Kusudio la kuifikisha TANESCO katika vyombo vya sheria

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,903
Nadhani muda umefika tufikishane kwenye vyombo vya sheria.

Hii migao ya umeme haijaanza leo. Hili tatizo lipo kila mwaka na sababu zinazotolewaga ni zile zile. Kusudio langu halihusu kuhoji uhalali wa mgao bali taratibu zinazotumika kuendesha mgao wenyewe.

Hatua hii itajikita kuwahoji na kuwataka TANESCO watoe ufafanuzi ni hatua gani za makusudi wanachukua kuhakikisha wanapunguza madhara ya mgao kwa watumiaji. Nahisi hili halijawahi kufanyiwa kazi ipasavyo.

Kwa mfano, nataka kuwahoji kwa nini maeneo ya makazi wanaacha umeme wakati mwingine siku nzima halafu wanakuja kukata mida ya usiku? Usiku kuna karaha za joto na giza, tofauti na mchana. Kwa nini mgao usijikite tu mida ya asubuhi-jioni. Kwa mchana hata wakikata kila siku masaa 6 kwa siku, wakibadili (saa 12 asubuhi-6 mchana) na (saa 6 mchana-12 jioni) zoezi halitakuwa karaha kama ilivyo hivi sasa.

Pia kwa nini hawatoi ratiba rasmi ya mgao? Ratiba inasaidia mtu au biashara kupanga shughuli zako ipasavyo.

Mahakama na vyombo vingine vya sheria inabidi iwalazimishe TANESCO kutengeneze mwongozo rasmi wa taratibu rafiki watakazokuwa wanazitumia katika migao maana sitegemeo kama huu utakuwa mgao wa mwisho.
 
Umeme uwake mchn kwakuw kuna shughuli nyingi za kiuchumi kulko ucku
 
Ni wazo zuri, lakini wanaowajibika kupatikana kwa umeme wako juu ya Sheria, hivyo mahakama hazina nguvu dhidi yao. Hata kama mahakams ikitoa maagizo, hawatatekeleza.
 
Mahakamani utaenda kuangukia pua tuu ndugu. Hoja zako zitajibiwa kirahisi, alafu itaishia hapo bila hatua yoyote ile.

Nchi bila kuwa na msukumo wa kisiasa hakuna litakalo fanyika. Serikali hii haina tabia ya kuheshimu mahakama... sana sana utakuta hukumu za mahakama zinaogopa mihimili mingine badala ya kuzingatia haki.

Kwa nchi hii tulipofikia wananchi tuamke... tupeleke watu imara bungeni. Wanaoweza kuihoji na kuisimamia na kuikemea serikali na wakasikilizwa. Siioni hili kwa bunge la sasa.

Bunge lilikuwa na wajibu kuhoji haya kwa niaba ya wananchi na kudai kupatiwa majibu na maelezo ya kutosha. Badala yake wapo tuu kimya siku zinaenda.

Sijajua kama unapoenda kuomba kufungiwa umeme, kuna kipengele kinachohusu SLA, ambazo tanesko wanapaswa kuzifuata... hizo ndio unaweza kwenda kuwadai mahakamani... kwa mfano kama walipaswa kuhakikisha huduma zinapatika kwa si chini ya asilimia 97% chini ya hapo wanawajibika either kwa kulipa fidia or penalties etc..

Ila kila la kheri unaweza kujaribu tuu... ila Andra hoja nzito vizuri.
 
Bado hamtaki kunisapoti katika azma yangu hii?

Watanzania wameathirika na kile kinachoitwa "Stockholm Syndrome". Mmechukuliwa mateka na mfumo dhalimu unaowanyanyasa na kuwatesa lakini badala ya kuchukua hatua mmebaki kumuonea huruma mdhalimu wenu.
 
Back
Top Bottom