni Zitto Zubeir na si Mbowe mzee wa Gubu, mshikaji ana gubu yule!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hata mimi ninayo hiyo template ya barua za Directorate of Presidential Communications, naweza kuandika chochote nikadai imetoka Ikulu. Cha msingi ni hiki, imesainiwa na nani?
 
Mkuu,

Kwani kuna kifungu cha katiba kinachomzuia rais kutowachagua viongozi katika kambi ya upinzani kuwa mawaziri? Ningependa kukipata kifungu hicho

Katiba inazungumzia uteuzi wa Waziri Mkuu toka kwenye chama chenye wabunge wengi sidhani kama inamzuia kuteua upinzani. Hata hivyo yeye ni raisi kwa Idhini ya Chama Chake hawezi kufanya kitu tofauti bila ridhaa ya Kamati Kuu ya CCM akifanye hivyo yatamkuta yaliyompata Thabo Mbeki
 
Ila inaonekana mheshimiwa ana kigugumizi sana kutangaza!

Hapa ndipo muheshimiwa Rasi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete anatakiwa kuwaonyesha watanzania wote kwa ujumla karata zake alizochanga kuwaonyesha wananchi wake ni safu gani ya mashambulizi kwa kuutokomeza umaskini uliokidhiri na bila kusahau zile ahadi alizowaahidi wananchi endapo atapata fursa nyingine tena ya kuwaongoza watanzania na kuwapeleka kwenye ile nchi ya ahadi kwenye Maziwa na Asali!

Yetu macho hatumuombei ashindwe bali anatakiwa atumie busara sana kutuletea wawajibikaji kwenye utendaji bila kusahau kuutokomeza ufisadi na kuacha kupeana madaraka kiushikaji kisa eti yule ni mtu wangu wa karibu!

:teeth:
 
Press-Release.jpg

Hivi kumbe barua kwa ajili ya Press hazina hata signature!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom