Kutoa "Lifti" - An Act of "Generosity" of "Fame"

Obuntu

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
510
34
Habari ya Jumapili?

Siku moja moja Obuntu hufanya maamuzi ya kutembea kutoka Mabagala Rangi Tatu (anakoishi) hadi Mbagala mission (Saint Anthony) : Kama sehemu ya kunyoosha vioungo na pia kuangalia mitaa ambayo "magari hayafiki"!

Mara kwa mara hukutana na "marafiki" wenye "usafiri" ambao baada ya kusalimiana hupenda sana kumuuliza hili swali "vipi: nikuzogeze kidogo"? au "naenda mjini vipi nikupe "lifti"? e.t.c

Ningependa kuuliza:

- Hivi ni lazima kila "mwananchi" anayetembea kwa miguu hana gari?
- Hivi kuna upungufu gani mtu anapoamua kutembe-tembea mtaani kwa miguu kwa sababu zake mwenyewe?
- Hivi ni lazima huu "utoaji wa lift" ni ishara ya "ukarimu" au "kuonyesha umaarufu"?

Siku Njema
 
Labda wanakuona umeelekea "kigarigari", yaani unayo gari lakini imepata matatizo na unakwenda kutafuta msaada. Pengine hata hiyo tembea yako ni ya shida ndiyo maana unaulizwa lifti.

Ila wewe usijaribu kutoa lifti kwa mtu usiyemjua, wafanyakazi wenzangu wawili wamechomolewa laptop zao kwenye gari baada ya kuwapa lifti watu wasiowafahamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom