Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

hakuna cha maana hapo,ni mbunge gani anaweza kumuuliza swali EL, zaidi ya wawili watatu tena kwa kumpongeza ktk kufanikisha kumaliza tatizo la umeme na kujenga shule nyingi kama ilani ya uchaguzi inavyosema.

Hakuna atakayethubutu kuuliza swali la ajabu ajabu toka sisiemu, maana anajua kuwa ataitwa kule kwenye vikao vayo vya siri na ataonywa na kupewa karipio kali.
Hawatathubutu! Sijaona mbunge yoyote mahiri wa sisiemu wa kumuuliza Lowassa maswali yenye mantiki kwa maendeleo ya taifa.
 
Swali la kwanza aulizwe kuwa zile mvua za Thailand alizotzngazia taifa ziko wapi?

Swali la pili , aulizwe yeye kama waziri mkuu analiambia taifa na bunge nini juu ya hali ya balali na mahali alipo?
 
Mambo ya Lowassa kuwekwa kitimoto tumeshayasikia kwa muda mrefu na hatukuwaona hao wabunge mabubu wa CCM wakimuweka kitimoto. Kwa hiyo hapo hakuna cha kitimoto wala kitijivu.
 
Kuna mtu kasema hapa kwamba wapelekewe maswali nadhani ana maana kwa njia ya mails.Nasikitika Wabunge walio wengi Bungeni wana akili ya kuiba kura na kushiriki uchafu tu lakini muda wa hata kuifunza kugusa keeyboard hawana .Labda wapigiwe simu wapelekewe barua kwa njia ya posta huko majimboni ambako pia hawakai .
 
Ripoti ya Richmond 'kuanikwa' leo

Na John Daniel, Dodoma

HATIMAYE hamu ya wabunge kutaka kuona na kujua wahusika katika mkataba wenye utata wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond itakidhiwa leo wakatakapokabidhiwa rasmi ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa Katika mkutano uliopita.

Habari za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali zilieleza kuwa hadi jana asubuhi, kazi ya kukamilisha ripoti hiyo ilikuwa ikiendelea na ilitarajiwa kumalizika jioni na kuwasilishwa mezani kwa Spika leo na baadaye kugawiwa kwa wawakilishi hao wa wananchi.

“Ripoti ile ni kubwa sana, si kama zile ambazo tulizoea kutoka kwa mawaziri (kauli za mawaziri), kuanzia wiki nzima inafanyiwa kazi ya maandalizi na leo (jana) ilikuwa kwenye hatua za kuwekwa majalada ili kesho (leo) wagawiwe wabunge,” kilisema chanzo chetu.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, hakukataa wala kukubali kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo na kusisitiza kuwa atatangaza kila kitu leo asubuhi.

“Nitatangaza kila kitu kesho (leo) saa nne asubuhi, kikubwa tu mtu wako asikose kuwapo,” alisisitiza Bw. sitta na kuomba mwandishi wa habari hizi kuvuta subira mpaka leo atakapoweka mambo hadharani.

Wakizungumza na Majira baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda majina yao yatajwe, walisema wao hawana taarifa hizo, ila wamepata matumaini mapya kama itakuwa hivyo, hasa baada ya Spika kusitisha ziara yake ya Marekani na kusisitiza kuwa ndicho walichokuwa wanasubiri kwa hamu.

“Ni wazi, kwamba hizo ni habari njema sana kwetu na kwa wananchi waliotutuma kuwasemea, lakini nakuhakikishia kuwa hatutamlinda mtu yeyote atayeonekana alishiriki kinyume na taratibu,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM.

Kuanzia juzi, vikao kadhaa vya wabunge wa CCM vilikuwa vikiendelea huku jambo kubwa ikidokezwa kuwa ni juhudi za kutaka kuweka mambo sawa, hasa baada ya joto zaidi kupanda, hata wabunge kugoma kujadili muswada wa umeme na biashara ya mafuta, hadi watakapopokea ripoti ya Richmond na kujua kilichomo.

Katika hali iliyoonekana kuwa si ya kawaida, kikao cha Kamati ya Uongozi ya CCM, pia kilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, ambapo ilidaiwa kuwa ajenda kuu ilikuwa ni kujipanga kwa ajili ya ripoti ya Richmond.

Awali akitoa matangazo baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Naibu Spika wa Bunge, Bi Anna Makinda, alisema kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM ambacho kilipangwa kufanyika jana sasa kitafanyika leo saa 2 usiku.

“Kwa hali ilivyokuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa ndicho chanzo cha kuahirishwa kwa kikao chetu leo (jana), kuna mambo ambayo yalikuwa hayajakaa sawa, hivyo ilibidi kwanza kiahirishwe mpaka hayo yakamilike kwanza,” kilisema chanzo chetu kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.

Habari zaidi zilieleza kuwa Kamati ya Uongozi ya chama hicho kilichofanyika juzi, kilihoji uwezekano wa wabunge wa CCM kukutana kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo na kwamba yaliyomo ni lazima yajadiliwe kwanza na wabunge hao kabla ya kutoa mawazo yao bungeni kesho.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwasili mjini hapa kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri huku kukiwa na taarifa kwamba baada ya kikao hicho, kutakuwa na jambo jipya linaloweza kuleta mabadiliko makubwa katika siasa na uongozi wa nchi.

SOURCE: MAJIRA
 
I hope na sisi JF tutapata Copy ya ripoti juu ya RICHMONDULI...

Mungu ibariki Tanzania
 
Mods unganisha hizi . Shukuru uwe unasoma kabla ya ku post kuna mada nyingi zinafanana na hili all you need to do is just under the previous kama vile una weka post ya kuchangia bado tutaisoma
 
mheshimiwa Moderator, kwa heshima na taazima napenda kujiunga nanyi wote katika blog yako hii. Mii ni msomaji mzuri wa hii blog na kweli ni mengi tumejifunza huku kuhusu ufisadi unaoendela huko nyumbani. Naomba niwakilishe hija yangu binafsi leoo hii ikiwa historia imewekwa, au itawekwa huko nyumbani tanzania, basi ni maombi yangu zitengenezwe DVD/video za kikao cha leo Bungeni na ziuzwe na tuombe hizo proceed zitumike kutunisha website yetuu hii. Wadau naomba maoni yenu kwa hili kwani Historia inatimia leo hii.
 
Mimi nakuunga mkono 100%,leo ni kama tanzania imenacheza world cup 2010,fainal na Italy
 
Mwanakijiji hilila DVD wewe unasemaje. Tunaomba urushe matangazo na kule kwa michuzi kuna watu wengi sana wanahitaji kujua hii historia inayoendela kutokea huko nyumbani.
 
mheshimiwa Moderator, kwa heshima na taazima napenda kujiunga nanyi wote katika blog yako hii. Mii ni msomaji mzuri wa hii blog na kweli ni mengi tumejifunza huku kuhusu ufisadi unaoendela huko nyumbani. Naomba niwakilishe hija yangu binafsi leoo hii ikiwa historia imewekwa, au itawekwa huko nyumbani tanzania, basi ni maombi yangu zitengenezwe DVD/video za kikao cha leo Bungeni na ziuzwe na tuombe hizo proceed zitumike kutunisha website yetuu hii. Wadau naomba maoni yenu kwa hili kwani Historia inatimia leo hii.

Hili ni wazo zuri sana. Siku ya leo ni kielelezo cha uwezo wa sauti ya uma kuleta mageuzi katika muelekea wa kiuchumi, siasa, na utamaduni wa Taifa. Kuna sehemu nyingi sana matatizo kama haya ya Richmond yameleta maafa na vita. Lakini tunajivunia Tanzania yetu ilivyokomaa kisiasa na kuitikia mwito na kilio cha wanyonge.

Hii inaleta heshima kwa Bunge, heshima kwa vyombo vya serikali, heshima kwa wananchi, na heshima kwa hii kada ya siasa pia. Imekuwa kwenye vichwa vya watu wengi sana kufikiri kwamba kuwa mwanasiasa ni ulaji na utajiri wa short cut.

Siasa, uongozi, na dhamana tunazopewa na wananchi ni vitu vitakatifu.

Nafikiri wazo la DVDs / Video ni zuri sana sababu litafanya jambo hili liwe ni kumbukumbu ya vizazi vijavyo na mafunzo kwa wanaojifunza mambo mbalimbali ya kijamii. Si tukio la kusahauliwa kabisa.
 
