Kusoma sio kazi, kazi kuigeuza elimu kuwa pesa

Hapa namaanisha kwamba,kupata elimu sio kazi,kazi kwamba je elimu ulioipata inakusaidia maisha yako?maana huwezi saidia jamii kama maisha yako yanakushinda.
 
Hii ni mada ambayo kila mmoja atafikiri kulingana na ubora wa elimu aliyonayo. Lakini tukumbuke kwamba jamii na dunia kwa ujumla inaendeshwa na maamuzi atakayofanya kila mmoja.

"The purpose of education is to make a world a better place". Thamani ya pesa inaonekana baada ya kuitumikia jamii, na pesa haina thamani yeyote kama itapatikana kwa kuikandamiza jamii kwa namna moja ama nyingine.

Jamii yenye wasomi wanaofikiria thamani ya pesa zaidi ya thamani ya njia ya kupata pesa naifananisha na jamii ya kiafrika, jamii ambayo inawasomi wenye pesa lakini dunia yao haina pesa.
Nakubaliana na kila kitu ulichoandika. Ila hapo unaposema thamani ya hela inaonekana baada ya kuitumikia jamii naomba ufafanue zaidi mkuu. Inawezekana sijaelewa vizuri point yako hapo. Asante sana.
 
Mkuu umeandika vizuri lakini sasa mm ninachojiuliza mbona kuna watu wana elimu wanaitumia effectively lakini bado hawana pesa ? Mfano waalimu wapo wanaofanya kazi kweli kweli tena mfano kama mm huwa nafundisha kweli kweli sipendi kuona mwanafunzi hajaelewa alafu niridhike najikuta natumia muda wangu kuhakikisha ameelewa nilichopanga aelewe lakini kila siku nina shida mpaka basi ,kwa sababu sioni wakuapriciate mchango wangu,unakuta hata daraja unaliangaikia mpaka unakata tamaa.
 
Nakubaliana na kila kitu ulichoandika. Ila hapo unaposema thamani ya hela inaonekana baada ya kuitumikia jamii naomba ufafanue zaidi mkuu. Inawezekana sijaelewa vizuri point yako hapo. Asante sana.
Elimu inampa mtu uwezo wa kuona na kutatua changamoto katika jamii, kufanya hivyo jamii inampa muhusika kiwango cha pesa sawa na huduma yake. Hiki ndio ninacho maanisha.
 
Mkuu umeandika vizuri lakini sasa mm ninachojiuliza mbona kuna watu wana elimu wanaitumia effectively lakini bado hawana pesa ? Mfano waalimu wapo wanaofanya kazi kweli kweli tena mfano kama mm huwa nafundisha kweli kweli sipendi kuona mwanafunzi hajaelewa alafu niridhike najikuta natumia muda wangu kuhakikisha ameelewa nilichopanga aelewe lakini kila siku nina shida mpaka basi ,kwa sababu sioni wakuapriciate mchango wangu,unakuta hata daraja unaliangaikia mpaka unakata tamaa.
Ndio maana mwanzo nikaandika kila maamuzi yanayofanyika (bila kujali ubora wake) lazima yawe na effects katika jamii.

Mwalimu na wafanyakazi mwingine wanaishi kwa taratibu zilizowekwa na wasomi wengine. Kama msomi anaepewa dhamana ya kuweka taratibu hazingatii thamani ya huduma ya mtu, walio wekewa taratibu hizo lazima wawe affected.
 
Elimu inampa mtu uwezo wa kuona na kutatua changamoto katika jamii, kufanya hivyo jamii inampa muhusika kiwango cha pesa sawa na huduma yake. Hiki ndio ninacho maanisha.
Jamii nayo inaangalia value au thamani ya huduma. Kama kuna watu kadhaa wanaotoa huduma hio kwa kiwango sawa, jamii itafuata yule mwenye bei ndogo zaidi. Watu wanaanzisha biashara ila zinakufa sababu ukiuza bei ya chini, faida hakuna. Ukiuza bei ya juu, wateja hakuna. Hasa kwa biashara mpya inakuwa hivyo. Biashara za muda mrefu kwa asilimia kubwa wameshajua namna ya kutunza wateja.

