Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 10,783
- 18,683
Wanajamvi habarini, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake wa pekee, mimi ni mhitimu wa chuo ngazi ya shahada mwaka huu, yaani mwezi july 2016. kwa muelekeo uliopo ajira za serikalini zinaonekana kuyeyuka hali hii imenigeuza fikra zangu na kuchukia ajira za serikalini hasa ualimu niliosomea ambapo hata hadhi ya mwalimu ni ya chini sana,
Nimetokea kujiamini sana na kufungua ukurasa mpya wa fikra na kuuweka pembeni utumwa wa fikra tegemezi za kulilia kipato cha laki tano kwa mwezi na ambapo hata hivyo unaweza kupelekwa mazingira yasiyo mazuri kuanzia miundombinu hadi kibiashara.
Naamini maamuzi haya sitajutia kwani kuendelea kuwaza ajira ambazo hazieleweki ni kupoteza mda wa kufanya mambo mengine yenye kuleta tija. wahitimu wenzangu na vijana wenzangu tubadilini mawazo badala ya kuwaza kuajiriwa na serikali tuwaze kujiajiri wenyewe ili tuepukane na utumwa na dharau hizi za kuzungushwazungushwa mara tutaajiri walimu 35000 mara 24000.
Tufahamu kuwa hakuna tajiri aliefanikiwa kwa kutegemea mshahara pekee, lets make business