Mbunge wa upinzani aibua kashfa nyingine nzito bungeni kuhusu ukimwi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Karatu (Chadema), Dk Willibroad Slaa, ameibua kashfa nyingine inayomhusisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu, kwamba hospitali yake ilihusika kufanya utafiti wa dawa za ugonjwa wa Ukimwi iliyotengenezwa Afrika Kusini, licha ya serikali kuzuia utafiti huo.


Bila kutaja jina la IGP huyo aliyehusika katika sakata hilo, Dk Slaa alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu suala hilo na chombo kilichohusika kutoa kibali cha majaribio hayo kufanyika Hosptiali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo na kuhusisha Watanzania 64.


Naibu Waziri wa Afya, Dk Aisha Kigoda katika jibu lake alisema hakuna taasisi yoyote ya serikali iliyowahi kutoa kibali cha kufanya utafiti wa dawa za Ukimwi kutoka Afrika Kusini.


Dk Kigoda alisema, kumbukumbu zinaonyesha ombi la kibali cha kufanya utafiti liliwasilishwa NIMR mwaka 2000, lakini baada ya tathmini serikali ilikataa ombi hilo kutokanana maombi ya utafiti huo kuwa na upungufu mkubwa wa sayansi na maadili.


Alisema utafiti huo umefanywa kinyume cha taratibu za utafiti kwa sababu sio serikali wala Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Tume ya Sayansi na Teknolojia (CoSTECH) waliohusika na utoaji wa kibali cha utafiti huo.


Hata hivyo, Dk Kigoda alisema kwa sasa serikali imesimamisha utafiti huo, kuzuia uingizaji dawa pia kuzirejesha Afrika Kusini.


Alisema suala hilo ni kosa la jinai na kwamba, wananchi wana haki kufuata mkondo wa sheria kudai fidia kwa kuhusishwa na utafiti huo ambao hauna baraza za serikali.


Hata hivyo, Waziri Kigoda alisema baada ya serikali kufanya mazungumzo na viongozi wa JWTZ, taarifa zilionyesha kukataa kuhusika na kuwezesha kufanyika kwa utafiti huo.


Naibu Waziri huyo alisema, wizara yake inajitahidi kuongeza uwezo wa TDFA na NIMR,

kuchunguza tafiti mbalimbali zinazofanywa nchini kuhusiana na dawa na magonjwa ili

kuhakikisha zinafanywa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.


Tuma maoni kwa Mhariri
 
Mahita mbali na ujambazi wa silaha kumbe na hata ujambazi wa deals alikuwa yumo ?
 
Hii ni kitu ya zamani kidogo. Nashangaa inaibuka sasa hivi. Suala hili pia lilimtia matatani Thabo Mbeki mwaka ikisemekana kuwa alikuwa na ubia katika utengenezaji wa dawa hii.
Soma hapo chini:

[Virodene, a dosage form of the industrial solvent dimethylformamide
(DMF), has been hotly debated in South Africa some years ago. The
SA DRA refused to approve clinical trial proposals. Apparently the researchers moved their trials to Tanzania, where they have now been asked to leave as the trials did not have correct approvals.
The SA Mail and Guardian noted that SA Health Minister
Tshabalala-Msimang actually visited the clinic in Tanzania where the trials were taking place...
Any Tanzanian E-drugger who can tell us more what happened?
From: Kaiser Daily HIV/AIDS Report - Sat, 8 Sep 2001; M&G website
www.mg.co.za Copied as fair use. NN]

