Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Nakubaliana na waziri mkuu Pinda kwamba nchi hii lazima iongozwe kwa sheria,kinyume chake kama sheria haifuatwi hasa na viongozi wenye dhamana kunaweza kukatokea machafuko makubwa. kwa hiyo, napendekeza tuangalie mazingira yaliyo sababisha waziri mkuu afikie hapo ndipo tuamue kumshtaki au tumsamehe. Hebu tuangalie mifano michache ambayo inawezekana ndo imemkera sana waziri mkuu mpaka akatoa kauli hiyo tata;
1)Serikali imeshasema na sote tunakubali kuwa madawa ya kulevya ni mabaya sana kwa vijana wetu. Madawa haya yanaua vijana wetu na kufifisha nguvu kazi ya Taifa letu. Lakini wapo watz tena wengine viongozi wakiwepo wabunge na mawaziri wanaohusika na biashara hiyo. Kama Pinda anataka wauza madawa ya kulevya wapigwe na polisi suing mkono hoja ya kushtakiwa nashauri tumsamehe, kwa awamu hii tu.
2)Wako watanzania wengi sana waliopoteza maisha yao ktk mikutano ya hadhara ya vyama ktk mazingira ya kutatanisha inayowahusisha vyombo vya dola yakiwepo mabomu ya Arusha. Kwa mujibu wa katiba, na katiba iko wazi, kukitokea kifo cho chote chenye utata Rais ataunda tume kimahamaka ya majaji kuchunguza tukio hilo. Na viko vyama vilivyoomba Tume ya kimahakama ya majaji iundwe kwa mujibu wa katiba. Bahati mbaya SANA Rais amekataa kuunda Tume hiyo na vifo hivyo viko vingi sana. Sasa, kama Pinda ana uchungu na vifo hivyo, na ameshindwa kumwambia bosi wake moja kwa moja, badala yake anataka polisi indo wampige bosi wake ili aunde tume husika ya kuchunguza vifo hivyo tata, nashauri tumsamehe Pinda.
3)Wako watu waliomteka Kibanda, wako waliomwua Mwangosi, na wapo waliomteka Dr Ulimboka akiwepo Ramadhani Ighondu, na wapo waliomwagia Kubenea na Mzee Tegambwage tindikali. Sasa haya mambo yamemkera sana Pinda, amesarika sana na ameghaflika. Inawezekana kabisa Pinda anataka Ramadhan Ighohundu na wengine waliohusika na mateso, utekaji wa namna hiyo wapigwe na polisi. Kama huu ndo mtazamo wa Pinda naomba tumsamehe.
4)Wiki hii kuna mabinti wawili wa secondary walivamiwa na kubakwa na watu wasiofahamika ktk ‘gheto' au chumba chao. Mmojawapo alishindwa kustahimili akajiua. Jambo hili limesababishwa na viongozi waliofisadi pesa zetu za kujenga mabweni mpaka watoto wote wa sekodnary nchi nzima wanapata madhila makubwa sana ukiwepo ubakaji. Kama Pinda anataka viongozi waliosababisha kutokuwepo kwa mabweni wakiwepo mawaziri wahusika na huyo mbakaji wa watoto wapigwe na polisi, naomba tumsamehe Pinda, walau mara moja tu.
5)Wako wanaotuhumiwa kuua tembo na kuiba nyara za serikali. Mbaya zaidi ripoti za serikali inasema tembo wetu wataisha ndani ya miaka 7 ijayo kama ujangili hautathibitiwa. Kati yao yupo katibu mkuu wa ccm Abdulrahamani Kinana. Sasa kama Polisi aliwalenga majangili hao akiwepo kinana tutafakari upya kabla hatujamshtaki.
6)Wiki hii mimi na baadhi ya madiwani kutoka Mbulu na Babati tunafuatilia sakata la Watz zaidi ya 90 kutoka Manyara na Arusha wengi wao wairaqw na Wamasai waliohamia Tanga na Morogoro ambao wamefukuzwa na viongozi wa serikali kama wezi. Mbaya zaidi mtu amekaa hapo zaidi ya miaka 10, anapewa masaa 24 yeye na watoto walioko shule na mifugo waondoke ktk muda huo. Wengi wakashindwa kufanya hivyo, wakaswekwa ndani. Sasa Pinda akiagiza viongozi wa namna hiyo wapigwe na Polisi napendekeza tumsamehe.
7)Wanafuzni wetu wa kidato cha nne wamefelishwa sana kwa maelfu,- sijasema wamefeli, mpaka kidato cha sita na vyuo kuna hatari ya kukosa wanafunzi mbeleni. Hii ina maana kwamba mabilioni ya fedha za kuwasomesha watoto waliofeli yamepotea kutokana na uzembe wa viongozi wakiwepo mawaziri wa Elimu Mulugo na Kawambwa. Kwa maoni yangu, kama Pinda aliwalenga viongozi wote na mawaziri hao tusimshtaki kwanza kwa sababu anawalilia wanafunzi waliojiua baada ya kufeli na ana uchungu na wazazi waliopoteza fedha zao kulipia ada na gharama nyingine. Kwa hiyo, kama Pinda anataka Kawambwa na Mulugo wapigwe, tusimshtaki kwanza, Tumsamehe.
8)Wiki iliyopita gazeti la Jamhuri liliibika na ufisadi wa Mabilioni ya shilingi yaliyoibwa na viongozi wa serikali wakati wa mkutano wa smart partnership uliofanyika mwezi uliopita jijini Dsm. Katibu mkuu Kiongozi aling'aka akakwama. Polisi badala ya kuwahoji mafisadi wakawahoji Deo Balile na Jacktona Manyerere. Sasa kama Pinda anataka viongozi walioiba fedha zetu wapigwe, nashauri tukae naye kwanza tujadiliane naye ili tumwelewe.
9)Wako Viongozi waliopanga kuwadhuru Viongozi wa Chadema na wapo waliotumia mitambo maalum kuingilia mawasiliano yao ili kuwabambikiza kesi, wako waliomwekea mmojawapo kifaa cha kunasa mawasiliano yake Dodoma. Wako waliotaka kuwaua baadhi ya viongozi wa chama hicho. Wapo wahuni waliowapiga wabunge wetu 2 kule mwanza na kuwaumiza sana. Kama Pinda analenga hawa wavunja amani ya nchi yetu, kwa kweli hatumtendei haki Pinda tukimshtaki bila kumsikiliza.
10)Wako watz magezezani waliobambikiwa kesi za uwongo na Polisi. Waziri Nchimbi amekri hivyo na Mbunge Lema alikutana nao huko gerezani akaleta na mifano hai ya hizo kesi na ushahidi wa ubambikaji wa kesi hizo. Hii ina maana kwamba kuna wajane na wagane mitaani kwa sababu wenzao wanatumiki vifungo feki. Watoto wao wamegeuka watoto wa mitaani. Sasa, kwa kweli kama Pinda anataka polisi wawapige hao watu na hasa polisi wanaobambika kesi wapigwe na polisi wenzao , basi tumfikirie kwanza Pinada kabla ya kumshtaki.
11) Wako mafisadi ambao Pinda alishasema hawashitakiki mahakamani kwa kuwa ukiwashtaki nchi itatikisika. Wako mafisadi wa EPA, Buzwagi, Richmond nk. Sasa kama Pinda ameona kuwa kwa kuwa hatuwezi kuwashtaki tuwaruhusu Polisi wawapige, napendekeza kabisa tumsamehe Pinda kwa sababu madhara ya matrilioni yaliyoibwa na hao watu ni makubwa sana kuliko kichapo watakachopewa na Polisi.
Hata hivyo, kwa kuwa Pinda ndo aliyeagiza wasiotii sheria wachapwe itakuwaje kama yeye mwenyewe akivunja sheria naye achapwe. Maana yeye pia aliwahi kudanganya Bunge kuhusu sakata mauaji ya Arusha la January 5, 2011 na amegoma kujizulu. Lema alipeleka ushahidi wa jinsi Pinda alivyolidanganya Bunge LAKINI Spika ameamua kumpotezea Lema. Au tuseme kwa kuwa yeye ndo aliyeagiza wavunja sheria wachapwe yeye asichapwe na polisi kwa kulidanganya Bunge?
Hata hivyo, kama Pinda anataka watazania wanaolalamikia na kuandamana kwa sababu nilizotaja hapo juu ndo wapigwe na Polisi naomba niwapongeze LHRC NA TLS kwa kazi nzuri ya kumfungulia kesi na Jumapili nitawaombea kwa Mungu wasitolewe Meno na kucha Bila ganzi ili Mungu awalinde.
Ni mawazo yangu tu, maana naipenda nchi yangu Tanzania, sina nyingine