Kwa hio ni kweli, jamii ni muhimu. Lakini changamoto kwa wengi ni kuwa na huduma ambayo jamii wataipenda sana, bei wataikubali, na ww utapata faida nzuri. In such a situation, everybody wins.
 
Kama unapata elimu na haikuwezeshi kuwa na fedha bado elimu haijakusaidia. Watu wengi wamesoma sana ila wanafeli kuzitumia elimu zao kuyamudu mazingira ili wapate mahitaji muhimu.

Actually waafrika wengi hawajui kwanini wanasoma au naweza sema kwamba asilimia kubwa ya africans wanasoma ili wapate ajira then wapate pesa hakuna kingine zaidi ya hapo.
So hapo ukiangalia kwa makini utakutana na ubinafsi pia umasikini.

Na mpaka hapo inamaanisha mtu huyo hajitambui.

Utakuta mtu ni amesomea physics.
Amesoma physics ili akaajiriwe means akikosa kuajiriwa basi atakufa masikini.
Na ukiangalia kwa makini kwenye jamii na mazingira yetu kuna vitu vingi vinavyohitaji utatuzi kwa kutumia hiyo physics.
Sasa kama mtu huyo angejua kwanini amesoma, angekuwa sio mbinafsi na asingekuwa na tamaa ya pesa za faster.
Basi lazima angeitumia elimu yake kutatua changamoto za jamii na mazingira na ukishatatua changamoto lazima faida irudi ambayo ni pesa.
Bty huwezi kutatua changamoto yoyote kubwa bila kuwa na pesa ya kutosha considering wewe ni masikini.
Na ukiangalia kwa makini wasomi wetu wengi hawawezi kuanzia chini sababu hawajitambui wanategema kupop-up na utajiri kama Facebook ads.

Well hapo ukikosa ajira basi unakufa masikini na vyeti vyako kabatini panya wakivifanya dinner.

Kuna vyanzo vingi vinavyofanya wasomi wa kiafrika wafe masikini ila nikianza kuandika sitomaliza sababu kila chanzo kinazalisha chanzo kingine.

Ila solution ni kufundisha wanafunzi kuhusu kutatua changamoto zinazotuzunguka kwa kutumia elimu means hapo ni kuchange education system yote.
Pretty sure that's not gonna happen considering walimu wenyewe nao walisoma ili waajiriwe wapate pesa.
Matokeo yake serikali haiwezi kuajiri kila mtu na hao wasomi kufa masikini na kuwa mzigo kwa taifa.
 
tatzo sio kubadilisha elimu kuwa pesa tatzo ni shule azifundishi elimu na hazijui maana ya elimu. elimu sio cheti, elimu ni kile unacho jifunza kila siku ndo maana wanafunzi weng elimu zao ziko kwenye vyeti unakuta mtu ukimuuliza unaelimu gan et nina degree, nina masters afu yuko ana landa landa mtaani kuna aina tatu za education
scholastic education. - hi ni elimu inayo kusaidia kujua kusoma kupiga hesabu za kawaida n.k yan inshort ni elimu ya msingi ya umuhimu sana kwasababu inatumika katika maisha ya kila siku
proffessional education.-hi elimu unasome kitu flan kama udaktari , huandisi, hualimu n.k
kuna elimu ya tatu ambayo hutakuja kuiona inafundishwa shuleni
Financial education.- hii ni elimu ya fedha utajifunza jinsi ya kupata fedha,jinsi ya kutunza fedha na jinsi ya kuzalisha fedha
kwanamna nyingine hio proffesional education imewakilishwa kwa mfumo wa chet ina maana uwe na cheti ili upate ajira afu ukishapata ajila ili upate fedha utakuta inaingia kwenye financial education kipengele cha tatu( jinsi ya kupata fedha)
swali linakuja vipi kama ajira hamna apo ni sawasawa unabeti na serikali
kwaiyo ukitaka kufanikiwa hakikisha unapate elimu sio shule kama watu wanavoamini ni kuwa na cheti hio sio elimu nenda google search maana ya education utajua maana yake hukuti cheti wala ajira
elimu ni ile inayokusaidia future yako ikiwemo kwenye upande wa uchumi bila ata kumtegemea mtu sijui serikali
yani your brain is your certificate na wala sio karatasi

kwa ushauli ukitaka ufanikiwe unatakiwa ujue elimu ya fedha
 
Back
Top Bottom