--
Tanzania to Expel Two South Africans For Importing 'Controversial'
AIDS Drug

The Tanzanian government has ordered two South Africans, charged with illegally importing the "controversial" AIDS drug Virodene PO 58 and
four other drugs, to leave the country by Saturday, the Dar es Salaam
Daily News reports. According to Tomric News Agency/AllAfrica.com,
Jacques Siegfried Visser and Khamalo Bafana are employed by Virodene Pharmaceutical Limited of South Africa, which has been conducting "disputed" clinical trials of Virodene PO 58 at the Lugalo Military Hospital in Dar es Salaam without the approval of the National Institute for Medical Research. The two South Africans were arrested in July, and Pharmacy Board inspectors confiscated and impounded all documents relating to the drugs, as well as any remaining batches of PO 58, which was banned in South Africa in 1997. The drug has failed to prove effective in clinical tests in Great Britain and Germany,
where it was determined that the drug was a derivative of the industrial solvent dimethylformamide (DMF), a finding that was met with
"widespread public outcry" in Tanzania (Tomric News Agency/ All Africa.com, 9/5). Visser maintained that institute approval was not necessary because his group had "worked closely" with the Tanzanian military and police to test the drug on 64 HIV patients. He added that the trial, held in Dar es Salaam between September 2000 and March 2001, was "properly approved" and "conducted with the highest ethical standards" (Kaiser Daily HIV/AIDS Report, 8/15). According to Tomric News Agency/AllAfrica.com, after failing to win approval for
PO 58, Virodene also imported the drugs PO 59, PO 60, PO 61 and PO 62, none of which were registered with the Tanzanian Pharmacy Board
(Tomric News Agency/AllAfrica.com, 9/5).

----
SA Aids quacks given the boot

JUSTIN ARENSTEIN, ONGERI JOHN, Nelspruit | Friday

THE Tanzanian government this week ordered the deportation of
two South Africans accused of secretly testing a discredited
anti-Aids drug on human guinea pigs.
Tanzania's Ministry of Home Affairs said on Wednesday that
Jacques Zigi Visser and Themba Khumalo appeared to have
conducted illegal medical trials with various versions of the
controversial Virodene drug on patients at Lugalo military hospital in Dar es Salaam.
Virodene's active ingredient is a highly toxic industrial solvent,dimethyl formamide (DMF), which has been banned for human
use in South Africa and elsewhere due to dangerous side effects.
Medical researchers writing in the journal Aids Research and
Human Retroviruses in 1997 also warn that DMF might actually
activate HIV.
Four years ago the African National Congress was seriously
embarrassed when its close links with Visser and his ex-wife,
Olga Visser, the "inventor" of the drug, emerged publicly.
Tanzania's home affairs permanent secretary Bernard Mchomvu
said on Wednesday the country's National Institute for Medical
Research (NIMR) never gave permission for the tests at Lugalo
and a second private clinic owned by the country's inspector
general of police, Omar Mahita.
Mchomvu said none of the Virodene formulas used in the trials
had been registered with Tanzania's Pharmacy Board. "And
finally, neither of the South Africans has a legal immigration
status in Tanzania. Their visas and permits have all expired. They have therefore been ordered to leave the country by Saturday, or face deportation."
The deportation order is not the first clash with Tanzanian
authorities for either Visser or Khumalo.
They were arrested for allegedly illegally importing the PO58,
PO59, PO60, PO61 and PO62 versions of Virodene to Tanzania
in July last year after the NIMR refused permission for human
testing of PO58. Quantities of all five versions of the drug were
confiscated during a raid on Viro- dene Pharmaceutical Holdings
(VPH) offices by health ministry inspectors in Tanzania's central
Shinyanga region.
Inspectors also seized a consignment of Oxyhumate drugs at Dar
es Salaam International airport shortly afterwards, including a
carton marked for a Dr Balele at the Lugalo hospital. The
consignment was marked as being imported by the Tanzania
chief of defence forces, sparking an ongoing investigation into the
trials.
VPH is a South African-registered company set up to develop and
market a commercial version of Virodene as an anti-Aids
medication. The compound was patented as an anti-Aids drug by
medical technician Olga Visser after she stumbled on it while
working on freezing animal organs for medical research. Virodene
has, however, not yet been approved for use by any regulatory
authority in the world.
An attempt to fast-track its approval and registration by the
Medical Control Council (MCC) in South Africa in 1997 unleashed
a political storm after the then health minister, Nkosazana
Dlamini-Zuma, gave the bid her public support, organised a
special presentation to the Cabinet and lobbied the issue in
Parliament despite MCC concerns about Virodene's safety.
The controversy forced Thabo Mbeki, who was deputy president
at the time, to publicly deny that the African National Congress or its leadership were funding or otherwise commercially involved
with Virodene.
Dlamini-Zuma continued to meet with VPH officials, however, and
her successor, Dr Manto Tshabalala-Msimang, recently visited
the Tanzanian clinic where Virodene trials are being conducted.
Tshabalala-Msimang's spokesperson Jo-Anne Collinge insisted at
the time that the visit was part of an official tour of Tanzania and
the link with Virodene purely coincidental.
Olga Visser, who remains a close business partner, insisted on
Wednesday that Virodene continued to enjoy the highest political
support both in South Africa and Tanzania.
She also dismissed the Tanzanian deportation order as "rubbish"
and "mischief by someone with an agenda".
"I met with Tanzania's inspector general of police two days ago,
and both Themba and Zigi met with senior officials today. Nothing
has been said about deportations. There was some trouble with
the NIMR a while ago, but that has been sorted out," she said.
Visser has previously insisted that NIMR approval was not
necessary because all trials were in military or police hospitals.
Mchomvu insisted, however, that both Khumalo and Visser were
in Tanzania illegally after their visas expired. Khumalo's
exemption certificate issued for South African pass-port number
4247-303-94 expired last Friday, while Visser's visa in South
African passport number 4041-888-52 expired on June 21.
"All the relevant authorities, including the health, defence and
national service ministries, and the State House have reviewed
this matter. The order to leave Tanzania stands," said Mchomvu.
VPH has, meanwhile, conducted initial tests on Virodene in the
United Kingdom, the Czech Republic and Germany but has yet to
release the results.
Court papers from a bitter ownership and patent dispute between
VPH shareholders indicate that the company had attempted to
sell the drug in Portugal, Ghana, Kenya and Mozambique.
Shareholders are also demanding to know exactly who is funding
the trials and who the "secret" majority shareholder is after VPH
agreed to sell a stake in the patent rights to former Umkhonto
weSizwe cadre Ngelezi Zaccheus Mngomezulu for R5-million.
"The money was never transferred, but the Vissers are being
funded by someone and must have spent at least R10-million on
these recent trials," said disgruntled shareholder Charles Fourie.
"In fact, Zigi called me from Tanzania just two weeks ago to offer to buy us all out for $5-million (R42,5-million)."
Both Visser and Khumalo were unavailable this week.
South African foreign affairs deputy director for Tanzania, Adriaan Smuts, confirmed that he had received "vague" reports on the deportation.
"Our high commissioner Theresa Solomon spoke briefly with
Khumalo on Wednesday and asked for clarification, but he has
failed to revert to us. We have therefore put an official on the
matter," said Smuts. - African Eye News Service
 
