Kusubiri ajira za serikali ni michosho tuu

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,766
18,620
Wanajamvi habarini, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake wa pekee, mimi ni mhitimu wa chuo ngazi ya shahada mwaka huu, yaani mwezi july 2016. kwa muelekeo uliopo ajira za serikalini zinaonekana kuyeyuka hali hii imenigeuza fikra zangu na kuchukia ajira za serikalini hasa ualimu niliosomea ambapo hata hadhi ya mwalimu ni ya chini sana,

Nimetokea kujiamini sana na kufungua ukurasa mpya wa fikra na kuuweka pembeni utumwa wa fikra tegemezi za kulilia kipato cha laki tano kwa mwezi na ambapo hata hivyo unaweza kupelekwa mazingira yasiyo mazuri kuanzia miundombinu hadi kibiashara.

Naamini maamuzi haya sitajutia kwani kuendelea kuwaza ajira ambazo hazieleweki ni kupoteza mda wa kufanya mambo mengine yenye kuleta tija. wahitimu wenzangu na vijana wenzangu tubadilini mawazo badala ya kuwaza kuajiriwa na serikali tuwaze kujiajiri wenyewe ili tuepukane na utumwa na dharau hizi za kuzungushwazungushwa mara tutaajiri walimu 35000 mara 24000.

Tufahamu kuwa hakuna tajiri aliefanikiwa kwa kutegemea mshahara pekee, lets make business
 
Ukishaweka hayo maneno kwenye vitendo ndio nitakuja kutoa neno

Wengi tulishafikiria the same same thing na katika mazingira hayo hayo (umebadili gia baada ya ajira kucheleweshwa)

Haya huo uamuzi wako ubadilishe kwenda kwenye vitendo
 
Enhee hapo Mimi nakuita jembe kimsingi kaza buti si unajua kila kitu mwanzoni kinakua kigumu??!
 
Ndugu nahisi umekosea, 24000 siyo waalimu pekee yake watakao ajiriwa na watumishi wengine. Taarifa niliyopata mimi ni kuwa katika ajira zinazotarajiwa kutolewa wiki ijayo zinajumuisha waalimu wa sayansi, madaktari, wauguzi na wataalamu wa maabara tu.
 
Ukishaweka hayo maneno kwenye vitendo ndio nitakuja kutoa neno

Wengi tulishafikiria the same same thing na katika mazingira hayo hayo (umebadili gia baada ya ajira kucheleweshwa)

Haya huo uamuzi wako ubadilishe kwenda kwenye vitendo
kiukweli nimebadili gia angani baada ya kuona ajira hazisomeki, sioni ubaya kwani lazima ubadilike kulingana na hali husika ( when you pour water into a cup it becomes a cup..when you pour it into a jug it takes the shape of the jug...water finds the way of its own..be like water my friend..BLUCE LEE)
 
Ndugu nahisi umekosea, 24000 siyo waalimu pekee yake watakao ajiriwa na watumishi wengine. Taarifa niliyopata mimi ni kuwa katika ajira zinazotarajiwa kutolewa wiki ijayo zinajumuisha waalimu wa sayansi, madaktari, wauguzi na wataalamu wa maabara tu.
yeah nlimaanisha ajira zote, sasa ukiangalia hapo mkuu walimu pekee waiohitimu mwaka jana ni wengi kuliko hata hizo ajira
 
yeah nlimaanisha ajira zote, sasa ukiangalia hapo mkuu walimu pekee waiohitimu mwaka jana ni wengi kuliko hata hizo ajira
Kumbe ni wengi kuliko idadi wanaotaka kuajiriwa basi ni majanga mwaka huu. Lazima kuwa na Alternative nyingine bora wengesema mapema
 
Back
Top Bottom