Kutembea na mke wa mtu ni mbaya ndugu zangu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Athari unazoweza kuzipata ukiwa katika uhusiano na mke/mume wa mtu.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa watu kutoka na wake/waume za watu. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake. Bila aibu huku akijua kuwa mwanaume aliyenaye ni mume wa mtu anatembea naye. Wengine wanatamba kwamba wao ni washindi.

Kwamba wake zao hawana lolote, ndiyo maana wakakimbilia nje na kufanikiwa kuwanasa. Hizi ni tambo za kijinga. Hakuna usahihi wowote wa mtu kutembea na ‘mali’ za watu.
Je, wewe unayesoma mada hii ukoje? Ni mke wa mtu lakini una mwanaume mwingine wa pembeni? Ni mume wa mtu, lakini una kimada wako wa nje? Kuna mke wa mtu anakutega kimapenzi au mume wa mtu anakusumbua akikutaka?


Uko kundi gani? Kujua ulipo, angalau kutakupa nafasi ya kuingia katika kipengele cha pili, ambacho ni kujifunza juu ya yote hayo. Rafiki zangu, najua kuna baadhi yenu hampendi ninachokiandika hapa lakini ni tatizo kubwa kwa wengine.
Ikiwa utaweka ubongo wako tayari kujifunza, kuna kitu utakipata kupitia mada hii. Zipo athari unazoweza kuzipata ukiwa katika uhusiano na mke/mume wa mtu.


UNAPOTEZA MALENGO


Kwanza kabisa, hakuna malengo unayoweza kutengeneza na mke au mume wa mtu. Tayari mwenzako yupo kwenye ndoa yake, kwa hiyo kuwa naye hakuwezi kubadilisha matokeo (hasa kama ana ndoa ya mke mmoja).
Sana sana unapoteza muda wako na kuziba bahati ya kuingia katika ndoa yako peke yako. Huwezi kuwa na malengo yoyote kwa kuwa katika uhusiano na mtu mwenye ndoa yake.
 
sasa kama alikua my first love and we are better together kuliko mmewe au mke wangu ila kwasababu ya ukatoliki hatuwezi kutengana?
 
Kwani nani mwanzilishi Wa mahusiano.. Nadhani ni mtongozaji.. Sasa hoja ya Mapenzi hapo inategemea nguvu ya tongozo .. Si kila Mwanaume anayetongoza Mke Wa Mtu anakubaliwa.. Kwa ivo Kusema mwanamke anajidai mshindi kubeba Mume Wa Mtu nadhani si sahihi sana coz yeye si mtongoza..

Lakini watu tunashambulia sana Mtoko Wa Mume-mtu _ mkwaju_ Mke-Mtu , hawara and other sort of this kind, Na kubatizana majina ya kijehanam kila kukicha.. But hatufikirii why Mtu atoke nje ya NDOA ?? Why ofisi zinageuka madanguro muda Wa hitimisho la Kazi..? Lipo tatizo.. Kusema tu ni uhuni, umalaya sidhani Kama ndo mwarobaini Wa tatizo..

Something Mapenzi Kwa wanandoa hakipo .. Mimi niseme nikijuacho ukinipinga weka hoja yako , kiini Cha mambo ya Posta mpya ni wanawake.. Wanasema chanzo Cha mabadiliko familiani ni Mwanaume SI KWELI.. Mabadiliko ni mwanamke sure I tell..

Unajua Mwanaume ni Ngumu sana kuoa.. Mara nyingi mawazo ya NDOA yanashinikizwa Na wanawake.. Wanaume wengi kabla ya NDOA wanawazia maisha .. Kupenda Mwanamke ni sehemu tu ya kukidhi matamanio lakini si utayari Wa kuoa.. Tofauti Na wanawake ambao kabla ya NDOA wao hawawazii sana maisha but kuolewa.. So akipata Mwanaume mdada Wa watu atajikokotoa, kujinajihisha Kwenye kila kitu amfurahishe Mkaka husika Na kimwaga miushawishi mingi wafunge ndoa fasta, Na Kwa sababu ya umbwe la Mapenzi Mkaka analofaidi kutoka Kwa Mpenzi wake huanzisha vuguvugu la NDOA ..

But baada ya NDOA mdada hujihisi amefika.. Amepata Taji aliyoisotea..mambo ya honey, love, MSG motomoto, mabusu Na hasa masuala ya mduara huanza kupungua kasi .. Mwanamke huwazia maisha Sasa Na kujisahau kabisa maeneo ya Ujenzi wa house la NDOA .. Mara nyingi maneno yake hugeuka ' tununue kiwanja', 'tununue thamani Za ndani', tuanzishe biashara hii au ile' , of which is true as far life is concern but Kwa mwanaume hugeuka kero.. Hasahasa nyakati Za mduara utamsikia mtu ' Leo sijiskii vipi ule mpango wa kununua kiwanja umefikia wapi' anakata topic Na kuzua nyingine..