Dawa yenyewe inaitwa Virodene, basically it is an industrial chemical. Waliwatumia watanzania kama guinea pig pale Lugalo.
 
Ina maana kazi kubwa ya Dk Slaa bungeni ni kuibua kashfa tu? Kila mara akiongea ni hadithi ile ile ya kuibua kashfa!
 
kwanini heading isingeandkwa Dr. Slaa aibua kashfa nyingine?
Four years ago the African National Congress was seriously embarrassed when its close links with Visser and his ex-wife, Olga Visser, the "inventor" of the drug, emerged publicly.Tanzania's home affairs permanent secretary Bernard Mchomvu said on Wednesday the country's National Institute for Medical
Research (NIMR) never gave permission for the tests at Lugalo and a second private clinic owned by the country's inspector general of police, Omar Mahita.

Haya ndio majibu ya Muuguzi Aisha Kigoda,siyo dr. kwanini waandishi wanaendelea kumpa ujiko??

Naibu Waziri wa Afya, Dk Aisha Kigoda katika jibu lake alisema hakuna taasisi yoyote ya serikali iliyowahi kutoa kibali cha kufanya utafiti wa dawa za Ukimwi kutoka Afrika Kusini.Dk Kigoda alisema, kumbukumbu zinaonyesha ombi la kibali cha kufanya utafiti liliwasilishwa NIMR mwaka 2000, lakini baada ya tathmini serikali ilikataa ombi hilo kutokanana maombi ya utafiti huo kuwa na upungufu mkubwa wa sayansi na maadili.

Alisema utafiti huo umefanywa kinyume cha taratibu za utafiti kwa sababu sio serikali wala Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Tume ya Sayansi na Teknolojia (CoSTECH) waliohusika na utoaji wa kibali cha utafiti huo.
 
Tatizo mojawapo ni kuwa ethical boards zetu haziko coordinated. Tuna institutional ethical boards e.g. NIMR, COSTECH, MUHAS lakini hakuna oversight.
 
Back
Top Bottom