Vijikero this way hufikia maturity yake wakipata Mtoto , Nara nguo, Shule Na mengi ambayo kweli ni wajibu Wa kifamilia but inakuja Kama kero.. Mduara unafanyika ilimradi no love at all.. Sababu hizi Mimi ndio nadhani ni vyanzo vikuu vya Mtu kutafuta farijio somewhere outside..

Sidhani Kama kuna shibe ya nguvu ndani Mtu atatafutia Nini makombo ya nje, makombo yenyewe hatari, TANESCO wako nje nje, Na watoto wao akina ngiri, kaswende, visonono.. But Mtu mwenye kiu ya Penzi ni kipofu kwenye hatari hizi..

Mie naona wanandoa ni nafasi tu ya kujiuliza kabla ya kuoana au Mwanzo Wa NDOA Na Leo hii zoezi letu limepata hitilafu gani .. Sometimes wanandoa wameumizana to an extend ya kupeana madonda ya kutosameheana.. Kila anayemsaliti mumewe au mkewe kuna kakisasi analipizia.. Hako ndio kiini ..

Anyway MWAMUZI Niishie hapo..

(mtoa maoni ni mwamuzi Wa kizazi kipya yuko huru kumpigia cm +255713254210 au SMS )
 
Shida unaweza ukajibana usitembee na mke wa mtu,
But kuna mtu anatembea na mkeo, imekaaje hii??
Kumbuka huyo mke wa mtu humbaki, mnakubaliana tu, na pengine hujui kama ana mumewe.
Huyo mke wa mtu angekua anatimiziwa kila kitu na mumewe angekuja kwako?

Somo hapa ni kua wakati tunajibana tusitembee na wake za watu, same time tuangalie nini tunawanyia au kuwakosesha wake zetu ili nao wasitembee nje.
 
kwa mtazamo wangu kuna mambo umeacha, chekecha kichwa halafu utuongezee darasa
 
MUNGU akutie nguvu kwa ajili ya mada hii, hakika imenigusa saaaaaannaaaa, be blessed man ila usiniulize sababu
 
ni kweli kabisha Sharks, watu wamesahau mno wajibu wao, na gadget zimechukua nafasi na ndio maana mama wengi wanahangaika ofisi asipofwata atatumia nguvu kuforce uhusiano
 
Mimi ninaowasikitikia zaidi ni wanawake wanaotembea na waume za watu. Kama kuna namna ya kujidharaulisha na kujidhalilisha ni kwa mwanamke kutembea na mume wa mtu. Hii ni dhahiri amejiweka ktk kundi la viruka njia kwani tayari anajua kuwa hakuna future hapo lkn bado anavua nguo yake.

Wengine ni wanawake walioko kwenye ndoa na still wanavuliwavuliwa nguo nje ya ndoa. Ukiona mwanaume anakutongoza ilhali akijua umeolewa, hiyo si dalili kuwa anakupenda bali anakudharau.

Anakudharau kwa misingi kwamba alipaswa kukuogopa kwa hilo lakini kwa kuwa una mazoea ya kujirahisisha kwa wanaume kwa kuchekacheka na kujipitisha, ameona INAWEZEKANA na INAFAA kukushawishi kufanya umalaya kwani unafanana nao.

Wanaume wenzangu tutakubaliana kuwa wapo wanawake ambao kwa jinsi wanavyojiweka na kujichukulia, sisi wanaume hujiuliza mara 8 kabla ya kuwataka. LKN pia wapo wanawake ambao ukimuona leo kesho unamtongoza kwa jinsi alivyo na mapepe.

Kwenu wanawake msio na akili: Kutongozwa na jirani ni dhalili na unapaswa kumchukia kwa kitendo chake cha kukutongoza ilhali anajua una mume na anamjua. Jiulize mpaka kakutongoza, KAKUONAJE? ANAKUCHUKULIAJE? NINI KIPIMO CHA HESHIMA YAKO KWAKE?

Heshima kwako mkuu MziziMkavu, hii mada ni muhimu kwa kizazi hiki kichafu cha maadili.
 
Last edited by a moderator:
Cha muhimu ni kujiuliza kwanini utembee nje ya ndoa,inabidi wanandoa kukaa chini kusolve tatizo na si kuongeza tatizo.
 
Vipi kama 'mume wa A' anatembea na 'mke wa B' halafu "A" nae anatembea na "B" (yaani couple mbili zina cross!)?
 
Back
Top Bottom